Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,178
- 876
Habari zaidi endelea hapaJK awaonya viongozi walafi
03 Dec 2007
By Maura Mwingira, Kibaha
Rais Jakaya Kikwete, amewatahadharisha viongozi wanaojigawia miradi ya wananchi maskini kuwa wasipoacha tabia hiyo atawataja hadharani.
``Naomba tuelewane kabisa Mkigawana miradi ya maendeleo ambayo imelengwa kuinua maisha ya wananchi maskini na kuwapatia kipato, mtakiona cha mtemakuni nitawasema hadharani mbele ya wananchi,`` alisisitiza.
Alitoa tahadhari hiyo jana baada ya kuelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Christine Ishengoma kuhusu mradi wa ugawaji wa miche ya miembe inayozaa kwa muda mfupi kwa wakulima maskini katika wilaya za mkoa humo.
"Vitisho vya kitoto" vya aina hii ungeweza kuvitarajia kutoka kwa kiranja wa darasa kule shule ya msingi,kwamba "atakayeendelea kupiga kelele nitamwandika,au kumtaja kwa mwalimu..." lakini sio kwa kiongozi wa nchi tuliyempa wadhifa wa urais.Kwahiyo akishatutajia hadharani kifuatie nini?Tuawazomee?Tuwapige mawe?Au TAKUKURU ndio waamke usingizini kuwachunguza?Hivi huyu mtu hana mtu anayemsaidia kuandaa hotuba zake?Anyway,pengine atakapoamua kutaja hao wanaogawana miradi atatutajia pia na wala rushwa alodai anawafahamu lakini anawapa muda wa kujirekebisha.Kaaazi kwelikweli