Tatizo lenu Watu wa CHADEMA, Wanaharakati na wale mnaomchukia Rais Dkt. JPM na hata wana CCM mnadhani kwamba GENTAMYCINE nikiwa humu nitakuwa upande Wenu ili niwaridhisheni na mfurahi. Sasa leo hii kupitia Kwako natamka wazi kwamba Mimi ni Mtanzania huru ambaye nawapenda Watu wote bila kujali tofauti zao zozote zile.
Rais JPM akipatia nitamsifia na akikengeuka nitamkosoa haraka sana vile vile Wapinzania nao hasa wana CHADEMA na ACT nao pia wakipatia watakoga Kongole zangu ila wakikosea sitowabakisha na nitawasema hapo hapo. Mimi siyo Mwanachama hai na halali wa CCM ila ni Shabiki wa kweli na mtiifa wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) na nitaacha Kukishabikia pale tu Jeneza langu likiwa linashushwa Kaburini.
Hata hivyo Mimi kuwepo Kwangu na ' mahaba niue ' kwa CCM haimaanishi kuwa eti wakikosea basi nitawabeba au kuwapamba na nashukuru Mungu kuwa hata wana CCM waliopo hapa wanalijua hili na wapo ambao wamefikia hatua hadi ya kunifuata ' Private ' na kusema kuwa nasema ukweli na kwamba Mimi siyo Mnafiki hadi kusema kwamba yapo baadhi ya mambo ambayo nikiyaibua basi nao wanayatafakari na ikibidi kuyafanyia Kazi.
Na tena nawaombeni nyote kuwa acheni na msikariri kuwa GENTAMYCINE yupo upande Wenu kwani mnakosea na mnapoteza muda Wenu bure. Tokea nizaliwe na kote nilikopita, kuishi na kufanya mambo yangu sijawahi Kujulikana kuwa Mimi nipo wapi halafu huwa ' sitabiriki ' na sipendi pia ' kutabirika ' kwa hali yoyote ile.
Kwa hili la leo naungana na Rais wangu Dkt. Magufuli kuwa kwa nchi ilipokuwa na ilipofikia acha awatumie hao hao JWTZ na tena naomba nimshauri Mheshimiwa Rais wangu kwamba kama ataona inafaa hata huko mbeleni akiamua sasa Taasisi na Ofisi zote za Serikali na Nyeti hadi maeneo mengine awatumie JWTZ naomba afanye hivyo na Mimi nitamuunga mkono kwa 100% zote.
Nuneni mtakavyonuna ila ' Mwanamume ' nimeshamaliza rasmi na huu ndiyo Msimamo wangu na ndiyo nitakavyokuwa daima.