Huyu Mchungaji, anafanya uchochezi au anatimiza wajibu wake kiimani?

Fascinating

Member
Joined
May 14, 2025
Posts
93
Reaction score
224
Wakuu nimekuta na hii video sehemu, Mchungaji anawasimanga vijana na kuna mahala anaenda mbali zaidi mpaka kusema Vijana hawezi hata kudai haki, wakipewa Elfu 5 tu wavaa T-shirt.
Hii mijadala ya dini na siasa imekuwa yakawaida sana hivi karibuni na mpaka wa Viongozi wa dini kuonekana wanafanya siasa au wanatimiza wajibu wao umezidi kuwa mwembamba kutokana namna watu wanaodhani vinginevyo kuwa na tafsiri nyingine.

Video hii hapa chini iliibua mjadala kijiweni kwangu jana, kulikuwa na mgongano wa maoni juu ya aina hii ya mafundisho, baadhi wanayachukulia kama itikadi kali na wengie wanaona ndio mafunzo sahihi vijana wanayotakiwa kuyapata ili kuwe na jamii yenye haki na usawa.

Maoni ya waliosema Mchungaji yupo sahihi yalikuwa yanaungwa mkono na sehemu kubwa. Ufafanuzi wa wagu wa upande huo ulitumia wigo mpana sana wa imani tofauti, Agenda yao kuu ilikuwa Kudai na kulinda haki ni msingi wa wa kila imani ya dini na kuwa kwenye dini nyingi duniani, mafundisho ya jamii yenye haki na usawa si mageni.
Nimejaribu kwenda kuangalia ukweli juu ya hoja yao na kupitia imani tofauti za Ibrahimu (Abrahamic) na Zisizokuwa na Asili hiyo (Non Abrahamic) nimeweza kupata hili jeduwari.

Mwelekeo wa Kimaandiko Juu ya Kudai Haki
DiniMsingi wa HakiWajibu wa Kudai Haki
Dini za Ibrahimu (Abrahamic Religions)
UkristoTabia ya Mungu na Upendo kwa Jirani. Haki huonyeshwa kwa kusaidia walio hatarini.Waumini wanatakiwa "kutenda haki" (do justice) kwa vitendo, si maneno tu. Hii inajumuisha kuwatetea yatima, wajane, na maskini na kupinga ukandamizaji (Isaya 1:17; Luka 4:18).
Ni wito wa imani unaowaweka waumini katika nafasi ya kuwatumikia walio wadogo.
UislamuAmri ya Mwenyezi Mungu na Usawa wa Watu (Tawhid). Haki ni nguzo ya utawala wa jamii.Waislamu wanatakiwa kuwa "wasimamizi madhubuti wa haki" (firmly established in justice).
Hii inamaanisha kutoa ushahidi wa kweli na kuhukumu kwa usawa bila kujali vyeo, utajiri, au uhusiano wa kifamilia. Kudai haki ni faradhi (wajibu) hata dhidi ya mtu mwenyewe (Qur'an 4:135).
Dini Zisizo za Ibrahimu (Non-Abrahamic Religions)
UhinduDharma (Wajibu wa Maadili/Sheria ya Maumbile). Haki hurejesha utaratibu wa ulimwengu (cosmic balance).Waumini, hasa viongozi na wafalme (kama ilivyoelezwa katika Dharma Shastras na Mahabharata), wana wajibu wa kulinda Dharma na kusimamia Nyaya (haki). Kudai haki huja kwa njia ya kutawala kwa uadilifu, kuadhibu waovu, na kuhakikisha ustawi wa raia wote.
UbuddhaHuruma (Karuna) na Kuepuka Kudhuru (Ahimsa). Haki ni upanuzi wa maadili ya kimsingi.Waumini wanadai haki kwa kupitia Maisha Sahihi (Right Livelihood) na Vitendo Sahihi (Right Action). Hii inajumuisha kukataa biashara na kazi zinazodhuru wengine (mfano: uuzaji wa silaha au ulevi) na kufanya kazi kusaidia kupunguza mateso katika jamii. Udai wa haki unatoka katika msingi wa Karuna (huruma).

Kwa upande wa waliokuwa na mtazamo kuwa Mchungaji hakuwa sahihi na kwamba mafundisho yake yanaweza kuwa na viashiria vya kuchochea vurugu walikuwa wanadharia zilizojikita kwenye kuheshimu mamlaka za duniani na za mbinguni...

Kwa upande wangu sikuweza kushawishiwa sana na watu wa upande huu.... ila sitaki kuwa na maoni ya watu wa upande mmoja pekee, hivyo nimeamua kuileta hii mada hapa ili nilisikie maoni ya wadau wengine lakini pia ningevutiwa zaidi kusikia upande wa wenye mtazamo kuwa Mchungaji alikuwa anatoa mafundisho ya kichochezi.
 
View attachment 3480371

Hachochei vurugu bali anakemea mambo ya kishetani. Kumpigia kura mgombea kwa malipo ya baiskeli, nyama, wali, t-shirt, etc. ni tabia ya kishetani.

In sum, anataka vijana wafanye kazi kwa uwezo wao wote na muda wote wasimame (fearlessly) upande wa haki. Huu sio uchochezi.
 
Back
Top Bottom