Huu msemo "Samaki mkunje angali mbichi" uko Real sana

Huu msemo "Samaki mkunje angali mbichi" uko Real sana

Kigugumizi ni ulemavu, kwann alikua anawatesa hivyo?

Mtoto wa dada ana kigugumizi kile haswaa, yaan hatari, hadi huwa tunamuonea huruma akiwa anapata shida ktk kuongea, tumejaribu kumlisha mayai mabichi lakini wapii, jaribu za mitishamba lakini wapii, bas tumeacha abaki hivyo.
Duuh,. Dogo saizi anaongea maneno hayakwami..
Ila ni anaongea taratibu akiwa ameshusha pumzi ,. Akipaza sauti lazima maneno yaishie njian😄😄,. Na hii mbinu bila mama asingeweza
 
Ktk familia yetu, watoto 3 wanaandikia kushoto,

Kunae huyu kaka niliyemfuata, yeye had mguu anatumia wa kushoto, na anacheza ⚽ sana, huwa najiuliza alikua anawezaje kuandika madesa, hasa Advance alisoma PCB, nikiwaza zile notes na namba namba mbna nachoka sana,

Ila wabarikiwe mno, kutumia mambo ktk upande wa kushoto ni kipaji. Lol
Nadhani pengine na mimi ningekuwa hivyo kama bimkubwa asingelisimamia suala langu😃😄,.
 
Basi kuna rafiki yangu yeye upande wake wa kushoto ndo una nguvu kuanzia mguu mpaka mkono, na pia ana kigugumizi. Huyo maza ako angepiga aue ila lijamaa lenyewe si haba lazima angeliogopa lina mwili kama bondia.
Hahahah . Angemuwahi kabla hajakuwa mtu mzima😃😃😃😃😂
Ni uumbaji wa Mungu mkuu huwezi kurekebisha sometimes,. Mama yetu tu sijui hata alikua anawaza nini ila imesaidia sana hasa kwa Dogo.

Naimagine saizi angekua kijana anasimamisha mtu anaanza kushusha vocals maneno yanaishia njiani mwe!😌😌
 
Hahahah . Angemuwahi kabla hajakuwa mtu mzima😃😃😃😃😂
Ni uumbaji wa Mungu mkuu huwezi kurekebisha sometimes,. Mama yetu tu sijui hata alikua anawaza nini ila imesaidia sana hasa kwa Dogo.

Naimagine saizi angekua kijana anasimamisha mtu anaanza kushusha vocals maneno yanaishia njiani mwe!😌😌
Yeye alikua ana amini nini kuhusu mtu anaetumia mkono wa kushoto??
Na kwanini soln yake ilikua kipigo tu??
 
Yeah mzee wangu hapendagi kujichosha aisee,.
Tena kwenye masuala yaso na msingi mtamuona kama anadharau😆😅😅😅
Hiyo ni kawaida kwa wanaume wengi tupo hivyo!, maana uwaze ada,kodi,kula, kuvaa na bill zote unazotakiwa kulipa the uwaze lee anaandikia mkono wakushoto!.. Haha! ni ngumu sana hii, kikubwa si anaandika haiui chochote cha mtu basi.
 
Hiyo ni kawaida kwa wanaume wengi tupo hivyo!, maana uwaze ada,kodi,kula, kuvaa na bill zote unazotakiwa kulipa the uwaze lee anaandikia mkono wakushoto!.. Haha! ni ngumu sana hii, kikubwa si anaandika haiui chochote cha mtu basi.
Dah😃😄😅😂😂,
Sema mnajikutaga busy hadi kwenye mambo yenu wenyewe hilo ndio tatizo
 
Wakuu habari ya weekend,,.
Vipi mmeshatoka jumuiya??,,Na bahasha za pasaka vipi mlisharudisha wote au kunaa wengine bado mnazo ndani?😃,.

Leo buana mama aliniomba tusaidizane kupanga vitu chumbani kwake,. Nimeshangaa kuona eti bado anatunza madaftari yangu ya chekechea😃😆😆,. Kwanza nlivyoona mwandiko ikabidi kwanza nianze kucheka,.

Ni hivi,. Ule mwaka naanza shule kwa kumbukumbu zangu mama alikuwaga kusoma,. Alirudi alinikuta niko chekechea mwaka wa pili ule,. Ile siku amerudi akaanza kuniuliza habari za shule akataka niandike ,. Amenipa daftari na penseli ananitajia maneno ya kuandika nikaanza kuandika pale ananisifia kwelikweli kumbe alikua na jambo lake bwana,. Akasubiri baba amerudi akaanza kumhoji eti " kwanini umeruhusu mtoto anatumia mkono wa kushoto kula na kuandika???"...

Hakuna aliyewaza kama alikua serious akaanza kuniambia hataki anione natumia mkono wa kushoto si nikajua utani labda mwe🥲,. Ilikua akinituma kitu nimpe au kupokea kitu kwa mkono wa kushoto nachapwa,. Akaniambia hadi shuleni hakuna kuandikia mkono wa kushoto,. Basi nkirudi nyumbani anaanza kunifundisha kuandika upya kwa mkono wa kulia na nikisema tu hata nimechoka nachapwa,. Madaftari nikirudi nyumbani anakagua anauliza ulitumia mkono gani kuandika nikisema wa kulia basi ananipa karatasi andika tena kama hivi kwa kutumia mkono wa kulia Asa ole nikosee anajua nimeandika kwa mkono wa kushoto nachapwaa,.basi nitahangaika mpaka nitaweza,. Hadi shule sasa badae nikawa naogopa kuandika, basi nitajikakamua wee niandike tu kwa mkono wa kulia ilimradi tu nikirudi nyumbani nisichapwe,.

Hadi walimu shuleni walikua wanashangaa, mama akiitwa kuambiwa anachokifanya sio sawa alikua anawajibu tu huyu ni mwanangu na atakua vile mimi nataka awe,. Walikua wanagombana na baba karibu kila siku kwamba anakazania kitu ambacho Mungu ameniumba nacho,. mpaka tu mzee alishazoea akiona nimeitwa na mama kusoma au kuandika ye huyo anaondoka zake maana alikua hapendi makelele asa vile navyochapwa na mama akikazania jambo lake,.

Kweli niliteseka ile chekechea mpaka nakuja kumaliza nilishaanza kuzoea sasa kuandikia mkono wa kulia,. La kwanza napo kwa shida shida hivyohivyo mpaka mikono ikawa na nguvu kiasi kwamba hata nikiwa naandika kwa mkono wa kushoto najistukia nahisi mama ananiona😃😅😅,..
But guess what.........,,. Kuanzia darasa la pili na kuendelea hadi leo mkono wangu wa kulia ndio unafanya shughuli zote,. Wa kushoto eti ndio naona umelegea sikuizi 😂😂😂😂

Ni hivyo tu,. Mnavyosoma hii namalizia kupanga vitu hapa nawahadithieni kisa kingine cha mdogo wangu aliyenifatia ana kigugumizi alivyokua anateseka na yeye ,. Ila mama🙌🙌

Endelea link hiyo hapo chini

Huu msemo "Samaki mkunje angali mbichi" uko Real sana
Daaah! Hii issue yako ya kuandika kwa left hand hadi mimi nimepigwa sana jamani, 😂😂😂 umenikumbusha mbali aisee
 
Hampendi kujinunulia nguo why why why??,. Yaani mtu kwa mwaka anaeza akawa amenunua nguo na viatu mara moja kwa mwaka au mbili na hawazi . Kwanini??
Mh! majukumu na labda ukute mwengine kuvaa sio mambo yake!.. wapo wengine kuvaa huwaambii kitu yupo radhi ajinyime kitu fulani fulani ila kuvaa lazima atokee tu!.
So nafikiri hivyo viwili vinachangia yani uchumi na hobby!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom