Ni kweli huu ni mwaka wa kudai demokrasia au mwaka wa kufa vyama visivyo na demokrasia?

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Mwishoni mwa 2018 baadhi ya vyama vinavyofanya vya upinzani vilikutana Zanzibar na kutoa tamko walilolibatiza kuwa TAMKO LA ZANZIBAR. Walidai katika tamko hilo kuwa imetosha. Sijui iliwatosha nini. Ila walitamka kuwa mwaka 2019 utakuwa mwaka wa nabadili. Mwaka wa kudai DEMOKRASIA.

Wakati wakidai demokrasia karibu viongozi woote waliokuwepo ni viongozi wa kudumu au tuseme maisha kwenye vyama vyao.

Alikuwepo Maalimu Seif ambaye licha ya ukweli kuwa uongozi WA CUF hauko tena mikononi mwake bado anaamini ni kiongozi! Hii nayo ni demokrasia sampuli mpyaaa! Kiongozi asiyetambua keshapokonywa uongozi ni mdemokrasia wa aina gani? Hata bado angekuwa kiongozi je ni demokrasia sampuli gani ya kuwa kiongozi wa chama zaidi ya miaka 25 ? Tena basi Chama kuanguka kila chaguzi na kiongozi ni huyohuyu! Hata akidai huwa anashinda ila anadhulumiwa kwenye demokrasia ya kweli ingetosha kiongozi kupisha wengine.

Alikuwepo Freeman (not free now) Aikaeli Mbowe. Huyu na katiba kabadili kufuta ukomo wa kiti chake. Naye anadai demokrasia mwaka 2019! Hajui demokrasia ni pamoja na kuheshimu utawala wa sheria. Kaitwa mahakamani yee kafunga safari ya bulicheka kwenda Marekani. Kwake demokrasia ni pamoja na kuidanganya mahakama.

Alikuwepo Zitto Kabwe. Yeye hata alivyopata uongozi wa Chama cha ACT utata mtupu. Hakuna mkutano wala nini. Kafika katwaa cheo kinaitwa KIONGOZI WA KITAIFA! Ndani ya Chama Yuko MKITI TAIFA ila hafui dafu Kwa KIONGOZI WA KITAIFA. Utadhani wanatoka mataifa mawili tofauti.

Naye hamna cha vikao. Anapeleka chama atakavyo. Yeye ndio ACT na ACT ndio yeye. Wengine waganga njaa. Watu makini walipoona ujinga huu wakaondoka ikiwa pamoja na Mkiti Taifa. Ana jina kuubwa lakini juu yake yuko mtu ndio kiongozi!

Walikuwepo pia kina Rungwe wa CHAUMA na wenzao DOVUTA. Hawa hata neno demokrasia hawajui lipo. Husikii vikao vya Chama wala chaguzi za Chama. Wapo tu kundini kama kupe kwenye nundu ya nyumbu! Nao walikuwepo kudai mwaka 2019 ni demokrasia tu!

Sasa tuko February. Lakini toka mwaka uanze tunachoshuhudia kutoka Kwa hawa ni vituko badala ya demokrasia! Ni kama vile wameamua demokrasia ni kufungua kesi mahakamani. Kesi zenyewe za hovyo hovyo wala hazisaidii kuboresha demokrasia nchini. Wengi tulidhani hawa watajirudi na kuomba serikali wakae pamoja kujadili masuala yanayowakwaza.

Lakini ndio kwanzaaa wanaongeza ufundi wa kuitukana serikali na mkuu wa nchi! Wameshindwa hata na makundi kama ya viongozi wa dini, wadau wa madini, wafanyakazi, wafanyabiashara, n.k.

Ni serikali au kiongozi wa nchi gani duniani anaweza kukaa meza moja na wajinga wa kiwango hiki? Akae nao ili wamtukane?
Hapo hapo wanadai KESHO NI NZURI KULIKO JANA! Hakika KESHO YAO NI CHUNGU KULIKO JUZI!

NDUGU zangu hebu badilikeni kutoka CONFRONTATIONAL POLITICS to CONSULTATIONS L POLITICS. Upinzani si ubabe! Hakuna mbabe kuliko serikali popote duniani.

Mngekuwa mna hulka ya majadiliano hata huu mswada wa vyama usingewapa taabu. Kwa wananchi walio wengi huu mswada unasaidia kukuza demokrasia kama mlivyojiapiza Zanzibar. Nani hajui kuwa ruzuku inatafunwa?

Nani hajui hamna utaratibu mzuri wa chaguzi za viongozi? Nani asiyeoona hatari ya nyie kutumiwa kuingiza itikadi za kigeni nchini? Si kiongozi wenu huko nje katetea ushoga? Muachwe mfundishwe au mfundishane ushoga?

Lazima elimu ya itikadi idhibitiwe.. Sheria hii mpya itafanyaje KESHO YETU WOTE IWE BORA KULIKO JANA.

Tafuteni njia ya kurudi kwenye mazungumzo kuliko kushinda mahakamani na BBC. Kwa sheria mpya mtapata tabu sana!

TAFAKARINI
 
Back
Top Bottom