Huyu Mpoki vipi jamani?

Huyu Mpoki vipi jamani?

Kwa hiyo watu wakitukanwa wewe ndiyo umetekenywa

Kutukanwa au kuambiwa ukweli kuhusu yale wanayofanya ili kama ni mabaya wajirekebishe kama ni mazuri waongeze bidii. Hamataki kuambiwa ukweli, manataka kusisfiwa tu, hata pale mnapokuwa mmekosea, mimi ingawa sikuwepo ukumbini, lakini pamoja na picha za startv kuwa na rangi rangi, nilichelewa kulala lengo kubwa likiwa ni kumsikiliza Mpoki alivyokuwa anawachana mmoja baada ya mwingine, utavaaje viatu virefu bila kufanya mazoezi ya kutembea navyo ?
 
Vanessa Mdee alipotaka kuanguka na High heels zake,jamaa akamkandamiza eti hivo viatu vilitakiwa viwe na sticker ya Learner,mpoki ni mjinga sana hahahaaa
 
si uende nini kinakuzuia!!!!!

Nina ticket moja hapa ya bure, changamkia fursa ni PM sa ivi.

Halafu ingependeza zaidi ungeandika " kwa hiyo unayo haki ya kuzuia wengine kutoa mawazo yao " hayo mengine sijui AIR THEIR VIEWS waachie mwenyewe kina ngoswe .ni mtazamo tu usinitoe roho

ah ah ah ah imebidi nicheke tu mkuu. huu ni uwanja huru bana wewe unaweza kuwa umeona, umesoma au umeandika uzi amabao mwenzako hajafanya hivyo. so uungwana ni kumuelekeza wapi akaone basi
 
lakin hakuongea kitu kibaya wala cha uongo

alikuwa anawafundisha mabishooo waache ubishoo. siku nyingine ukiingia katika hafla kama hiyo alafu ukamkuta MPOKI ndani ya mjengo inabidi ujipange jinsi ya kujiachia maana akikuona tu umekaa kibishoo lazima akupe zako.
 
Vanessa Mdee alipotaka kuanguka na High heels zake,jamaa akamkandamiza eti hivo viatu vilitakiwa viwe na sticker ya Learner,mpoki ni mjinga sana hahahaaa

me nimempenda sana kwa ajili ya mabishoo
 
mpoki alikuwa aawaweka watu sawa waache ushamba wao. hebu fikiria yule mdada hata jinale simjui kaingia na kiswanglishi chake paleeee ah! mpoki nae hakumlazia damu akampa zake... kumbe ni mparreee!!! wa kuleee... me nilidhania ni katoka ulaya kumbeee paree loh!! MPOKI NDIO DAWA YA MABISHOO. tena next time itabidi wamuite na JOTI waungane ndio itanoga sana.
Walewale kina mpoki ndiyo nyie ..nani alikuambia mtu akitoka Ulaya ndiyo anaongea English .Nyie ndiyo wale anaongea KIZUNGU :der:
 
Jamaa juzi siku ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards alikuwa kama vile anatania lakini vile vile alikuwa anaboa sana, hata kama ni msanii hapana alikuwa too much,

Alimwambia mama mmoja kuwa "Anafaa kwa matumizi ya binadamu"

Then akamwambia wema sepetu "Alinyangw'anywa penzi na akalirudisha"

Alipokuja RAY, kama vile Ray alianza kupatwa na wasi wasi sana asijue mpoki atasema nini juu yake, jamaa akamchana kuwa "Kuna maneno mtaani kuwa umeachana na Johari"....RAY alionekana kuogopa sana jamaa asiendelee kumchana.

Akaja Hashim Lundenga "Mpoki alimchana indirect, kuwa ni mtu aliyeweza kuvumbua vipaji vya wasichana....alitaka kutamka jambo hapa yule dada akamuwahi...

Alipokuja LULU Michael...hapa aliona aibu kidogo, hata mimi nilikuwa nasali sana asiropoke jambo lolote kuhusu Lulu....

Waadaaji wa tuzo walipotoka sana; badala ya kumuita msanii mshereheshaji wao wakaangukia kwa msanii mropokaji hovyo; mpoki ni kesi ya Mirembe hospitali yule! hakika aliembarass watu wengi sana mpaka hata wengine ambao hawakuwepo ukumbini kwa kuhofia atakachomropokea mtu!.

halijui kwamba watu wengine wako sensitive sana haswa kwenye public kama pale! sio kila mtu ni kamikaze au Al shabab kama lenyewe; watu wengi wanapenda kusitiriwa hadharani hata kama wanajua wana makosa fulani fulani!
Organisers wa Kili music awards; angalieni sana hiyo gaffe, mwaweza kuishia mahakamani na kulipa damages next time around
 
Akammaliza kabisa na Martin Kadinda,eti mkiwa mnakula mayai mnapiga picha mnaweka instagram oohh ndio tunapata breakfast,kwani huwa hamli mihogo???
 
Vanessa Mdee alipotaka kuanguka na High heels zake,jamaa akamkandamiza eti hivo viatu vilitakiwa viwe na sticker ya Learner,mpoki ni mjinga sana hahahaaa

hahaaaaa kumbe alisema viwekewe sticker ya learner hahaaaahahaaaaaaaaaa

pozi la L kwenye high heels hahaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kutukanwa au kuambiwa ukweli kuhusu yale wanayofanya ili kama ni mabaya wajirekebishe kama ni mazuri waongeze bidii. Hamataki kuambiwa ukweli, manataka kusisfiwa tu, hata pale mnapokuwa mmekosea, mimi ingawa sikuwepo ukumbini, lakini pamoja na picha za startv kuwa na rangi rangi, nilichelewa kulala lengo kubwa likiwa ni kumsikiliza Mpoki alivyokuwa anawachana mmoja baada ya mwingine, utavaaje viatu virefu bila kufanya mazoezi ya kutembea navyo ?
Nasikia harufu ya chuki chuki hapa au yaweza kuwa joto hasira si bure
 
Walewale kina mpoki ndiyo nyie ..nani alikuambia mtu akitoka Ulaya ndiyo anaongea English .Nyie ndiyo wale anaongea KIZUNGU :der:

ngoja kwanza we MZUSHI TU!! usipayukepayuke wewe kabila gani?? au ndio walee wapareeee!! hivi uliumia sana siku ile madongo yalikushika vizuri etieee.. kama alikuwa ankuzingua si ungezima tv yako au ungebadilisha stesheni... maana najua hukuweza kuhudhuria kwa sababu kadha!! hahahaaa
 
kwa taarifa yenu msiokuwa na dogo.. MPOKI NI COMEDIAN kwahiyo mambo ilibidi yaende vile.. najua wengi wetu tulifurahi sana siku hiyo wachache sana ndio walijifeel vibaya ukiwemo na wewe ambae umeangalia kwenye tv tu afu eti unanuna kwani MPOKI Alikuonaa?? au alikutaja!!!
 
Nasikia harufu ya chuki chuki hapa au yaweza kuwa joto hasira si bure

Mkuu labda wewe ndio mwenye chuki chuki, miye anunga mkono ukweli ukweli uliokuwa unasemwa na Msanii Mpoki kwa wahusika. Kama alikuudhi, mbona hukuvunja tv set uliyokuwa unaangalia.
 
Mkuu labda wewe ndio mwenye chuki chuki, miye anunga mkono ukweli ukweli uliokuwa unasemwa na Msanii Mpoki kwa wahusika. Kama alikuudhi, mbona hukuvunja tv set uliyokuwa unaangalia.

kamanda huyu MZUSHI kama lilivyoovyo jinale... ndio anaonekana m'binafsi na mwenye chuki binafsi.. sasa yeye kinamuuma nini au yule mparreee ni jamaa yake?
 
Hii mada tulishaimaliza kitambo kuwa Mpoki ni Janga katika sanaa.full stop

Teh..teh..teh..kwanza nianze kwa kucheka kumchulia seriuos mchekeshaji kama mpoki na kutokwa na povu kumsema mpoki utafikiri wewe ndio uliotaniwa hapo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, kwani wewe mpoki ndo ulimjua juzi?. Binafsi bila yeye usiku ule ungekua unaboa na kupooza kupita maelezo!! Mwakani wampe shavu tena!! Ha..ha..ha..bravo mpoki
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom