Huu ni ugonjwa gani? msaada tafadhali

Wgr30

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
1,770
2,375
Amani iwe nanyi!

Niende moja kwa moja kuelezea ugonjwa wenyewe,

Wandugu kuna rafiki yangu wa kike ni rafiki yangu wa mda mrefu, mwaka 2007 akiwa shule kidato cha pili alipatwa na ugojwa ambao mpaka leo unamsumbua na hana raha ya kuishi hapa duniani,

Huyu dada kuna hali fulani huwa inamtokea mara kwa mara anaanguka sana na kila akianguka mwili wake unakuwa wa baridi sana, yaana kama wewe ni mgeni wa hali yake unaweza ukahisi amefariki, akianguka anachukua masaa 5-8 ndo hali yake inarejea kuwa ya kawaida,

Huwa anasikia mambo yote yanayotendeka wakati akiwa katika hali ile cha kushangaza hawezi kuongea, kufungua macho wala kunyeyua mguu.

Ni mda mrefu sasa akiwa na hali hiyo nakumbuka siku aliyo wahi kizima kwa mda mrefu alichukua masaa 11, tulisha mtibisha hospitali mbali mbali bila mafanikio na kadiri mda unavyoenda hali inakuwa mbaya zaidi hukuzaliwa hivyo ila ilitokea akiwa kidacho cha pili.

Msaada/ushauri wenu wakuu, kama kuna mmoja wetu aliwahi kuugua/kushuhudia na akapona alifanya ni nini mpaka akapona, tumsaidie huyu dada!!

Asante.
 
Maombi tushafanya kila aina ya lakini hakuna mabadiliko yoyote,

Kwa sasa yeye yuko Tabora mkuu mimi niko Mwanza.
Mm nina hakika na nnacho kisema maana nimewaona ambao walilala zaidi ya miezi mitatu kitandani wanageuzwa tu kila kitu wanafanya hapo hapo, ila walisimama haya nnayo sema sio nayatunga nimeshuhudia kwasababu nipo chini ya huduma hiyo ,kama hutojali ni Dmn
 
Daktari aliwaambia ni tatizo gani linamsumbua?
kuna siku alizima masaa zaidi ya 8 tukamkimbiza hospital ya mkoa tukaambiwa tumpeleka Mhimbili tukaenda wakamuwekea maji yale maji hayakufanya kitu chochote kwa sababu yalikuwa haendi bali yanarudi tena na damu mpaka wakamfanyia vipimo majibu ni hamna ugonjwa mkuu!
 
Hyjawahi kuskiaa kwambaa watu huwa wanatumikishwa kuzimu? Akiamkaa anakuwa kachokaa na hajuii alikuwa wap mambo yakuchotwa ufahamu hayoo. Afanyiwe maombi ya nguvu MUNGU wetuu huwa hashindwi kitu nimkubwaa kuliko vikubwa choirs huvijuavyo
 
Anapokuwa anajitambua aombe sana kutafuta mahusiano mema binafsi na Mungu atubu na kuacha aina zote za dhambi na Yesu atampatia uponyaji kusoma biblia na kufunga iwe tabia yake Mungu
 
Back
Top Bottom