Wadau, nimeona maoni ya wadau mbalimbali kuhusu kile kinachoitwa Maridhiano, wengine wakipinga, wengine wakiyaunga mkono na kila kundi likitoa sababu zake. Nimeona CHADEMA wametoa Masharti ya awali (pre conditions) kama 3 za Maridhiano
1. Mwenyekiti Lissu Aachiwe huru pamoja na wafungwa wote wa kisiasa
2. Msuluhuhishi huru
3. Katiba mpya.
Mimi siyo mwana siasa, ila nadhani kuna haja ya kuboresha hizi hoja ili ziwe na mashiko na kuleta maana. Kwanza napendekeza kugawanya hoja katika makundi matatu na nadhani ni vyema kutofautisha haya makundi ya hoja.
1. Kwa nini Maridhiano? Sababu inayo lazimisha kuwepo na maridhiano ni ipi?
2. Masharti ya Awali (Pre conditions)
3. Matarajio (Expected Results/Delivarables)
Tuanze na namba 1. Kwa nini Maridhiano.
Inafahamika kuwa maridhiano hayako kikatiba, wala si sehemu ya uchaguzi. Hakuna mahali ambapo imeandikwa kuwa Watanzabia wakitoka kwenye uchaguzi utafuatiwa na maridhiano.
Kwa mtazamo wango tunahitaji maridhiano kwa sababu Uchaguzi ulivurugika. Hii ndo hoja ya msingi kwa nini tunahitaji maridhiano. Kama uchaguzi usinge vurugika tusinge hitaji maridhiano.
Tunahitaji maridhiano kwa sababu uongozi ulipo haukuingia madarakani kihalali hivyo kufanya uwe haramu.
2. Masharti ya awali.
Kama nilivyo eleza hapo juu masharti ya msingi kabla ya kuanza maridhiano yanatakiwa yawe yafuatayo
1. CCM kukiri kwamba uchaguzi ulivurugika na hivyo kuna haja ya kuandaa uchaguzi upya. Hatu hitaji kuwa na maridhiano kama uchaguzi ungekwenda vizuri.
2. Kuwe na msuhulishi huru. Maridhiano yoyote lazima yawe na msuhuhishi ambaye hatokani na pande zinazotofautiana.
3. Kuwe na muda maalumu (fixed time frame). Hii itaepusha CCM kurefusha maridhiano ili kuvuta muda hadi miaka 5 iishe. Hivyo kabla ya kuingia na kuanza maridhiano lazima kuwe na muda uliokubaliwa kwamba maridhiano hayatazidi miezi kadhaa.
4. Kuwaachia huru wafungwa na mahabusu wote wa kisiasa.
3. Matarajio ya maridhiano.
Matarajio ni mambo ambayo tunategemea kuyapata kama zao la maridhiano. Haya ni baadhi ya matarijio.
1. Kwa kuwa serikali iliyopo madarakani haikuingia kwa njia ambayo ni halali baada ya kuvurugikakwa uchaguzi, hivyo matarajio ya maridhiano ni moja kati ha haya:
a. Kuipa ridhaa(uhalali) serikali kuendelea kwa muda uliobakia
b. Kuunda serikali ya mpito
2. Kukubaliana jinsi ya kuandaa na kutekeleza mchakato wa katiba mpya na mabadiliko ys sheria za uchaguzi.
3. Kukubaliana tarehe na jinsi ya kurudia uchaguzi.
4. Makubaliano ya jinsi ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wale wote walioendesha na kutekeleza vitendo vya utekaji, uuwaji, waliosababisha kuvurugika uchaguzi, na walio endesha mauaji kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Hivyo basi
Ni muhimu kwa CHADEMA kwa niaba ya wananchi kuandaa Hati ya Majadiliano, Memorundum of Negotiation itakayo eleza haya mambo niliyosema hapa pamoja na mengine kwa upana wake na kuwasilisha kwa msuhuhishi huru atakae teuliwa na kukubaliwa na pande zote.
Kuhusu upatikanaji wa Msuhuhishi huru.
Serikali iwaandikie Commonwealth au SADC kuomba kupatiwa mpatanishi.
Hivyo CHADEMA kwa sasa hasiseme hawaingii kwenye mariadhino ila, waseme wako tayari kwa maridhiano iwapo hati ya majadaliano itajumuishwa haya mambo niliyo pendekeza.