Huu msemo "Samaki mkunje angali mbichi" uko Real sana

Huu msemo "Samaki mkunje angali mbichi" uko Real sana

Mh! majukumu na labda ukute mwengine kuvaa sio mambo yake!.. wapo wengine kuvaa huwaambii kitu yupo radhi ajinyime kitu fulani fulani ila kuvaa lazima atokee tu!.
So nafikiri hivyo viwili vinachangia yani uchumi na hobby!.
Majukumu yapo ndio lakini ndio hata kujiwekea unasema tu hata kila mwezi nitenge ef10 ya tushet moja,. Au hata 30 mwezi huu unanunua jeans mwezi ujao unanunua kiatu au mwezi unaokuja shati
sio lazima mpaka uwe na laki uingie dukani ukapate vyote kwa pamoja
 
Majukumu yapo ndio lakini ndio hata kujiwekea unasema tu hata kila mwezi nitenge ef10 ya tushet moja,. Au hata 30 mwezi huu unanunua jeans mwezi ujao unanunua kiatu au mwezi unaokuja shati
sio lazima mpaka uwe na laki uingie dukani ukapate vyote kwa pamoja
Basi mfanyie wewe hivyo ukiona hafanyi...
 
Eti kwenye ule Uzi wangu niliposema hakuna kipaji duniani/hakuna mtu anayezaliwa na uwezo wa kufanya jambo au kitu watu walikuwa wanabisha kisa wamekaririshwa na mabeberu kutoka ulaya.

Oya Nomadix Al-mukheef implicit memory njooni hapa mjionee kisa kinachofhihirisha kuwa hakuna kipaji.

#hakuna kipaji duniani, neno kipaji nai optical illusion.
Sasa hapo hakukuwa na kipaji
 
Ali
Wakuu habari ya weekend,,.
Vipi mmeshatoka jumuiya??,,Na bahasha za pasaka vipi mlisharudisha wote au kunaa wengine bado mnazo ndani?😃,.

Leo buana mama aliniomba tusaidizane kupanga vitu chumbani kwake,. Nimeshangaa kuona eti bado anatunza madaftari yangu ya chekechea😃😆😆,. Kwanza nlivyoona mwandiko ikabidi kwanza nianze kucheka,.

Ni hivi,. Ule mwaka naanza shule kwa kumbukumbu zangu mama alikuwaga kusoma,. Alirudi alinikuta niko chekechea mwaka wa pili ule,. Ile siku amerudi akaanza kuniuliza habari za shule akataka niandike ,. Amenipa daftari na penseli ananitajia maneno ya kuandika nikaanza kuandika pale ananisifia kwelikweli kumbe alikua na jambo lake bwana,. Akasubiri baba amerudi akaanza kumhoji eti " kwanini umeruhusu mtoto anatumia mkono wa kushoto kula na kuandika???"...

Hakuna aliyewaza kama alikua serious akaanza kuniambia hataki anione natumia mkono wa kushoto si nikajua utani labda mwe🥲,. Ilikua akinituma kitu nimpe au kupokea kitu kwa mkono wa kushoto nachapwa,. Akaniambia hadi shuleni hakuna kuandikia mkono wa kushoto,. Basi nkirudi nyumbani anaanza kunifundisha kuandika upya kwa mkono wa kulia na nikisema tu hata nimechoka nachapwa,. Madaftari nikirudi nyumbani anakagua anauliza ulitumia mkono gani kuandika nikisema wa kulia basi ananipa karatasi andika tena kama hivi kwa kutumia mkono wa kulia Asa ole nikosee anajua nimeandika kwa mkono wa kushoto nachapwaa,.basi nitahangaika mpaka nitaweza,. Hadi shule sasa badae nikawa naogopa kuandika, basi nitajikakamua wee niandike tu kwa mkono wa kulia ilimradi tu nikirudi nyumbani nisichapwe,.

Hadi walimu shuleni walikua wanashangaa, mama akiitwa kuambiwa anachokifanya sio sawa alikua anawajibu tu huyu ni mwanangu na atakua vile mimi nataka awe,. Walikua wanagombana na baba karibu kila siku kwamba anakazania kitu ambacho Mungu ameniumba nacho,. mpaka tu mzee alishazoea akiona nimeitwa na mama kusoma au kuandika ye huyo anaondoka zake maana alikua hapendi makelele asa vile navyochapwa na mama akikazania jambo lake,.

Kweli niliteseka ile chekechea mpaka nakuja kumaliza nilishaanza kuzoea sasa kuandikia mkono wa kulia,. La kwanza napo kwa shida shida hivyohivyo mpaka mikono ikawa na nguvu kiasi kwamba hata nikiwa naandika kwa mkono wa kushoto najistukia nahisi mama ananiona😃😅😅,..
But guess what.........,,. Kuanzia darasa la pili na kuendelea hadi leo mkono wangu wa kulia ndio unafanya shughuli zote,. Wa kushoto eti ndio naona umelegea sikuizi 😂😂😂😂

Ni hivyo tu,. Mnavyosoma hii namalizia kupanga vitu hapa nawahadithieni kisa kingine cha mdogo wangu aliyenifatia ana kigugumizi alivyokua anateseka na yeye ,. Ila mama🙌🙌

Endelea link hiyo hapo chini

Huu msemo "Samaki mkunje angali mbichi" uko Real sana
Alikosea sana, mashoto ni watu adimu na wa muhimu, ni vinasaba, mama yako alienda kinyume na Mungu.
 
Hawana akili hao, hawajui genetics. Tatizo lao elimu ndogo, watanzania tumekalia upumbavu usio na maana
Na hii ndio benefit 🤗 😊,. Mikono yote iko active kufanya chochote kile..
Sema sijui walikua wanawaza nini hadi kutuchapa,. Kwamba ni ulemavu au??
 
Kigugumizi ni ulemavu, kwann alikua anawatesa hivyo?

Mtoto wa dada ana kigugumizi kile haswaa, yaan hatari, hadi huwa tunamuonea huruma akiwa anapata shida ktk kuongea, tumejaribu kumlisha mayai mabichi lakini wapii, jaribu za mitishamba lakini wapii, bas tumeacha abaki hivyo.
Mama yake huyo ni mnyanyasaji wawatoto, anatakiwa ashtakiwe.
 
Hawana akili hao, hawajui genetics. Tatizo lao elimu ndogo, watanzania tumekalia upumbavu usio na maana
Kwenye elimu ndogo nakupinga tena kwa HERUFI KUBWA😃😃,. Na wala hawajai kuwa wapumbavu...

Respect is a key 🔑 👌
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom