Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 22,989
- 27,926
ITAKAPOBAINIKA ni BORA AKAJIENGUA auAKAFUKUZWA KULIKO KUFICHA UCHAFU ULIOOZA
Nakuunga mkono Kurugenzi ya habari imelala ama ni kama hawatambui wajibu wao sitegemea Dr.Kujibu tena vitu vya aina hii.Wakati mwingine ni bora kuambiana ukweli.Dr.W.Slaa
===>Mleta mada hajakosea hata kidogo,ichukueni hii kama taarifa na muifanyie kazi
===>Kama huyo Bwana yupo na mmemuajiri na mkigundua kuwa ana makosa mumuondoe kwenye hiyo nafasi
===>Jitahidini kufanya kazi kitaalamu kidogo,kabla ya kuajiri watu angalau mfanye ka "Vetting hata kadogo tu" si mna kitnego cha usalama?kazi yake ni nini?mojawapo ya majukumu yake ni kuangalia watu wa kuajiri.
===>Mnalalamika kila siku kuwa kuna watu wanavujisha siri za chama,kama hamna utaratibu wa kuajiri mnategemea siri zisivujue?
===>Nina wasiwasi na majibu ambayo siku hizi umekuwa ukijibu hapa JF,nina wasiwasi kama unajibu wewe mwenyewe,kama kuna Admin umempa asimamie acc yako hapa JF mwambie akuulize nini cha kujibu kabla hajakurukupa,haya majibu sio mazuri na hayajitoshelezi kabisa.
===>Kurugenzi ya habari ya CDM inafanya kazi gani?au bado wamelala mpaka saa hizi?wao ndio wanawajibika kujibu vitu vidogo vidogo kama hivi.
kajambe ulale huna hoja
Wana JF,
Nilisha eleza matatizo mengi waliyonayo Chadema, siku nyingi kuanzia;
1. Chama chenyewe (Chadema)
2. Aina ya Uongozi wao (Kidini/Kikanda)
3. Utawala (Ajira zao)
Hata 'delegation of power' kwao hawa jamaa ni matatizo. Hilo la Mhasibu ni moja tu yako mengi hayafai ndani ya CDM.
Lakini tuwape muda, watapita kama wengine walivyopita.
NKUU SINDE
Heshima yako Dr,
Mimi sikukosoi ila nakushauri tu kuwa siku nyingine ungemjibu mleta mada kuwa mhasibu mkuu wa chadema ni nani na aliajiriwa kwa vigezo vipi
Je nafasi ya kazi ilitangazwa?
Kama ilitangazwa, kwenye gazeti lipi?
Pia tungependa kujua kama unamfahamu huyu mtu anayeitwa Mwaluisi tafadhali.
Nadhani majibu hayo kama yangetolewa ungekuwa ndio mwisho wa hii thread ....
Janjaweed,
Mhasibu Mkuu ni lazima atakuwa ameajiriwa. Ili wana JF wakuamini weka ushahidi wa kuajiriwa kwake kwa nafasi ya Mhasibu Mkuu. Vinginevyo ni propaganda. Aidha Kama ni kweli amevurunda kwenye Halmashauri nyingi na baado yuko mitaani, waziri wa Tamisemi ni kwanini asijiuzulu kwa uzembe?
pia nafikiri dr slaa ni kheri ungekaa kimya kuliko kuja kujibu majibu mepesi mepesi,hata nami bado cjakuelewa,wajibu wana jf ni mkweli uyo mtu ni mhasibu mkuu? ni kweli ameajiriwa? je ni kweli uyo mtu ni mwizi? maana naamini kabla haja ajiliwa mlimchunguza kwa umakini ko mnataarifa zake sahihi,haya ndo ulipaswa uyajibu,na kusema kurugenzi ya hbr ndo ijibu mbona umechangia thread wkt ww ni m2 mkubwa mwenye majibu,ndo maana 2nasema ni kheri ungekaa kimya,pia makene na mnyika mkwapi kujibu hili mbona post zikiwahusu mnajibu haraka sn?
Dr. Slaa, jibu lako ni zuri, lakini pia sio zuri
ili mtu aajiriwe ni lazma awe vetted, hivyo naamini mlifanya vetting, pamoja na hayo, tena hasa kwa wahasibu, inapotokea mengine yanaibuka basi mwajiri hufanya chunguzi haraka, mimi kama mwajiri hufanya hivyo
kuhusu mimi kuweka ushahidi, nadhani umepotoka, aliyeleta mada sio mimi, ila nimechangia tu.... Tena wewe uko best placed kusema endapo ni mwajiriwa wako, katika hiyo nafasi au nyingine yoyote chamani
Kuhusu kujiuzulu kwa waziri wa tamisemi, je unazungumzia waziri gani? Inakuaje endapo huyu bwana alikua tamisemi miaka ya nyuma na si chini ya waziri wa sasa? Vipi mfumo wetu...unaoufahamu vizuri,would you rush to judge waziri au katibu mkuu wa wizara.?
Swali la mwisho.... Unamtetea huyo bwana au vipi?
i smell something bad here
Dr. Slaa, jibu lako ni zuri, lakini pia sio zuri
ili mtu aajiriwe ni lazma awe vetted, hivyo naamini mlifanya vetting, pamoja na hayo, tena hasa kwa wahasibu, inapotokea mengine yanaibuka basi mwajiri hufanya chunguzi haraka, mimi kama mwajiri hufanya hivyo
kuhusu mimi kuweka ushahidi, nadhani umepotoka, aliyeleta mada sio mimi, ila nimechangia tu.... Tena wewe uko best placed kusema endapo ni mwajiriwa wako, katika hiyo nafasi au nyingine yoyote chamani
Kuhusu kujiuzulu kwa waziri wa tamisemi, je unazungumzia waziri gani? Inakuaje endapo huyu bwana alikua tamisemi miaka ya nyuma na si chini ya waziri wa sasa? Vipi mfumo wetu...unaoufahamu vizuri,would you rush to judge waziri au katibu mkuu wa wizara.?
Swali la mwisho.... Unamtetea huyo bwana au vipi?
i smell something bad here
Aah kwani si ndio huyu mwaluisi alikuwa anamgegeda hawa ngulume mpaka vi futa jasho vyote vya yule mama huyu jamaa alivimaliza akahakikisha familia ya ngulume imebaki patupu tunamjua sana amezunguka humo tamisemi sana kila alikokwenda aliwapiga huyo jamaa ni noma na dr lazima utete hili kwani hata wewe sio msafi kipesa.
Akirudi kujibu hoja hii... nampa kura 2015
Dk Slaa hapaswi kuja hapa kuthibitisha kama aliyetajwa ni mwajiriwa wa Chadema au la, wa kuthibitisha ni mwenye kuteta tuhuma hiyo, na ndio kanuni za ushahidi, hata hivyo kuzungumzia kwamba kuna uzembe katika Tamisemi, tukiwatetea tamisemi basi tuichukulie hatua serikali kwa sababu waziri anaweza kubadilishwa lakini kwa miaka yote tumekuwa tukiongozwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi inayobadilisha mawaziri wasiochukua hatua. Tusipoona tatizo kwa Waziri basi tuone tatizo kwa Chama kinachounda serikali isiyochukua hatua
Sio lazima uchangie mkuu.