Hiyo ni Regulator haihusiani na Mtungi wa GESI kazi ya REGULATOR ni kupima kiwango cha Pressure ya Gesi iliyopo ndani ya mtungi na kulingana na Pressure iliyopo REGULATOR itakuonyesha mshale upo wapi.
Green Gas yako Pressure imejaa vizuri haina shida kadri unavyoendelea kutumia mshale utashuka kuitafuta RED.
RED mshale ukiwa eneo hilo maana yake gesi yako inaisha muda wowote hivyo unatakiwa ujiandae kisaikolojia na kipesa maana muda wowote jiko linazima.
Yellow Mtungi wa gesi unajazwa gesi ndani kwa kipimo maalum,kile kipimo ni either kiwe kawaida (green) au kiwe chini kiishe (red) lakini ikiwa kwenye yellow maana yake huo mtungi umezdshwa pressure ni wa kurudsha uliponunulia na wao waurudshe kiwandani,ni makosa toka kiwandani (ni nadra sana kutokea japo hutokea)
REGULATOR haihusiani na ujazo wa gesi ndani ya mtungi wako,Hiyo Picha inaonyesha mshale upo kwenye green maana yake gesi yako ina pressure nzuri ipo safi kwa matumizi
Kuhusu GESI imejaa au haijajaa,Unapaswa pale unaponunulia mtungi wako wa gesi upime kwenye mzani Ujazo wa Mtungi wa gesi unaochukua.
Najua unatumia Mtungi mkubwa Mitungi yote ya GESI ina Namba zimechorwa zikiwa na maana Tofauti
ORYX = Mitungi yao utaikuta ina namba
(30.5,30.1,29.7,30.3,nk) = Namba hizi ni za Jumla ya GESI iliyojazwa ndani ya mtungi na Hilo lichuma ambalo tunaliita mtungi.
Namba zingine utakazozikuta kwa Mtungi wa Oryx ni
(21,22,23,24,25) = Zinakuaga zimezungushiwa DUARA hizi namba maana yake ni mwaka wa Huo mtungi unaotumia ulitengenezwa Mwaka gani, kwahyo hii ni MIAKA inayomaanisha huo mtungi wako ni lini ulitoka kiwandani.
(15.5,14.7,15.3,20,nk) Hizi namba zinamaanisha Uzito wa Hilo Chuma lililojaza GESI kwahyo ukiziona hizi namba ujue ni uzito wa hilo lichuma lenye gesi, ukitumia mtungi wako ukaisha gesi ukienda kuupima uzito Utapata jibu ambalo ni namba iliyoko kwenye huo mtungi.
Uzito wa GESI mtungi mkubwa YOTE ni 15kg bila kujali umbo,rangi,size,nk mitungi yote ya size ya kati GESI iliyopo ndani ni 15kg
UTAJUAJE GESI IMEJAA AU PUNGUFU UNAPOKUA KWA Muuzaji WAKATI ANAKUPIMIA GESI?
Angalia namba Kubwa Juu ya Mtungi wako zile zinazojumlisha MTUNGI + GESI za juu kabisa mkipima kwenye mzani basi mzani ukupe jibu sawa na namba unayoona.
Mtungi wako ukichorwa 30.5 na mzani usome 30.5 au 29. 5 and above not below
Mtungi ukisoma 29.7 na mzani usime 29.7 au 28.5 and above that not below
hapa tunarudi hesabu za approximation shule, sio lazima mzani usome exactly number printed on a cylinder ila tunajua any number above 5 in decimal tunaipeleka mbele... Tusikariri "tuelewe"
UNAJUAJE MTUNGI WAKO UNAVUJA UNAPOUNUNUA KABLA HUJAUFUNGA REGULATOR?
Bandua seal ile karatasi pale juu kisha usiweke regulator mwagia maji pale juu ya mtungi wako utaona bubles vipulizo vidogo vidogo, ukiona hivyo Yawezekana mtungi unavuja.
Ili kuhakikisha, Chukua kitu chembamba kama kijiti au toothpick bonyeza kile kichuma ili gesi itoke kdg tu italia psssssiiii then mwagia tena maji ukiona bubbles hapo Jua Mtungi unavuja.
Unaweza ukaurudsha Uliponunua au kama Una utaalamu basi ukafunga tu Regulator then ukai control gesi kupitia regulator (haushauriwi,hii wafanye ma PRO kwenye GESI) wewe ukiona mtungi unavuja rudisha Dukani.
MWISHO