Huu mtaa unanishinda tabia

Huu mtaa unanishinda tabia

Ukipigwa vita sana na watu jua kabisa ww uko zaidi ya wao...

Akili kichwani mwako ,tumia maneno yao kama chachu ya kukufanya usonge mbele na wala usitumie kama ngazi ya kujishusha ,

Dunia hii si pepo kusema utaishi kwa raha katika kila nyanja
 
aisee! mie majirani zangu hata siwajui labda tunao sali nao Jumuiya! siku moja Katibu alitangaza kuwa Jumamosi ijayo tutasali kwa Michael, nikawa wa kwanza kumuomba Katibu atoe maelekezo ni wapi! nilishangaa watu wote wanacheka! Lahaula! kumbe ni jirani yangu tunayetizamana! ahahahaah
 
uskubali kusikia ya kuambiwa......... mimi hata sijui kama wananisema sababu hata siambiwagi teh ..
Ulikuwa unanikwaza ukija kuomba kuchota maji huku umevaa sweta lako la shule lililofumuka mikononi!
 
Jenga ukuta alaf fuga mbwa wakali hatarr..alaf nawewe anayekwambia ni nani
 
Piga mmoja wapo watajuzana maana c wambea, na wataacha kabis hata me nilifanya hivyo
 
Fanya yako mama Wambeya wapo kila mahali, usiwaruhusu kabisa wakukoseshe raha katika ndoa na maisha yenu hivyo kukuweka roho juu. Wadharau tu.
 
zungusha ukuta wa futi 7 alafu poga kimy
siyo lazima ya ukuta mrefu na wactofali. wee weka wa seng'eng'e na nguzo za zege au miti ile isiyooza wanayojengea vyoo vya shimo au zilizowekwa dawa na geti ambalo lina uwazi chini na juu amalo mtu hawezi kuruka halafu panda ile maua ya miiba kuzunguka utaishi kwa amani kwa gharama ndogo ya uzio
 
kwanza nyie si watani,

hayo yatakua ni utani wa jadi hata usichukie
 
Dawa ya machakubimbi ni kufanya maendeleo sio kuingia vita nao
 
Hao ni wajinga na mjinga ukimjibu anavimba kichwa, waache, ni maeneo gani?.
 
Dah
Habari zenu wapendwa wangu.

Ndugu zangu huu mtaa ninaoishi ni majanga mtupu, nimezungukwa na WAMBEA KUPITA MAELEZO, ni majiran zangu lakini wanapenda sna kufatilia maisha ya watu.
Yaan wanataka wajue leo umepika nn, ndani kwenu kunaendelea nn. Wakimuona mume wangu karudi kutoka job, wanamtuma mtoto nenda kasikilize wanaongea nn,

Hapa kwangu ninamtoto wa wifi yangu tumemchukulia uhamisho anasoma hapa kwangu, wanaaanza kutusema mtoto wao anasoma English medium mtoto wa wifi yke amempeleka st. kayumbo, alafu huwezi mtoa mtoto wa darasa la tano st kayumbo ukampeleka english medium yaan hata pata kitu nikayasikia nikawapotezea.

Mwezi ulioisha huby alikua likizo wakaanza vicheko yaan, hawajui mambo ya likizo wakaanza kusema Magufuli amemtumbua , saiz hana kazi wanakazi ya kuangalia tamthilia na kucheza karata na bado, watacheza mpaka rede mwaka huu wanatusema mpaka kero, hubby anasema achana nao hao dawa yao ntawakea ukuta mrefu mpaka watataman kutuona.

Hatuwezi kuhama kwan ndo kwetu, tumehamia mwaka jana. Wakiona hawakuoni nje wataanza kuja kuomba, huyu kaomba chumvi, huyu kaona mchuzi yaaani shida kwelikweli, ubaya sasa mm sina time nao wanaanza kusema naringa, mala najiona mzuri yaaan ili mradi tyu wakuchafue roho.

Sasa hv nina ujauzito yaan mtaa mzima wanajua ninaujauzito story ni zangu, wanaanza kusema wazigua kwa kuzaaa hawachekan na wapemba, mtoto wao mdogo washambebea mimba, na ukiangalia first born wangu ana miaka mitatu.

Nipeni ushauri nifanye nn, ili niepuke na majungu yao.
Mnisamehe kwa story ndefu.
Dah! Pole sana.
 
Back
Top Bottom