Huyu JK vipi???

Moja kati ya udhaifu mkubwa sana kwa kiongozi ni kutotekeleza anayoyasema, hii inaonyesha dharau kwa wale anaowaeleza maneno hayo.

Mbaya zaidi yeye mwenyewe anafahamu kuwa amesema mambo mengi na kuwaahidi watanzania lakini hakuna chochote anachofanya,
Dawa yake ni ndogo sana, 2010, pale tutakapo mwuliza maswali, yeye na wenzake wagombea ubunge 'mbona maneno yenu mengi mliyosema yamebaki kuwa hadidhi' hapo ndipo tutasikia kigugumizi na kazi ni moja tu piga wote Chini akina sisiemu.
 
Mi naona bora hata mzee wa ruksa kuliko huyu "HANDSOME BOY" Sijui hata anatupeleka wapi? Kesi ya mpambe wake ndo ilisaisha hivyo, uliona wapi muuaji tena kwa makusudi yuko nje kwa dhamana tena anapeta tu Dar-Tabora, anasafirisha zake asali bila hata wasiwasi.

Ila mi bado nayasubiri hayo maisha bora kwa kila Mtanzania, maybe 2009,manake kampeni zitakuwa zimekaribia.
 
Mimi sijasikia wala kuona mazuri yoyote. Shule za msingi nyingi bado zina majengo ambayo hayastahili kuitwa shule, wanafunzi hawana viti na madawati, hakuna vyoo na wana walimu wachache au hawana walimu kabisa, haya kwangu si mafanikio. The jury is still out when it comes to criminals.

*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Posted Date::12/3/2007
Majambazi yamtumia salamu mpya Mwema

*Yateka, yapora mamilioni mgodini

*Yalewa, yabaka na kuondoka bila hofu

* Baadhi wachimbaji wajinufaisha

*DC Bukombe aamuru mgodi ufungwe


Shija Felician na Suzy Butondo,Bukombe
Mwananchi


Asante mzee mimi nilikuwa nimempa credit JK kwa kumaliza majambazi. Kumbe nayeye sasa anaanza kuzalisha majambazi. basi hana cha kujivunia.
 
Naona umejaribu kutetea lakini cha ajabu kila mafanikio ulioyataja unakuwa mwepesi kukubali kwamba lakini.... kwa kiingereza 'but's na 'if's kibao!
Suala la majambazi inabidi nikatae! Hivi unasoma magzeti kweli? Hujasoma wikiendi hii majambazi walivyokuwa na field day! And FYI masuala ya ujambazi yalikithiri JK alipoingia madarakani siyo wakati wa BWM! Hata ishu ya akina Zombe ilikuwa enzi zake, so let's put the record straight! This was a power struggle among the police, nadhani kuna wachambuzi wenye information zaidi.
Suala la elimu - university, primary na secondary - enzi za danganya toto Bongo imekwisha! Wanalazimisha wananchi wajenge mashule na wanakomba misaada alafu tunasoma kila leo pesa za MMES na MMEM zimetafunwa, alafu watoto wanaenda shule na kujikuta na mwalimu moja. Then what happens? Panic! "Basi tuchukue ma-failure wa form four waende kufundisha watoto wetu" - ludicrous! Mungwana hana strategy katika elimu! Kaikuta imebaki from BWM era anaiendeleza it is not his initiatve, hili nalijua maana nliona mpango wa kuendeleza elimu. Walianza na MMES under BWM na next stage ilikuwa ni sekondari then baadaye vyuo. Siyo mafanikio yake JK!

Lakini thread hii haiko hapa kuchambua mafanikio ya JK, bali tunachojaribu kuelewa ni kwamba ana matatizo gani rais wetu? Maana it is without doubt kwamba mambo hayaendi kabisa Bongo. Sasa tunajaribu kuchambua psyche yake.
Look sisi kama raia wa Tanzania, in fact wapiga kura, tunampa mtu kura kuwa rais ili atende vitu fulani, sasa kusema anajitahidi and that he is training on the job for 2 years is WRONG!
Inaonyesha kwamba a) he is slow to understand maana miaka 2 bado tu! b) he understands but is incapable of action

Naomba: mwaka 2010 iwe mwaka wa mabadiliko jamani we cannot take more of the same!

Mzee nashukuru kwa updates. Basi nafikiri kuna haja za makusudi za kupiga kampeni za waziwazi kuhakikisha MR. JK anashindwa kwa kishindo kama alivyoshinda kwa kishindo.

Ikidhihirika kuwa hakufanya kitu na kuendelea kujichanganya kwa kutojua wananchi walikuwa wanategemea nini kwake, nafikiri itabidi tupige ndogondogo hata ndani ya CCM asipite katika mchujo wa kutafuta mgombea.

Lakini pia nafikiri kuna haja ya kuainisha failure zake balabala hili ziweze kutumika wakati wa uchaguzi mwaka 2010, hili hata yeye asije akalalamika pale misaafu itakapochomolewa.

Hizi kauli zake ikiwapo pia ya nguvu mpya kasi mpya itunzwe vizuri hili tuweze kupima kama kweli ameweza kufanikisha objective yake.
 
"Naomba: mwaka 2010 uwe mwaka wa mabadiliko jamani we cannot take more of the same"(Susuviri)

Your anguish, and that of many now is obvious, but alas, your wish under CCM cannot happen. And it is CCM definetely 2010.QUOTE]

Susuviri umeeleza vizuri sana una napenda watu wenye courage kama yako.Tatizo tuko wachache.Siwapendi watu wenye mitazamo ya Kalamu ya kukata tamaa.Haiwezekani maanake nini.Kufufua wafu tu ndo kitu ambacho hakiwezekani.What is CCM anyway??They are not ALFA and OMEGA.They not gods. They are just a bunch of Greedy,Selfish and Corrupt people who don't have any moral conscious.Their main objective is just to gain power and then use it rob Tanzanians.
Kwa nini watushinde kuwaondoa madarakani kama kweli tutakuwa tumeamua.Lakini kama tuna mawazo kama ya Kalamu ya kukata tamaa kabla ya kutenda ni kuwa tunawapa ushindi kabla hata ya kupiga kura na wakati kura tunachofanya ni kuwahalarishia.Kwa kuwa hatufikiri na kuchanganua kipindi cha uchaguzi that is why to end up na wat kama JK.
Watanzania tuamke,hakuna ambacho hakiwezekani zaidi ya kurudisha uhai
 
huyu shetani anaitwa nyani siku yake ikifika ya kutereza kila mti ni TAWI sasa ngojeni tu huyu JK havuki 2010 nakuapieni tusijekupata sifa bure ya kuwa watabiri hata kwa vitu wazi namna hii!!!!

wewe jiulize ni amri ngapi ametoa na zikawa amri? huyu alizoea kuruka na mademu sasa anafikiria tuko huko huko kwenye field hiyo mpuuzi mkubwa?

Ebana vipi mbona umenijia juu hivyo? Unataka kuanzisha shari na mimi au nimekuelewa vibaya? Hebu fafanua zaidi....
 
Kinyau, ongezea na hizi!

5. "Tanzania tunasaini mikataba mibovu kwa sababu hatuna wataalamu wabobevu wa sekta ya madini". (Swali kwa Rais: Nyerere na STAMICO yake waliwatoa wapi wataalamu?)
6. "Sijui umasikini wa Watanzania unatokana na nini" (Swali kwa Raisi: Uliomba uraisi ili ufanye nini? Sasa uko madarakani kufanya nini? Biashara? Utalii?

i wish huyu mkuu wetu wa idara ya utalii na bnez kwa mabiashara Tz angekua member wa JF naye ajadili nasi ili tujue hasa yuko pale kwenye jumba jeupe kwa minajili gan?as waTz hatuelewi
 
Mmh! yaani Chadema kina Dr. Slaa & Co. ni wakali na trend setters, yaani mpaka Raisi wa jamuhuri anawaiga staili yao ya kuwashitaki wabadhirifu kwa wananchi?
 
Rais Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kutambua kuwa njia pekee itakayowakwamua kiuchumi na kuwaletea maisha bora ni kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo na si kukaa tu vijiweni na kulalamika.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akijibu malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Nyumba ya Mungu, kilichopo katika kata ya Lang`ata, tarafa Msitu wa Tembo, wilayani Simanjiro, ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Manyara.
 
Mkuu nimekuelwa vizuri ila wewe kufikia uamuzi kwamba ni JF hapo you went out of line!Ina maana you mean JF ni Kijiwe?Hapa hatulalamiki kama JK anavyodai but we are providing solutions to some of the most pressing issues in our country ambazo zinahitaji solutions and pointing out the weaknesses of the govt and other people as well as how to bring them back on track!
 
Umejuaje amekusudia Jamii Forums ?

Sasa mwenye macho haambiwi tazama ,si unajua JF tupo mstari wa mbele kuzidumba kauli za Muungwana na maisha bora kwa kila Mtanzania ,hivi nani aliahidi kuwa atahakikisha kila Mtz anapata na kuishi katika maisha ya wastani.

Sasa kama yeye aliahidi inakuwaje leo arudi atuambie tusikae na kulalamikia ahadi zake ambazo hajazitekeleza,hivi ni nani aliahidi kupambana na rushwa,ni nani aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania ,ni nani aliahidi kutengeneza ajira au nafasi za kazi kwa mamilioni ,hivi huelewi kama Mheshimiwa anakengeuka ahadi zake ?

Hivi Muungwana hajui kama waTz wanasubiri hizo ajira ili waanze kuchapa kazi ? Sasa kusema tusikae vijiweni kupiga makelele kudai ziko wapi sera zake za kuwania Uchaguzi ndio imekuwa nongwa ?
JF ni kijiwe ambacho waTz wenye maoni mbali mbali hukutana na kupeana uwono kwa kina ,sasa ukisikia kijiwe sijui kwa akili yako inakufananishia na nini ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom