Huu mtaa unanishinda tabia

Huu mtaa unanishinda tabia

Samahan hvi Hayo yote wanayozungumza umeyajuaje kama hauna muda nao?
Yaaan hawana haya, wanaongea unawasikia kabisaaaa. Wala hawajifichi wanakusema live ila hawakutaji jina ila kama unaakili unajua dongo langu hilo.
 
Hiyo tabua sio kwa wasambaa tu mimi huku ninaishi na jirani zangu hata sijui kabila zao ila nasikia wengine ni watu wa kusini. Nilihamia nyumbani kwangu niliezeka vyumba viwili tu wakaanza kusema eti mnajenga majumba makubwa halafu yanawashinda. Sasa baada ya kuimaliza na kuweka uzio wanaanza tena maneno yasiyo na tija katika ustawi wa jamii ya leo. Amepata wapi hela za ghafla namna ile sio bure huyu atakuwa fisadi au anauza madawa. Hizi habari huwa zinamfikia wife na huwa anakuja kunipa taarifa. Ila kiukweli maneno mengine yanakera sana lakini namwambia wife take it easy though hata mimi naumia.


Nimeamua kujenga sehemu nyingine ili nihame hapa ninapoishi sasa hivi na bahati nzuri eneo nililopata nimeona wanaojenga asilimia kubwa ni wale wenye uwezo wao kifedha . Hii tabia ya kuchunguzana wanayosana watu wenye vipato vya chini ambao hawana kazi za uhakika na hawajui kesho watakula nini! Siruhusu mtu kutoa chumvi wala mchuzi hayo maisha sijayazoea kabisa.

Usiwalaumu hao wasambaa tu angalau ndio sifa yao kubwa huo umbea ila wapo pia wa makabila wengine hasa wale wasio na shughuri za kufanya.
Ahsante kaka kumbe hata kwenu wapo, maaana nataman niuze nyumba nikapangishe raskazone kwenye watu wenye akili zao
 
Kwan nyumba unayoishi nikoje?
Ipo karibu na barabara wakiwa wanaenda town wanasubilia daladala karibu na kwangu, yaan wamegeuza kituo cha daladala kwaiyo wakisubili huku wanakupa madongo wanajifanya wanamema mtu, kumbe ni ww unasemwa bila kujijua
 
Pole sana kwi kwi kwi kwi utakua unakaa uswazi sana izo ni roho za kimasikini uzeni iyo nyumba mkajenge sehem kama goba au madale kule kidogo kuna middle class hawana mambo hizo
 
Nimejilazimisha kuchangia, lakini huu uzi ni kama unahusu jinsia furani. Kifupi Dada hata wewe waonyesha ni mbea ila wenzako wamekuzidi maarifa. Kwa kifupi acha umbea ili ufanye yako kwa amani. ukipenda kuwafatilia watu nao watakufatilia tu.
 
hayo mambo ni kawaida,ni sawa saiv mkuu wa nchi anavyolaumiwa,ndio ivo ivo hata atawale mungu bado atalaumiwa tu,sembuse wewe kusemwa,shukuru kuwa kumbe unaonekana hadi watu wanapata nafasi ya kukusema,wengine wanapenda kuipata hiyo nafasi ya kusemwa/kuzungumziwa ila hiyo nafasi hawaipati,hongera kwa kusemwa shemeji..
 
Habari zenu wapendwa wangu.

Ndugu zangu huu mtaa ninaoishi ni majanga mtupu, nimezungukwa na wasambaa WAMBEA KUPITA MAELEZO, ni majiran zangu lakini wanapenda sna kufatilia maisha ya watu.
Yaan wanataka wajue leo umepika nn, ndani kwenu kunaendelea nn. Wakimuona mume wangu karudi kutoka job, wanamtuma mtoto nenda kasikilize wanaongea nn,

Hapa kwangu ninamtoto wa wifi yangu tumemchukulia uhamisho anasoma hapa kwangu, wanaaanza kutusema mtoto wao anasoma English medium mtoto wa wifi yke amempeleka st. kayumbo, alafu huwezi mtoa mtoto wa darasa la tano st kayumbo ukampeleka english medium yaan hata pata kitu nikayasikia nikawapotezea.

Mwezi ulioisha huby alikua likizo wakaanza vicheko yaan, hawajui mambo ya likizo wakaanza kusema Magufuli amemtumbua msukuma mwenzake, saiz hana kazi wanakazi ya kuangalia tamthilia na kucheza karata na bado, watacheza mpaka rede mwaka huu wanatusema mpaka kero, hubby anasema achana nao hao dawa yao ntawakea ukuta mrefu mpaka watataman kutuona.

Hatuwezi kuhama kwan ndo kwetu, tumehamia mwaka jana. Wakiona hawakuoni nje wataanza kuja kuomba, huyu kaomba chumvi, huyu kaona mchuzi yaaani shida kwelikweli, ubaya sasa mm sina time nao wanaanza kusema naringa, mala najiona mzuri yaaan ili mradi tyu wakuchafue roho.

Sasa hv nina ujauzito yaan mtaa mzima wanajua ninaujauzito story ni zangu, wanaanza kusema wazigua kwa kuzaaa hawachekan na wapemba, mtoto wao mdogo washambebea mimba, na ukiangalia first born wangu ana miaka mitatu.

Nipeni ushauri nifanye nn, ili niepuke na majungu yao.
Mnisamehe kwa story ndefu.
mtaa gani huo?
 
Geuza hiyo vituko vyao iwe ndiyo burudani, wataacha tu.
 
Nimejilazimisha kuchangia, lakini huu uzi ni kama unahusu jinsia furani. Kifupi Dada hata wewe waonyesha ni mbea ila wenzako wamekuzidi maarifa. Kwa kifupi acha umbea ili ufanye yako kwa amani. ukipenda kuwafatilia watu nao watakufatilia tu.
Pole kwa kujilazimisha coz hukutumwa wala kulazimishwa na sio kila story inayopita mbele yko ucoment nyingine pita kimya kimya tu.
 
Ahsante kaka kumbe hata kwenu wapo, maaana nataman niuze nyumba nikapangishe raskazone kwenye watu wenye akili zao
Mkuu nadhali utakuwa unaishi AR? Pande zipi? Mi naishi mianzini nakumbwa na maswaibu kama yako; watoto wangu (2), wote wanasoma Int'l schools; mmoja ISM (Kisongo) & mwingine St. Constatine; na kwa uwezo wa mungu wote nawalipia transport i.e wanafwatwa na magari ya shuleni kuwachukua na kuwarudisha nyumbani; sasa nikitoka na wife nawaona machoni mwao kama kuna mada inaendelea juu ya familia yangu (ukichukulia mm na wife tupo early 30's), imefika wakati nikileta hata h/girl akienda dukani tu, wa naanza kumuhoji juu ya maisha yangu na familia, hadi h/girl anamwambia wife mbona nkifika madukani watu wananihoji juu ya mnaisha yetu? Any way ninaplan B, ya kujenga njiro niachane na uswazi. Ubinadamu kazi; nimejenga kwangu; mm na familia yangu hatumlilii mtu njaa;tunakazi mm na wife, maisha yanasonga. Ila majirani ss.........
 
Dawa nzuri kuliko zote toka asubuhi rudi usiku.
 
Back
Top Bottom