May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Siku za hivi karibuni kumezuka Wanasiasa na Wanaharakati wanaohanikiza kupatikana kwa katiba mpya, huku wakijaribu kuiaminisha jamii ya Watanzania kwamba kupatikana kwake ndio itakuwa mwisho wa Matatizo ya nchi hii.
Kwa muda wote ninajaribu kuwasikiliza mmoja baada ya Mwingine na bado sioni ni kiasi gani nashawishika kuona kwamba kuna ukweli unaojitosheleza, ningetamani kusikia hoja nzito zinazonithibitishia kuwa kama Nchi basi tumekuwa tunakwamishwa na mambo haya au yale, na kwamba tukipata katiba mpya basi kila kitu kitakuwa sawa. Zaidi naona kama mengi wanayojaribu kuyapigania ni ya kisiasa na madaraka zaidi kuliko matatizo halisi ya kila siku ya Wananchi.
Nijuacho mimi ni kuwa Mwanasiasa anaishi kwa siasa, hivyo kuanzisha jambo la kuwafanya waonekane wapo kazini kwao ni namna nzuri ya kuweka tiki kwenye kalenda zao kwamba tar hii walikuwa Makambako, tarehe ile Kahama, iliyofuata Namtumbo n.k na hivyo kujiongezea CV, na hata kipato maana tayari watakuwa na namna ya kuwaonesha Wahisani/Wafadhili kuwa wapo busy.
Watajitahidi kuwashawishi Wananchi ili wawaunge mkono bila kujali ya kuwa tofauti na wao Wananchi hawana wa kuwafidia muda wao maana wao kwa wakati huo wapo kazini ili hali Wananchi wataacha shughuli zao za siku kuhudhuria mikutano hiyo, yaani kama ni Muuza chipsi, Kinyozi, Fundi wa kuchomelea, Mama Lishe n.k watatakiwa kufunga ofisi zao wakawasikilize Watu ambao wao wapo kazini.
Natamani nimsikie aliyekuwa Mbunge kwenye jimbo ninakoishi la Arusha Mjini, kwa muda wote aliokuwa kiongozi wa Jimbo aseme ni nini kilimkwamisha kutekeleza aliyokuwa anaahidi kwa kukwazwa na katiba iliyopo.
Mbunge huyu ni juzi tu ametoka kupokea mamilioni ya pesa kama mafao, hivi ni kiasi gani ametenga kwa waliokuwa wapiga kura wake kwa vipindi vyote hapa jimboni kuwasadia hili na lile kwenye shughuli zao?, au pia amekwamishwa na katiba iliyopo?. kumuona tena ni mpaka 2025 aje kupambana kutafuta fursa nyingine ya kurudi Bungeni.
Hivi ni Vijana/kina Mama wangapi wamewahi kupata msaada 'support' wa kiujuzi au mtaji ili waanzishe Viwanda vyao Vidogo Vidogo?, walipieni Vijana mafunzo ya Sido pale Ungalimitedi? natamani nioneshwe Wapiga Kura walionufaika kupitia Kiongozi wao na kama hakuna naomba Kiongozi aniambie ni kwa namna gani katiba iliyopo imemkwamisha.
Hivi isingekuwa zaidi Kwa Kiongozi anayejinadi kuwatetea na kuwajali sana Wananchi wake kuja na madai yawayo yote yale huku tayari akiwa na mamia ya Watu nyuma yake wanaomiliki viwanda/miradi/mashamba kwa muongozo/usimamizi/ushauri wake? au hata hilo wanakwamishwa na katiba iliyopo?.
Ninachojua mimi ni kuwa Mbunge wetu alikuwa anajiangalia yeye na familia yake kwanza na sio Wapiga kura/Wananchi.... Sasa leo wakitaka kutuambia kuwa inatakiwa katiba mpya ndio ibadili roho za Wanasiasa ni usanii wa kisiasa tu.
Na hebu hata Wananchi wa maeneo mengine nao wafanye tathmini ya mabadiliko waliyoyapata tangu wawashawishike kuwachagua Wabunge wao...Walinganishe hali ya Mbunge kabla ya kupata Ubunge na baada ya kupata Ubunge, ni nani amenufaika...ni yeye ay wao?....aulizwe Msigwa, aulizwe Sugu, aulizwe Mnyika, aulizwe Bulaya n.k.
Huenda ni kweli kuna umuhimu wa katiba mpya lakini si kweli kwamba wanasaiasa wanafanya hivyo kwa manufaa ya Wananchi bali ni kwa faida yao kwanza.
Na kama inabidi kufanya hizo harakati zao basi zifanyike bila kuathiri muda wa Wananchi?. Yaani Wananchi waachwe wajitafutie riziki zao za siku hadi siku huku na Wanasiasa wakipambania hilo wanalofikiri lina manufaa kwa nchi?.
Mimi kama Mwananchi kama kipo ninachotamani kukiona basi ni namna ya kuwawajibisha Wabunge/Wawakilishi wetu, walau kila Mwaka tuwe na mkutano tuwahoji ni mangapi ametimiza kati ya aliyoayaahidi...na maksi zikiwa chache basi apoteze sifa ya kuendelea kuwa Mbunge....hivi jambo kama hili halitekelezeki kwa kurekebisha tu kifungu bila kuhitaji mchakato mreeefu wa katiba mpya?.