Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

Umewahi kufuga kwa uchache nkimaanisha unaexperience hiyo? pia kuku unauzoefu nao mkuu?.....

Kama hauna experience ni vyema ukavifanya hata kwakuwa na nguruwe 2 na kuku hata 10 na nyanya uzilime kama kibustani kwako ili ujue changamoto ili ukiingia uweze kuifanya project yako kwa viwango vzuri na ufanikiwe maana kuacha kazi na kuingia kujiajiri inamaanisha unauhakika hautaflot account yako mkuu.....

Idea ya nguruwe na kuku ninayo pia....

Ninachijua kinyesi cha kuku unaweza kigeuza kuwa chakupa cha nguruwe,

Ni vzuri kulima mahindi ili badae uyabaraze yawe chakula cha kuku yanaounguza sana cost.

Ujifunze na uwe vizuri katika upandaji fodder za ngano, mahindi etc ili kuokoa kiasi cha fedha za chakula

Tumia sana mbegu bora za kizungu kama large white, durocs hizo ndizo zinazaa watoto 11 -12 etc na zina nyama nyingi.....

Kuku changanya kuroiler na kienyeji ili upate kuku wakubwa wemye uwezo wa kutaga na kuhatamia pia wanaouzika kwa urahisi sokoni....

Jitajidi usolve suala la maji mapema

Kuna majani ya mihogo, majani yanayoota juu ya maji, migomba ya ndizi hivyo vyote vikichemshwa ni vyakula vya nguruwe.... Unaweza panda mugomba mingi ikakusaidia kuokoa cost pia.....

Ukue utaratibu wa nguruwe kula ni mara 2 asubuh na jioni na nini wanakula mchana (wanapaswa wanywe maji kwa wingi sana)

Kuna aina ya mabanda yanayosaidia sana ukuaji wa nguruwe na kuku...

Pia fahamu hata kutengeneza mashine ya kutotoresha ya mayai 50( home made incubators itakupa faida kubwa sana katika ufugaji wako

Pia ujue kurecycle vifaa mbalimbali kwenye shamba lako kama utaweza geuza matairi kuwa kama vyombo vya kunyweshea maji kama utaweza tengeneza sprinter ya kumwagilia kwa kutumia mpira wa maji ya vyupa vya soda itakuwa vizuri...

Jitahidi sana kuwa creatibe kwakila kitu na kakila kifaa ili uokoe fedha na upate faida na bidhaa bora zaidi
 
Mkuu mii nilifanya hayo maamuzi ya kijasiri miaka 30 iliyopita nikiwa bado kijana.
Sikurudi nyuma na sijutii kuacha kazi serikalini.
Mi ilikuwa tofauti katika mtazamo wangu.
Sikuwa na hata senti tano nilipoacha kufanya kazi, lakii nilijiwekea malengo kuwa nikitengeneza fedha sawasawa na mshahara wangu kwa mwezi, basi nimevuka malengo.
Nilitengeneza zaidi ya mara kumi ya mshahara wangu na ikanipa motisha wa kutisha na kiwewe!
Sikutazama nyuma aslilani, na wenzangu niliowaacha kazinisasa hivi naweza kuwaajiri.
 
Hongera sana mkuu,nipo mbioni na mimi.
Baada ya kupitia mawazo ya watu nimeona nisiache kazi kwanza bali niwatoe watoto kwenye shule za kulipia ili nipate capital ya kuanzisha mradi hapa nyumbani huku nikijipanga kuacha kazi.
 
Asante sana Mungu akubariki sana
 
Nashukuru sana kwa mchango wako mkuu.
 
Kuajiriwa sio kubaya na kujiajiri pia ni jambo jema sana.Hakuna mjanja wala mjinga kuliko mwenzake endapo utaamua kuwa katika mojawapo ya makundi haya mawili.
Soon na mimi namaliza mkata wangu na nategemea kuingia katika kuifukuzia ndoto ya maisha yangu ambayo ndani yake naamin nitapata uhuru wa kipato na self fullfilment pia.
 
Kila la kheri sana mkuu
 
1.Biashara inahitaji mda wa kukua
2.kilimo cha nyanya hakitaki uzembe na kinahitaji mtaji mkubwa.

Nyanya inaweza kukutoa lkn laZima ukubAli kuwa na roho ngumu utashinda shamba sana unaogesha mimea na dawa kwa sana,utatumia pesa sana kwahiyo ni bora hizo nyanya walau utoe kwenye msimu wa hela mweZi wa 1,2,3

Zao lenye bei za uhakika ukiweka store ni maharage

Ufugaji wa kuku usitarajie makubwa hasa mwanzoni

Ushauri wangu
1.Km utagusa eka ya nyanya uwe na million 1.5-3 mfukoni kulingana na eneo ulilopo chini ya hapo utakuwa unaletea utani nyanya itakupiga za uso mpk ushangae.Shambani weka mweZi wa 10-11.5.

2.Zao la kuweka store iwe maharage bei isizidi 22000 debe(usafiri+gunia+gharama za kununua).Kama mahindi debe liwe 3000-4500 kwa gharama zote

3.Kuku

Pata eneo kubwa la kuwaachia huru wanakula asubuh then wanaenda zao

4.Panda pilipili kali na nyanya nyungu miche 2000 kwa kila zao

Wewe unahitaji hela za mara kwa mara za kuendeshea hago mazAo mawili hayana gharama kubwa hlf yaweza kukupa hela za mara kwa mara za kufanyia mradi mkubwa.

Tenga kibustani mchwara cha kukupa 5000 kwa siku

Note:Sio lelemama unachotaka kufanya,kilimo cha nyanya hakipatani na mtaji mdg,mazao ya kukupa hela za mara kwa mara ni LAZIMA na sio Muhimu tu.
 
Hiyo ni risk kubwa sana. Kwani huwezi kuchukua mkopo?
Kampuni ninayofanyia kazi haijatuwekea mazingira mazuri ya kukopa mkuu,ila pamoja na hayo nimepata suluhisho ambalo ni kuwapeleka watoto shule za kawaida ili niweze kupata mtaji.
 
Mkuu nakushukuru sana kwa ushauri wako...nitaufanyia kazi mkuu.
 
Kwanini usingeanza
Kwanini usianze kwaa kulima muda huu wakati bado unafanyakazi.Anza kwa awamu mdogo mdogo upate uzoefu
 
Japo haukuwa ushauri wangu ila nimepata kitu kikubwa sana. Thanks brother Mungu akubariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…