huu ni ugojwa au kunamkono wa mtu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huu ni ugojwa au kunamkono wa mtu?

Discussion in 'JF Doctor' started by ummu kulthum, Aug 11, 2012.

 1. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu anamatatizo ya kuanguka/kuzimia pale tu anapoona maiti na akilia kwa sauti ghafla anajikuta analegea na kuanguka, kwa madai yake anasema wakati anaanguka huwa anajijua lakin anashidwa kujizuia na wanaompa huduma ya kwanza huwa anawasikia kwa mbali sana lakin kujibu anashidwa na nguvu hana kabisa!!.

  chanzo cha tatizo;

  ilikuwa ni usiku wa manane akaota mama yake alikuwa mgojwa amefariki na siku 3 kabda ya kuota mkono wa kulia ulikuwa unamuuma sana bila sababu yeyote na ukawa haunyooki kabisa.katika ndoto hizo akaota amefariki na analia sana mpaka anazimia na kubebwa na watu na ni kweli baada ya siku tatu ndicho kilichotokea.
  mama yake akawa amefariki R.l.P.
  sasa hicho kitu huwa kinajirudia akiwa ameenda msibani akiona tu maiti lazima azimie je hii kitu inasababishwa na nini?
  wadau kama mtu anajua tiba atujuze kwani hali ni mbaya af huwa anashtuka shtuka kwa mfano akiwa chumbani ukifungua mlango kwa haraka anashtuka sana hadi unamuonea huruma.
   
 2. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,697
  Likes Received: 8,232
  Trophy Points: 280
  Psychological problem inaonyesha....sijui matibabu ila mtaalamu wa masuala hayo atasaidia zaidi.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mpe Pole sana bibie ndugu yako ningelikuweko huko Singida ningelimuombea Dua. ninakushauri hivi mpelekee kwa Sheikh wa mkowa akamsomee Dua kisomo cha RuQya amepatwa na pepo mbaya Sheytani mbaya ndie anaye muangusha angusha haswa anapoona Maiti na anapokuwa hapo kwenye mazishi ya mtu yoyote yule akisomea na kupewa Dawa ya kunywa basi inshallah Matatizo yatamuondokea. Kama Ndugu yako ni Mkristo mwambie aende kuombewa kwa Mchungaji matatizo yake yatamuondokea inshallah.
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mashehe watamuongezea matatizo. Hao pamoja na wachungaji wengi wao ni wachafu kuliko hata hao nguruwe. Ningeshauri aende kwa wataalam wa afya hasa wana saikolojia na watabibu wa akili. Mambo ya kuombewa dua au kutolewa mapepo ni utapeli wa kawaida na yamepitwa na wakati. Sayansi imekuwa kiasi cha kuondoa hisia za namna hii.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  ummu kulthum Msome Sigmund Freud anaielezea kwa undani hiyo hali.

  Kwa kifupi binaadam tuna khulka ya kukataa tusiyoyataka "subconsciously" na hicho ndicho kinamtokea nduguyo. Kila anapoona maiti ile hali ya kuondokewa na mama'ke huwa inajirudia na anaikataa (avoidance) (subconsciously) na hupelekea kuizima (kuzimia) hali yake ya kuwa "conscious" na ndio mwili hujipeleka kwenye kitu kinachoitwa "avoidance" ya hiyo hali.

  Hiyo ni kawaida kwa binaadam wote lakini kila mmoja ana namna yake ya kuionesha. Wengine huingia kwenye "avoidance" kwa kuzimia, wengine huingia kwenye "avoidance" kwa kusahau, wengine hungia kwenye "avoidance" kwa kupatwa na usingizi mzito, wengine huingia kwenye "avoidance" kwa kujisahaulisha kwa kutumia njia ya uraibu kama pombe, bangi na dawa za kulevya, wengine huingia kwenye "avoidance" kwa kufunga na kuwa wacha mungu, na hawa ndio bora kati ya wote

  Nduguyo asome sana Ayatul Kursii na kuielewa maana yake. Itamuondoka hali hiyo akiizingatia.

  Na pia psychological consultations kwa anefahamu hiyo hali zitamsaidia sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kufika huko kote nadhani wangeangalia kwanza hysteria.
  huyo ndugu yako ni msichana? ana miaka kati ya 15-30? ni single?
  Ana pata attention ya kutosha kutoka kwa nduguze na marfiki?
  Kuna social study nilisoma ikisema kua more tha 80% ya wasichana
  wanao dai kukumbwa na "mapepo" simply wanasumbuliwa na hysteria
  (if this is the case, a little mental therapy and a support group would help
  nikikumbuka nilikosoma hii study nitaleta link. Nilisikitika sana niliposoma.
  But she could also be among the 20% who suffer from other conditions
  msifikirii kabisa mambo ya majini au mikono ya binadam hapo. mental health!
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii tunaita post traumatic stress disorder (PTSD) aende pale Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili amwone Dr Hogan au Dr frank atamsaidia tu na hii hali itapungua with training. All the best.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mimi huwa ninaposema kitu huwa ninakuwa na Ushahidi wangu matatizo hayo pia yaliwahi kumkuta Marehemu Mama yangu Mzazi Mwaka 1991 nilipofiwa mimi na twins Pacha wangu wa kike alikuwa mama yangu ni mtu mwenye kuanguka na

  Pressure kuwa juu kila anapomfikiria mwenzangu aliyoondoka duniani nikamfanyia Dua ya maombi kwa Mwenyeezi Mungu akamsahau Pacha mwenzangu na Matatizo yakamuondokea aliwahi kwenda Hospitali na kumpa Dawa hazikumsaidia kitu

  mpaka nilipoamuwa mimi Mwenyewe nifanye Maombi Kwa Mwenyeezi Mungu na matatizo yakaondoka kabisa sasa wewe unasema Mashehe watamzidishia matatizo labda Mashehe wako wewe mkuu Father of All
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Najua wewe ni mtu wa kutafiti na kutoa changamoto zenye kila faida. Kwa hili sikubaliani nawe kwa vile ulitumia maombi kwenye kisa kimoja au tuseme case study. Pia matatizo ya mama yako hayawezi kuwa sawa na huyu vinginevyo kungekuwa na ushahidi wa kisayansi. Maana nijuavyo huyu jamaa hamjaonana wala hujamuona huyo mganga. Kwa ufupi, kisayansi, huwezi kugundua dawa ukamfanyia panya au mtu mmoja majaribio na ukasema matokeo yake yanafaa kuthibitisha uvumbuzi wako.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kila kitu ni kujaribu na kuomba Mungu Kwa Mungu kila kitu kinawezekana Asifiwae ni Mmoja Bwana Mungu Muumba wa vitu vyote kila kitu Muombe yeye Bwana Muumba atakupa na Kukusaidia tu. mkuu Father of All
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa hilo nakubaliana nawe. Maana mafanikio na maisha yetu siyo matokea ya juhudi au ujanja wetu bali majaliwa yake Maulana. Mkuu MziziMkavu respect.
   
 12. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,681
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Mwoga na anaamini kalogwa, atateseka sana mpaka hapo atakapojua kuna nguvu ya Yesu Ambayo Ni zaidi ya shetani.


   
 13. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  naunga mkono hoja,waende kanisani wakaombewe mkuu,hiyo ndo kila kitu...
   
 14. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Polen,em Mtafute Mwakasege,hata kwa simu,au email..na uwe na imani atapona.
   
 15. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ana miaka 25 hajaolewa na alikuwa mtoto wa kwanza na wadogo zake wawili kumbuka hiyo mkuu
   
 16. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asante na ninashukuru kwa mawazo yako
   
 17. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asanteni kwa mchango wenu wa mawazo sina cha kuwalipa isipokuwa SHUKURANI.
   
 18. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nashkuru, ye ni muislam na kila mara anavyoanguka huwa wanamsomea dua na anazinduka wakati mwingine huzinduka mwenyewe hata hajasomewa na kumwagiwa maji,kubwa ni pale hata akikuta watu wameenda mazishini na maiti hakuiona, akilia sana anazimia.anatatizo gani huyu na dawa za kizugu ashatumia sana?
   
 19. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Basi anafit sana katika hiyo category ya wanawake
  ambao wengi wao wanapo patikana na tatizo hili
  inakua ni Hysteria tu (in fact 80% as I mentioned)
  Mpelekeni kwa daktari wa matatizo ya akili tu.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kawaida sana, aonane na psychologist wala sio kitu cha kuumiza kichwa. Kama tatizo kumpata phsychologist hapo Singida, basi aonane na pshychiatrist wa hapo hospital ya Singida.
   
Loading...