Komando ni askari aliyepitia mafunzo maalumu (special trainings) kumfanya awe na uwezo maalumu wa ziada wa kufanya mambo zaidi ya askari wa kawaida kwa jina la kimombo wanaitwa special forces. Mfano mzuri ni SAS (wa uingereza) na SEAL TEAM SIX ( Wa USA).
Katika medani za kivita, askari wa kawaida mara nyingi hupigana kuelekea upande wa adui, lakini komando yeye amefunzwa namna ya kupigana akiwa anatoka kwa adui kwenda upande wa kikosi rafiki. Hapo namaanisha kuwa komando anauwezo wa kujirinda na kushambulia kwa wakati mmoja..! Kuna kipindi komando inabd apambane akitokea nyuma ya adui (behind the enemy line) na hapo ndipo linapokuja somo la namna ya kutua na parachuti (paratrooper trainings).
Wenzetu marekani wameendelea kiasi cha kwamba wana vikosi vingi sana ambavyo vinaweza visiwe vya makomando (kwa definition yao) ila vinafanya kazi sawa na makomando mfano Green berets , delta force nk.
Katika jeshi la nchi yoyote, mara nyingi makomando huwa ni wachache ukilinganisha na askari wote. Unaweza kukuta kwenye jeshi la askari 15,000 makomandoo wakawa wasizidi 1000 pekee. Hii hutokana na namna wanavyopigana katika medani za kivita, mara nyingi section ya komando huwa haizidi watu saba na ndo hao hao wanaotumwa kufanya mission ngumu. Lakini pia gharama za kufunza kamando mmoja inaweza kugharamia mafunzo ya askari watatu wa kawaida.
Kuna story zisizo na uhakika nilizisikia kuwa "eti" kipindi nchi yetu inaingia vitani na nduli iddi amin dada jeshi letu lilikuwa na takribani makomando mia tano (500) pekee so nadhani unaweza kupata picha ya shughuli na uwezo wa makomando.
Komando huwa wanakazi maalumu ya kuhakikisha kuwa askari wa kawaida wanafanya majukumu yao bila ya kupata shida zinazo epukika, hapo huweza kufanya sabotage missions ( shambulio la hila) ili kupunguza kasi ya adui asifikie (delaying) kikosi rafiki na hapa humaanisha ulipuaji wa madaraja, silaha, maangamizi, ghala la chakula cha adui au hata vifaa vya usafirishaji wa adui kwa kutumia mabomu lakininpia huweza kutumwa katika rescue missions (misheni za kukomboa mateka) nk.
Mara nyingi komando hupatikana baada ya askari wa kawaida kumaliza mafunzo yao na hapo huchaguliwa baadhi yao wenye sifa zitakazo muwezesha kuhimili mikikimkiki ya mafunzo ya ukomando. Kwa tanzania sifahamu mafunzo huchukua kwa muda gani ila huko dunia ya kwanza mafunzo huwa ni kuanzia miezi tisa mpaka miaka miwili kilingana na mahitaji ya askari hao..
Hata aina ya silaha anayotumia komando ni tofauti na silaha anazobeba askari wa kawaida, sijui kwa tanzania ila ukienda marekani special forces wao mara ya mwisho kuangalia walikuwa wanatumia silaha aina ya M16 na niliwahi sikia kuwa wanampango wa kubadirisha.
Kama utakuwa mfatiliaji wa mambo utakuwa unaahamu kuwa jeshi hugawanyika kwenye makundi matatu kulingana na mafunzo waliyopitia kuna askari wa miguu(infantry division) ambayo hii ndo tunasema katika jeshi lolote infantry huwa ni wengi zaidi kuliko division nyengine, pia kuna Air division (kikosi cha anga), Navy (kikosi cha Maji), lakini pia kuna watu wa mizinga na vifaru ambao hawa wakati mwengine huingizwa kwenye infantry. Sasa basi makomando huwepo pia katika kila division, namaanisha ya kwamba kuna komando wa anga, maji na pia ardhi.
Kutokana na umuhimu na uwezi wa makomando kumeibuka story mbali mbali kuelezea uwezo wao kwenye medani. Zinaweza kuwa zina ukweli au zikawa ni ngano tu, yote kwa yote kwa yote wao wenyewe (komando) na wale wenye security clearance inayowaruhusu kuona uwezo wao ndo wanaojua ukweli wa mambo.. Sie wengine tutabaki kuhisi tu!
Ubavu