nsimba
JF-Expert Member
- Oct 7, 2010
- 782
- 55
"...Ni hatua inayoibua maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano, kwa nini Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda waliona vyema kumkaripia Waziri Magufuli hadharani, tena kwa kauli za kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi na wapigakura wake ili aonekane kama mtu katili asiye na utu wala ubinadamu? Kwa nini hoja na kauli zao hazikupelekwa kwanza katika Baraza la Mawaziri kama kweli walikuwa na nia ya kufanya hivyo? Na kama wanaona kuwa sheria inayosimamia hifadhi za barabara haifai kwa nini wasizungumzie haja ya kupeleka muswada bungeni ili sheria hiyo iwekewe utu na ubinadamu badala ya kumsingizia waziri huyo kwamba anatumia ubabe?
Tunadhani kwamba tatizo sio Waziri Magufuli bali kuna ajenda zilizojificha hapa. Badala ya kumlaumu na kumdhalilisha waziri huyo tunapaswa kumpongeza, na Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda ndio wangekuwa wa kwanza kufanya hivyo, kwa maana kwamba ni mmoja wa mawaziri wachache sana katika historia ya Baraza la mawaziri ambao wameiletea Serikali heshima kubwa na kuijengea imani kwa wananchi kutokana na kuchapa kazi na kusimamia sheria na Katiba ya nchi yetu.
Wananchi wanajiuliza kwamba hatua ya kumpiga stop Waziri Magufuli ni kwa faida ya nani? Hakuna anayeweza kujidanganya kuwa ni kwa faida ya wananchi maskini kama watawala wanavyotaka tuamini. Hatua hiyo ni ya kuwanusuru vigogo na matajiri walioweka mabango ya matangazo na waliojenga vituo vya mafuta na majengo mengine ndani ya hifadhi ya barabara. Wananchi wanasema kuwa kamwe hawadanganyiki..." (mwananchi, machi 23, 2011).
nionanvyo mimi, Kumzuia waziri mwenye dhamana husika kutotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na katika ya nchi ni "ukiukwaji wa sheria na kaTiba ya nchi" uliofanywa na PM na Rais jk katika kuzuia utawala wa kisheria. Naamini jambo hili limefanywa kutufanya tuamini kuwa serikali ina huruma kwa wananchi wake; jambo ambalo naamini si kweli; bali ni kwa masilahi ya (1) matajiri/mafisadi wenye sheli za mafuta/miradi anuwai na mabango kando ya barabara (2) kisiasa kumdhalilisha magufuli ambaye tangu zamani ameshaonesha uhodari wake kwa watanzania wa kushughulikia mambo ya watu kwa mujibu wa katiba pasipo kuogopa yeyote. Kiongozi ambaye anaonekana pia kuwa miongoni mwa wang'aao machoni mwa watanzania kwenye mbio za 2015. Kisiasa, naamini anafanyiwa "siasa ya maji taka".