Huyu JK vipi???

[/B]

Kuweni wavumilivu watanzania, Rais wenu hana experience kwenye post yake ya sasa, hajawahi kuwa Rais before kwahiyo on job training haiwezi kukwepeka hapa!

Wakudata! Kwanza huyu rais ni wa kwako pia! So ni 'rais WETU' not 'rais wenu' Pili, hakuna mtu ambaye alikuwa ana expereince ya kuwa rais and that's what advisors are for. Ndiyo maana kuna speechwriters na madudu yote. Sasa kama unaamua kwamba huhitaji mwongozo unaenda kujiongelea tu na kupayuka hovyo ujue hakuna wa kukutetea. Nyie fanyeni mchezo kuna siku atadeclare vita na nchi nyingine kimzaha tukajikuta tuko vitani! ohooo!
Mi nimechoka kuambiwa eti tumpe muda eti anajifunza.
Whatever qualms we may hve about BWM lakini jamaa alipoingia kazini alijua what to do na alichapa kazi esp miaka 5 ya mwanzo!
Mwungwana tatizo ni mtu wa pwani katuliiiia anajua yuko na mabesti saa zote!
 
Susuviri unajuaje kuwa alikua 'anapayuka'? na alikua hasomi speech iliyoandaliwa? Labda hapo speech writer wake ndo kajipinda kikwelikweli na mkuu mwenyewe akaona iko bomba?
 
Jamani mi niliwaambie mkaniona nina mipasho. Our handsome president is a national burden. He is a shame, no wonder he is in the list of shame. Ukiwajua mafisadi ukawachunia na wewe ni fisadi tu. Rais gani anavunja sheria za nchi kwa kuficha wahalifu? Polisi wanasubiri nini kumkamata kuisadia polisi? Leo mimi nikitoka nikasema namjua fulani aliyemuua fulani Asha mie nitaozea mahabusu nikiisadia polisi. Nawaombeni jamani mumkamate Jakaya Halfani Mrisho Kikwete; yeye anawajua wahalifu wote- wauza unga, wanaotia mimba watoto washule, wanafuja fedha za miradi, wala rushwa wakubwa, wanaosambaza virusi vya ukimwi kwa makusudi wote anawajua. Akamatwe aisaidie polisi, na apandishwe kizimbani kama shahidi namba moja. Si anawajua jamani?
 
Habari zaidi endelea hapa

"Vitisho vya kitoto" vya aina hii ungeweza kuvitarajia kutoka kwa kiranja wa darasa kule shule ya msingi,kwamba "atakayeendelea kupiga kelele nitamwandika,au kumtaja kwa mwalimu..." lakini sio kwa kiongozi wa nchi tuliyempa wadhifa wa urais.Kwahiyo akishatutajia hadharani kifuatie nini?Tuawazomee?Tuwapige mawe?Au TAKUKURU ndio waamke usingizini kuwachunguza?Hivi huyu mtu hana mtu anayemsaidia kuandaa hotuba zake?Anyway,pengine atakapoamua kutaja hao wanaogawana miradi atatutajia pia na wala rushwa alodai anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Kaaazi kwelikweli

Ndiyo matatizo ya kuweka madarakani watu wasiostahili kuwa madarakani. Wewe kama Rais wa Tanzania una taarifa kwamba kuna watendaji wako wanafanya kinyume na vile ilivyotarajiwa kufanya, basi cha kufanya ni KUWAFUKUZA KAZI! siyo kuanza kuwatisha. Ukishaanza kuwatisha na hatimaye kuwataja hadharani, nani atakayefanya maamuzi ya kuwafukuza kazi!? :confused:

Ndio maana mawaziri wote waliozembea na wana kashfa chungu nzima akina Karamagi, Meghji, Msolla, Magufuli, Mramba na wengineo mpaka leo wanapeta madarakani maana wanajua Kiranja wao hana ubavu wa kumfumkuza yeyote kazi.
 
Susuviri unajuaje kuwa alikua 'anapayuka'? na alikua hasomi speech iliyoandaliwa? Labda hapo speech writer wake ndo kajipinda kikwelikweli na mkuu mwenyewe akaona iko bomba?

Kama imeandikwa na speech writer, basi Muungwana ana akili ya kupambanua baya na zuri na amekuwa madarakani muda mrefu tu kabla ya kuwa Rais. Hakuisoma hiyo hotuba kabla haijatoa kwenye kadamnasi ili kurekebisha makosa kwenye hotuba hiyo!? Au yeye ni kihiyo kwa sababu tu imeandikwa na speech writer basi inabidi itolewe kama ilivyo bila kubadilisha makosa yaliyomo!? :confused:
 
Nyangumi,

Nakuunga mkono 100% maana mtu mwenye macho hawezi kukubali kuongozwa na kipofu kama ambavyo tunajaribu kuonyesha ktk thread hii. Mimi nina macho, naogopa kusema Rais wangu ni kipofu ilhali tulimchagua kwa ushindi wa kishindo.

Nina rafiki Mkenya, siku hizi naogopa kabisa kuongea mambo ya $iasa mbele yake maana siku aliposikia JK kashinda kwa 80% aliiambia wazi kuwa "Tanzanians u'r kidding" (tena akasisitiza kuwa "UTAKUJA NIAMBIA"). Tobaa, kwa mwendo huu soon nitabadili njia tusionane kabisa!! We have to borrow a leaf from our Kenyan brothers, la sivyo tutaendelea kuwa masikini generation to generation!
 
Najaribu kufikiria mwananchi fulani pale mkutanoni aliyekuwa na wazo la kumpelekea JK majina ya viongozi mafisadi, mara rais akabadili kibao na sasa yeye ndio anataka kumpelekea huyo mwananchi hayo majina. Bonge la confusion! Wachora katuni mpo hapo?
 
I want to echo dada Asha Abdala above. Kwa rais kusema kuwa anawajua wahalifu na kuzidi kuwapa muda wa kuzidi kufanya uhalifu wao ni usaliti mkubwa.

Hii inaonyesha ni jinsi gani rais anavyojali kaulimbiu za "Public Relation" kuliko kufanya kazi. What we have is not a political process, rather a tragi-comic farce of epic proportions.

But then again what do you expect from somebody whose track record is full of appeasement and grand corruption and severely lacking in achievement of any sort.

I dare anybody to name one achievement (ukiacha kumtoa nishai Malima which was a politically deadbeat move anyway since he roused CCM's anger).The guy lacked initiative whatsoever, and Tanzanians made him president.

A current Ikulu staff once sarcastically said -just to show you the level of grave nonchalant apathy- That there is a saying he once read at an Amsterdam airport lavatory.

"A Million flies eat shyt, they can't be wrong". Comparing the million flies to Tanzanians, and shyt to the decision of electing Kikwete.Basically drawing the strength of numbers in a ridiculous fashion. It would be funny if it wasn't so tragic.

This guy is currently a speechwriter for Kikwete.Kiwete is the problem, not the solution.If you will vote 2010 make him a one time president afunge vilago kwenda kwao.
 
Baada ya kusikia tafsiri mbali mbali nimekuwa na wasiwasi na JK kama kweli ameisha fanya vya kutosha ningeomba tuweze kuweka mazuri aliyoweza kufanya mpaka sasa hivi maana najua pamoja na kwamba inaonekana kulemewa na mzigo kuna ambayo kidogo amejitahidi kulingana na uwezo wake.

La kwanza kabisa ninaloliona waziwazi ni suala la majambazi wale wa sinza ambalo lilipelekea kukamatwa kwa akina afande zombwe. Hili suala alionekana kufaulu vizuri.

Suala la Pili aliloweza kufaulu ni suala la majambazi yaliyokuwa yametanda kila mahala wakati BWM akitoka madarakani. Hili suala alilishughulikia kwa makini sana na nafikiri kwa asilimia 60% aliweza kufaulu.

Suala lingine limekuwa la kuanzisha vyuo vikuu kama DODOMA university ambavyo pamoja na ukosefu mkubwa wa wafundishaji, lakini amejitahidi kuanzisha hiki chuo ambacho kitaweza kuzalisha wataalamu katika nchi hii.

Suala lingine ambalo nalo amelichukulia bango ni suala la Elimu ya Msingi ambalo pia nimeona ameweza kulifanyia kazi pamoja na kwamba pia lina matatizo makubwa sana ya ukosefu wa walimu ambalo limepelekea kuturudisha ktk kutumia walimu ambao hawakusomea fani hiyo.

Lakini pia mapungufu yanaonekana kuwa makubwa kuliko mafanikio. Masuala mengi sana inawezekana anayafahamu sana na ana ushahidi wa kutosha hila ameshindwa kufunga paka kengele. jamani mimi niliyoyajua ni kama haya ningependa pia kama kuna mazuri ambayo ameisha yafanya pamoja na kwamba kuna ambao wanasema muda bado anajifunza au anajipanga kama alivyowahi kusema waziri Mramba naomba atoe data.
 
Habari zaidi endelea hapa

"Vitisho vya kitoto" vya aina hii ungeweza kuvitarajia kutoka kwa kiranja wa darasa kule shule ya msingi,kwamba "atakayeendelea kupiga kelele nitamwandika,au kumtaja kwa mwalimu..." lakini sio kwa kiongozi wa nchi tuliyempa wadhifa wa urais.Kwahiyo akishatutajia hadharani kifuatie nini?Tuawazomee?Tuwapige mawe?Au TAKUKURU ndio waamke usingizini kuwachunguza?Hivi huyu mtu hana mtu anayemsaidia kuandaa hotuba zake?Anyway,pengine atakapoamua kutaja hao wanaogawana miradi atatutajia pia na wala rushwa alodai anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Kaaazi kwelikweli

Hapa simlaumu JK sana, hiyo inaitwa "scare tactic" wale jamaa pale kawachimba mkwara mzito! kwa hiyo hata hana haja ya kuwatumia wapelelezi wala tukururu hiyo miti hawatagawana wao kwa wao kwa sababu hawajui je atafanya kweli au la na hawatataka ku-take risk, watawapa walalahoi hiyo miti.
 
Baada ya kusikia tafsiri mbali mbali nimekuwa na wasiwasi na JK kama kweli ameisha fanya vya kutosha ningeomba tuweze kuweka mazuri aliyoweza kufanya mpaka sasa hivi maana najua pamoja na kwamba inaonekana kulemewa na mzigo kuna ambayo kidogo amejitahidi kulingana na uwezo wake.

La kwanza kabisa ninaloliona waziwazi ni suala la majambazi wale wa sinza ambalo lilipelekea kukamatwa kwa akina afande zombwe. Hili suala alionekana kufaulu vizuri.

Suala la Pili aliloweza kufaulu ni suala la majambazi yaliyokuwa yametanda kila mahala wakati BWM akitoka madarakani. Hili suala alilishughulikia kwa makini sana na nafikiri kwa asilimia 60% aliweza kufaulu.

Suala lingine limekuwa la kuanzisha vyuo vikuu kama DODOMA university ambavyo pamoja na ukosefu mkubwa wa wafundishaji, lakini amejitahidi kuanzisha hiki chuo ambacho kitaweza kuzalisha wataalamu katika nchi hii.

Suala lingine ambalo nalo amelichukulia bango ni suala la Elimu ya Msingi ambalo pia nimeona ameweza kulifanyia kazi pamoja na kwamba pia lina matatizo makubwa sana ya ukosefu wa walimu ambalo limepelekea kuturudisha ktk kutumia walimu ambao hawakusomea fani hiyo.

Lakini pia mapungufu yanaonekana kuwa makubwa kuliko mafanikio. Masuala mengi sana inawezekana anayafahamu sana na ana ushahidi wa kutosha hila ameshindwa kufunga paka kengele. jamani mimi niliyoyajua ni kama haya ningependa pia kama kuna mazuri ambayo ameisha yafanya pamoja na kwamba kuna ambao wanasema muda bado anajifunza au anajipanga kama alivyowahi kusema waziri Mramba naomba atoe data.

Mimi sijasikia wala kuona mazuri yoyote. Shule za msingi nyingi bado zina majengo ambayo hayastahili kuitwa shule, wanafunzi hawana viti na madawati, hakuna vyoo na wana walimu wachache au hawana walimu kabisa, haya kwangu si mafanikio. The jury is still out when it comes to criminals.

*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Posted Date::12/3/2007
Majambazi yamtumia salamu mpya Mwema

*Yateka, yapora mamilioni mgodini

*Yalewa, yabaka na kuondoka bila hofu

* Baadhi wachimbaji wajinufaisha

*DC Bukombe aamuru mgodi ufungwe

Shija Felician na Suzy Butondo,Bukombe
Mwananchi

KUNDI la majambazi yakiwa na bunduki juzi yaliwateka wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu katika machimbo mapya ya Nyakasaluma wilayani Bukombe na kisha kuwapora vitu mbalimbali vikiwemo dhahabu na fedha taslimu.

Habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Stansilaus Mulongo, zinaeleza kuwa majambazi hayo yaliyokuwa zaidi ya 20 yakiwa na bunduki kila mmoja ambayo mbali ya kupora pia yalibaka baadhi ya wanawake waliokuwa katika eneo hilo, yaliingia katika machimbo hayo saa 2:00 usiku na kuondoka saa 9.00 usiku bila kukamatwa wala kubughudhiwa.

Baada ya kuvamia machimbo hayo ambayo yapo kilomita 45 kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Bukombe, Ushirombo ambako kuna kituo cha polisi yakiwa yamevalia nguo nyeusi na kofia kubwa ziliyokua zimefunika nusu ya nyuso zao maarufu pama, yaliwateka wanunuzi wa dhahabu na kuwapora mamilioni ya fedha na dhahabu nyingi walizokuwa wamenunua.

Ili kuwatisha watu waliokuwa katika eneo hilo, yaliwajeruhi watu wawili kwa kuwapiga risasi mmoja mguuni na mwingine pajani pamoja na kupiga risasi nyingi hewani na wengine kadhaa yakawateka nyara.

Kwa mujibu wa watu waliokuwepo katika eneo hilo la tukio, baada ya kuwapora wanunuzi, majambazi hayo yalivamia kwenye mighahawa na mawakala wa kuuza pombe ambao pia waliporwa fedha zote za mauzo kabla ya kuhamia kwenye vibanda vya kuuza vyakula vya Mamalishe ambavyo viko mbali na machimbo ambako pia yalipora fedha.

Baada ya kumaliza uporaji huo, majambazi hayo bila ya wasiwasi yaliingia katika sehemu ya baa zilizokuwa hazina watu baada ya kukimbiwa na wafanyakazi wake kutokana na kusikia milio ya risasi na kuanza kunywa pombe.

Katika purukushani ya kuyakimbia majambazi hayo ili kusalimia maisha yao, baadhi ya wachimbaji waliumia baada ya kutumbukia kwenye mashimo ya dhahabu.

Hata hivyo, msemamo wa kiswahili usemao; 'Kufa kufaana' ulijidhirisha baada ya baadhi ya wachimbaji waliokuwa mbali kidogo eneo walilokuwa majambazi hao kuanza kuiba vitu vilivyoachwa na wenzao waliokuwa wamekimbia baada ya kusikia milio ya risasi.

Baada ya kumaliza kunywa pombe majambazi hayo yaliwachukua baadhi ya wanawake waliokuwa yamewateka na kuanza kuwabaka huku yakiwatishia kuwapiga risasi iwapo wangekataa.

Kama vile hiyo haikutosha, baada kumaliza starehe yao kwenye majira ya saa 9:00 usiku, majambazi hayo yaliwachukua baadhi ya wachimbaji waliokuwa chini ya ulinzi na kuwalazimisha kuwasadia kubeba mabegi yaliyojazwa vitu mbalimbali walivyopora zikiwamo dhahabu na fedha hadi porini yalipokuwa yameacha gari lao.

Mulongo alisema hadi kufika jana hali ilikuwa shwari katika eneo hilo na kwamba polisi walikuwa wameshafika huo kuendelea na upelelezi.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa Polisi kutoka Kituo cha Ushirombo wilayani humo walipata taarifa za enoe hilo kuvamiwa na majambazi lakini walishindwa kwenda kupambana nayo na kwamba walifika katika eneo la tukio baada ya kuondoka saa 9:00 usiku yakiwa tayari yameondoka.

Mulongo alisema serikali inaangalia utaratibu wa kuyafunga machimbo hayo kwa kuwa hali ya usalama katika eneo hilo si nzuri kwa vile machimbo ya yako katikati ya msitu na hakuna ulinzi wa kutosha haupo.

Machimbo hayo mapya ambayo yalianza Novemba mwaka huu yana watu zaidi ya 30,000 ambao wanafanya kazi mbalimbali wakiwamo wachimbaji ambao wanachimba saa 24 na wafanyabiasha mbalimbali.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Shiyanga, Ibrahim Shaibu alithibitisha kuwepo kwa tukio na kwamba tayari wameweka askari wake katika barabara kuu zote mkoani Shinyanga kuyasaka majambazi hayo.

Hivi sasa kasi ya vitendo vya ujambazi inaanza kurejea kwa kasi mpya kama zamani sehemu mbalimbali nchini na kuendesha vitendo vya uporaji na mauaji.

Juzi majambazi yaliliripotiwa kuua askari polisi mmoja pamoja na kupora Sh44 milioni jijini Dar es Salaam kutoka kwa mfanyabiashara mmoja ambaye yalimvamia dukani kwake.

Siku hiyo majambazi mamilioni ya fedha zinazosadikiwa kuwa mishahara ya watumishi wa Kiwanda cha Kutengeneza Vyandarua cha ATOZ cha mjini Arusha na mengine yaliteka gari lilokuwa na mchanga wa madini ya tanzanite huko Simajiro, mkoani Manyara.

Mkuu jeshi la polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema alipoingia madarakani alianzisha operesheni ya kusafisha jeshi hilo ikiwamo kupambana na majambazi.

Operesheni hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, lakini hata hivyo hivi sasa vitendo vya ujambazi vimeibuka upya na kutishia maisha ya raia na mali zao kila mahali nchini.
 
Mbona sioni constructive criticism hapa? labda mkuu wa kaya katoa kauli hiyo kulingana na upeo wake (pamoja na timu yake)wa kufikiri. Tumsaidieni jamani ili next time ajue nini kinapaswa kusemwa aki encounter similar situation.

Hivi unamsaidia vipi mtu aliyetumia miaka 10 kujiandaa kuchukua uongozi wa nchi,implying kwamba alishafanya maandalizi ya kutosha kabla hajakabidhiwa jukumu hilo.Au msaada gani zaidi tunaoweza kumpatia ilhali ana WASAIDIZI WENGINE 60 (ukubwa wa cabinet yake) wanaolipwa fedha za walipakodi?
 
Baada ya kusikia tafsiri mbali mbali nimekuwa na wasiwasi na JK kama kweli ameisha fanya vya kutosha ningeomba tuweze kuweka mazuri aliyoweza kufanya mpaka sasa hivi maana najua pamoja na kwamba inaonekana kulemewa na mzigo kuna ambayo kidogo amejitahidi kulingana na uwezo wake.

La kwanza kabisa ninaloliona waziwazi ni suala la majambazi wale wa sinza ambalo lilipelekea kukamatwa kwa akina afande zombwe. Hili suala alionekana kufaulu vizuri.

Suala la Pili aliloweza kufaulu ni suala la majambazi yaliyokuwa yametanda kila mahala wakati BWM akitoka madarakani. Hili suala alilishughulikia kwa makini sana na nafikiri kwa asilimia 60% aliweza kufaulu.
Suala lingine limekuwa la kuanzisha vyuo vikuu kama DODOMA university ambavyo pamoja na ukosefu mkubwa wa wafundishaji, lakini amejitahidi kuanzisha hiki chuo ambacho kitaweza kuzalisha wataalamu katika nchi hii.

Suala lingine ambalo nalo amelichukulia bango ni suala la Elimu ya Msingi ambalo pia nimeona ameweza kulifanyia kazi pamoja na kwamba pia lina matatizo makubwa sana ya ukosefu wa walimu ambalo limepelekea kuturudisha ktk kutumia walimu ambao hawakusomea fani hiyo.

Lakini pia mapungufu yanaonekana kuwa makubwa kuliko mafanikio. Masuala mengi sana inawezekana anayafahamu sana na ana ushahidi wa kutosha hila ameshindwa kufunga paka kengele. jamani mimi niliyoyajua ni kama haya ningependa pia kama kuna mazuri ambayo ameisha yafanya pamoja na kwamba kuna ambao wanasema muda bado anajifunza au anajipanga kama alivyowahi kusema waziri Mramba naomba atoe data.

Naona umejaribu kutetea lakini cha ajabu kila mafanikio ulioyataja unakuwa mwepesi kukubali kwamba lakini.... kwa kiingereza 'but's na 'if's kibao!
Suala la majambazi inabidi nikatae! Hivi unasoma magzeti kweli? Hujasoma wikiendi hii majambazi walivyokuwa na field day! And FYI masuala ya ujambazi yalikithiri JK alipoingia madarakani siyo wakati wa BWM! Hata ishu ya akina Zombe ilikuwa enzi zake, so let's put the record straight! This was a power struggle among the police, nadhani kuna wachambuzi wenye information zaidi.
Suala la elimu - university, primary na secondary - enzi za danganya toto Bongo imekwisha! Wanalazimisha wananchi wajenge mashule na wanakomba misaada alafu tunasoma kila leo pesa za MMES na MMEM zimetafunwa, alafu watoto wanaenda shule na kujikuta na mwalimu moja. Then what happens? Panic! "Basi tuchukue ma-failure wa form four waende kufundisha watoto wetu" - ludicrous! Mungwana hana strategy katika elimu! Kaikuta imebaki from BWM era anaiendeleza it is not his initiatve, hili nalijua maana nliona mpango wa kuendeleza elimu. Walianza na MMES under BWM na next stage ilikuwa ni sekondari then baadaye vyuo. Siyo mafanikio yake JK!

Lakini thread hii haiko hapa kuchambua mafanikio ya JK, bali tunachojaribu kuelewa ni kwamba ana matatizo gani rais wetu? Maana it is without doubt kwamba mambo hayaendi kabisa Bongo. Sasa tunajaribu kuchambua psyche yake.
Look sisi kama raia wa Tanzania, in fact wapiga kura, tunampa mtu kura kuwa rais ili atende vitu fulani, sasa kusema anajitahidi and that he is training on the job for 2 years is WRONG!
Inaonyesha kwamba a) he is slow to understand maana miaka 2 bado tu! b) he understands but is incapable of action

Naomba: mwaka 2010 iwe mwaka wa mabadiliko jamani we cannot take more of the same!
 
"Naomba: mwaka 2010 uwe mwaka wa mabadiliko jamani we cannot take more of the same"(Susuviri)

Your anguish, and that of many now is obvious, but alas, your wish under CCM cannot happen. And it is CCM definetely 2010.

To bad my compatriot!
 
Kalamu, mbona mimi naona kwamba there are 2 alternatives for changes:
a) CCM is not homogenous and I know that there are plentiful who also think 'we can't have more of the same' politics is very unpredictable, so change can happen within the party (possibility: 30%, max 40%)
b) 2010 is not set in stone for CCM. I feel that if no significant changes will be made (and no sign of it so far) then JK will be a 1 term president. (possibility 50% max 60%)

That is my amateurish take of things. I am ready for a discussion on this in a separate thread.
 
Mama Salma awe nazo ngapi? Hujui ukiachilia Ujenzi wa South Africa humu nchini nani katumalizia cement? Na Je wajua anafanya nini? Mkubwa Ikulu ya Danganyika hata kama hujui Biashara Utafundishwa.
 
Mama Salma awe nazo ngapi? Hujui ukiachilia Ujenzi wa South Africa humu nchini nani katumalizia cement? Na Je wajua anafanya nini? Mkubwa Ikulu ya Danganyika hata kama hujui Biashara Utafundishwa.

Sorry, sikuelewi, :confused: unaweza kutufafanulia labda wengine nani katumalizia cement? Asante
 
Ntereyehirungu

Kwahiyo mama Salma anajenga South Africa?Hii kitu nimesikia sehemusehemu kwamba huyo mama ameanza bishara chafu Ikulu.Hebu tupe kidogo
 
Huu ni utani sasa, akishatutajia so what, nilitegemea sisi ndo tumtajie a take actions, huu ni usanii sasa.
 
Huu ni utani sasa, akishatutajia so what, nilitegemea sisi ndo tumtajie a take actions, huu ni usanii sasa.

Si tumeomba ufafanuzi? Mbona unakuwa kama unatetea mtu au ishu? Hapa JF tunaomba mtu alete data na ikiwezekana ushahidi tuifanyie kazi. Kama ni uzushi tutajua maana atakaa kimya! Sasa tatizo liko wapi? Hakuna usanii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom