Huu mtaa unanishinda tabia

Huu mtaa unanishinda tabia

Dawa ni kuwapotezea fanya yako dia..... Yaani me napenda kweli kuongelewa najionaga bonge ya mwanamke.. Nikipita nawapa salamu nzuuuuuri... Nimemaliza. Watachoka wenyewe
 
Dawa ya wambea ni kutokuwajibu tu....mwisho wa siku wanajiona wajinga
 
Mkuu nadhali utakuwa unaishi AR? Pande zipi? Mi naishi mianzini nakumbwa na maswaibu kama yako; watoto wangu (2), wote wanasoma Int'l schools; mmoja ISM (Kisongo) & mwingine St. Constatine; na kwa uwezo wa mungu wote nawalipia transport i.e wanafwatwa na magari ya shuleni kuwachukua na kuwarudisha nyumbani; sasa nikitoka na wife nawaona machoni mwao kama kuna mada inaendelea juu ya familia yangu (ukichukulia mm na wife tupo early 30's), imefika wakati nikileta hata h/girl akienda dukani tu, wa naanza kumuhoji juu ya maisha yangu na familia, hadi h/girl anamwambia wife mbona nkifika madukani watu wananihoji juu ya mnaisha yetu? Any way ninaplan B, ya kujenga njiro niachane na uswazi. Ubinadamu kazi; nimejenga kwangu; mm na familia yangu hatumlilii mtu njaa;tunakazi mm na wife, maisha yanasonga. Ila majirani ss.........
Pole mkuu

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Kosa lako kesi ya gedere umeipeleka kwa nyani. Humu ndo kuna wambea waliokubuhu.
 
Ila pia hata wewe huna kazi, ungekuwa na kazi haya mambo usingeyasikia hata.

Tafuta kitu cha kufanya, acha kukaa idle.
 
Nilichogundua unashinda nyumbani ndiyo maana unakuwa na muda wa kusikiliza maneno, mwambie bwashee akutafutie kazi/biashara ya kufanya uwe busy muda wote, nyumbani upatikane j2. Over
 
Hata wewe umeleta umbea humu, umeshindwa nini kwenda kuwambia haya yote unakuja kutoa povu humu, haya humu kuna jirani yako yoyote??

Au ulitaka tujue kuwa una ujaauzito!!!

Harafu huyo mtoto anasomea kwako!! Au anasoma kwako?

Umbea mwingine bila picha haunogi kabisa.
Nyumba na mimba
 
Nipeni ushauri nifanye nn, ili niepuke na majungu yao.

Jenga ukuta na uweke geti; halafu pale getini weka door entry videophone.

de4tbw_1-330x330.jpg
 
Mbona simple???

Unafunga vioo tu

Wakija kuomba chumvi waeleleze dukani...wakitaka mchuzi waambie hawakuwemo kwenye bajeti
 
Habari zenu wapendwa wangu.

Ndugu zangu huu mtaa ninaoishi ni majanga mtupu, nimezungukwa na wasambaa WAMBEA KUPITA MAELEZO, ni majiran zangu lakini wanapenda sna kufatilia maisha ya watu.
Yaan wanataka wajue leo umepika nn, ndani kwenu kunaendelea nn. Wakimuona mume wangu karudi kutoka job, wanamtuma mtoto nenda kasikilize wanaongea nn,

Hapa kwangu ninamtoto wa wifi yangu tumemchukulia uhamisho anasoma hapa kwangu, wanaaanza kutusema mtoto wao anasoma English medium mtoto wa wifi yke amempeleka st. kayumbo, alafu huwezi mtoa mtoto wa darasa la tano st kayumbo ukampeleka english medium yaan hata pata kitu nikayasikia nikawapotezea.

Mwezi ulioisha huby alikua likizo wakaanza vicheko yaan, hawajui mambo ya likizo wakaanza kusema Magufuli amemtumbua msukuma mwenzake, saiz hana kazi wanakazi ya kuangalia tamthilia na kucheza karata na bado, watacheza mpaka rede mwaka huu wanatusema mpaka kero, hubby anasema achana nao hao dawa yao ntawakea ukuta mrefu mpaka watataman kutuona.

Hatuwezi kuhama kwan ndo kwetu, tumehamia mwaka jana. Wakiona hawakuoni nje wataanza kuja kuomba, huyu kaomba chumvi, huyu kaona mchuzi yaaani shida kwelikweli, ubaya sasa mm sina time nao wanaanza kusema naringa, mala najiona mzuri yaaan ili mradi tyu wakuchafue roho.

Sasa hv nina ujauzito yaan mtaa mzima wanajua ninaujauzito story ni zangu, wanaanza kusema wazigua kwa kuzaaa hawachekan na wapemba, mtoto wao mdogo washambebea mimba, na ukiangalia first born wangu ana miaka mitatu.

Nipeni ushauri nifanye nn, ili niepuke na majungu yao.
Mnisamehe kwa story ndefu.
Wagambile wakadye mibusa ya tati yawe
[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Back
Top Bottom