Huu mtaa unanishinda tabia

Veronica7598

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
361
408
Habari zenu wapendwa wangu.

Ndugu zangu huu mtaa ninaoishi ni majanga mtupu, nimezungukwa na WAMBEA KUPITA MAELEZO, ni majiran zangu lakini wanapenda sna kufatilia maisha ya watu.
Yaan wanataka wajue leo umepika nn, ndani kwenu kunaendelea nn. Wakimuona mume wangu karudi kutoka job, wanamtuma mtoto nenda kasikilize wanaongea nn,

Hapa kwangu ninamtoto wa wifi yangu tumemchukulia uhamisho anasoma hapa kwangu, wanaaanza kutusema mtoto wao anasoma English medium mtoto wa wifi yke amempeleka st. kayumbo, alafu huwezi mtoa mtoto wa darasa la tano st kayumbo ukampeleka english medium yaan hata pata kitu nikayasikia nikawapotezea.

Mwezi ulioisha huby alikua likizo wakaanza vicheko yaan, hawajui mambo ya likizo wakaanza kusema Magufuli amemtumbua , saiz hana kazi wanakazi ya kuangalia tamthilia na kucheza karata na bado, watacheza mpaka rede mwaka huu wanatusema mpaka kero, hubby anasema achana nao hao dawa yao ntawakea ukuta mrefu mpaka watataman kutuona.

Hatuwezi kuhama kwan ndo kwetu, tumehamia mwaka jana. Wakiona hawakuoni nje wataanza kuja kuomba, huyu kaomba chumvi, huyu kaona mchuzi yaaani shida kwelikweli, ubaya sasa mm sina time nao wanaanza kusema naringa, mala najiona mzuri yaaan ili mradi tyu wakuchafue roho.

Sasa hv nina ujauzito yaan mtaa mzima wanajua ninaujauzito story ni zangu, wanaanza kusema wazigua kwa kuzaaa hawachekan na wapemba, mtoto wao mdogo washambebea mimba, na ukiangalia first born wangu ana miaka mitatu.

Nipeni ushauri nifanye nn, ili niepuke na majungu yao.
Mnisamehe kwa story ndefu.
 
Hata wewe umeleta umbea humu, umeshindwa nini kwenda kuwambia haya yote unakuja kutoa povu humu, haya humu kuna jirani yako yoyote??

Au ulitaka tujue kuwa una ujaauzito!!!

Harafu huyo mtoto anasomea kwako!! Au anasoma kwako?

Umbea mwingine bila picha haunogi kabisa.
 
Jaribu kuwa busy na mambo yako being ideal sometymz ndio inakupa access ya kujuwa wanasema nini. Ukiwa busy huwez pata hata tym nao mda utakao kuwa nao uta angalia familia yako mwingine unapiga kazi. So ongeza juhudi kweny ubusy na shughuli
 
Habari zenu wapendwa wangu.

Ndugu zangu huu mtaa ninaoishi ni majanga mtupu, nimezungukwa na wasambaa WAMBEA KUPITA MAELEZO, ni majiran zangu lakini wanapenda sna kufatilia maisha ya watu.
Yaan wanataka wajue leo umepika nn, ndani kwenu kunaendelea nn. Wakimuona mume wangu karudi kutoka job, wanamtuma mtoto nenda kasikilize wanaongea nn,

Hapa kwangu ninamtoto wa wifi yangu tumemchukulia uhamisho anasoma hapa kwangu, wanaaanza kutusema mtoto wao anasoma English medium mtoto wa wifi yke amempeleka st. kayumbo, alafu huwezi mtoa mtoto wa darasa la tano st kayumbo ukampeleka english medium yaan hata pata kitu nikayasikia nikawapotezea.

Mwezi ulioisha huby alikua likizo wakaanza vicheko yaan, hawajui mambo ya likizo wakaanza kusema Magufuli amemtumbua msukuma mwenzake, saiz hana kazi wanakazi ya kuangalia tamthilia na kucheza karata na bado, watacheza mpaka rede mwaka huu wanatusema mpaka kero, hubby anasema achana nao hao dawa yao ntawakea ukuta mrefu mpaka watataman kutuona.

Hatuwezi kuhama kwan ndo kwetu, tumehamia mwaka jana. Wakiona hawakuoni nje wataanza kuja kuomba, huyu kaomba chumvi, huyu kaona mchuzi yaaani shida kwelikweli, ubaya sasa mm sina time nao wanaanza kusema naringa, mala najiona mzuri yaaan ili mradi tyu wakuchafue roho.

Sasa hv nina ujauzito yaan mtaa mzima wanajua ninaujauzito story ni zangu, wanaanza kusema wazigua kwa kuzaaa hawachekan na wapemba, mtoto wao mdogo washambebea mimba, na ukiangalia first born wangu ana miaka mitatu.

Nipeni ushauri nifanye nn, ili niepuke na majungu yao.
Mnisamehe kwa story ndefu.
Hao hutakiwi kushughulika nao na ikiwezekana hata ukiwa na nafasi ya kuwapa zawadi wapatie! Ukishughulishwa na wanachoongea utatengeneza B.P, kisukari n.k bila sababu za msingi maadam hawarushi ngumi wewe wapotezee sababu kukasirika kwako ndiyo kutimia kwa malengo yao.
 
Wapotezee atakuja kuhamia jirani mwingine watakua na issue zake Zaidi kwani za kwako watakua wamezizoea. Lakini hao my home people inaelekea hawana maisha dizaini.
 
Wekeni fensi la maana ,hata hivyo ukiona wanawachosha wafungieni vioo.
 
Hiyo tabua sio kwa wasambaa tu mimi huku ninaishi na jirani zangu hata sijui kabila zao ila nasikia wengine ni watu wa kusini. Nilihamia nyumbani kwangu niliezeka vyumba viwili tu wakaanza kusema eti mnajenga majumba makubwa halafu yanawashinda. Sasa baada ya kuimaliza na kuweka uzio wanaanza tena maneno yasiyo na tija katika ustawi wa jamii ya leo. Amepata wapi hela za ghafla namna ile sio bure huyu atakuwa fisadi au anauza madawa. Hizi habari huwa zinamfikia wife na huwa anakuja kunipa taarifa. Ila kiukweli maneno mengine yanakera sana lakini namwambia wife take it easy though hata mimi naumia.

Nimeamua kujenga sehemu nyingine ili nihame hapa ninapoishi sasa hivi na bahati nzuri eneo nililopata nimeona wanaojenga asilimia kubwa ni wale wenye uwezo wao kifedha . Hii tabia ya kuchunguzana wanayosana watu wenye vipato vya chini ambao hawana kazi za uhakika na hawajui kesho watakula nini! Siruhusu mtu kutoa chumvi wala mchuzi hayo maisha sijayazoea kabisa.

Usiwalaumu hao wasambaa tu angalau ndio sifa yao kubwa huo umbea ila wapo pia wa makabila wengine hasa wale wasio na shughuri za kufanya.
 
Wapotezee atakuja kuhamia jirani mwingine watakua na issue zake Zaidi kwani za kwako watakua wamezizoea. Lakini hao my home people inaelekea hawana maisha dizaini.
Ulijuaje yaan maisha yao msosi mala moja, hali yao duni balaaa wakiishiwa wanakuja kwangu kuomba msaaada mpaka nawaza wakija niwapotezee tu ili waseme vzr.
 
Back
Top Bottom