Huu mpira wa bongo bana

Huu mpira wa bongo bana

Pacome hakuwa offside Bali alikuwa eneo la offside, na ilikufa baada ya mabeki na kipa wa simba kublock shuti la maxi na kutengeneza rebound
Yaani unakuwa sio offside bali unakuwa kwenye eneo la offside? Unapokuwa upo kwenye offside position huruhusiwi ku interfere kwenye move kwani unakuwa automatic offside. Ukifunga kwenye rebound ukiwa unatoka kwenye offside position basi ni offside. Kungekuwepo na VAR huo mjadala usingekuwepo.VAR ingeanzia Pacome alipotoka kwenye offside position na kushiriki kwenye move na kufunga akitoka kwenye offside position.
 
Ukitoka kwenye offside position halafu urudi kushiriki kwenye mpira sio offside?
Mjitahidi hata kuangalia mechi za ulaya zitawafundisha vingi tu kuhusu utafsiri wa sheria. Pacome kabla ya mpira kuchezwa na Maxi n wazi alikuwa katika eneo la kuotea ila alichokifanya ni kuuacha ule mpira kisha akawa anarudi nyuma ( hakushughulika na mpira kwa wakati huo) Maxi alivyopata mpira alipiga shuti kisha ikachezwa na goli kipa. Hapa kwenye rebound inaangaliwa sasa mchezaji anayepiga rebound hiyo yupo katika eneo gani ni onside au ni offside position na kwa wakati huo Pacome tayari alikuwa katika onside position.

Ingekuwa ni offside endapo ingetokea mambo matatu:

1) endapo ule mpira pacome angeenda kuuingilia kuucheza yeye
2) Maxi Zengeli angetoa pasi moja kwa moja kwa Pacome kwa wakati ule
3) mpira uliokuwa ume rebound, ungemkuta Pacome akiwa peke yake katika eneo la kuotea
IMG_20250916_220148.jpg
 
Pacome alikuwa mbele ya Rushine wakati Max anaupiga mpira.Rudia kuangalia.Na sio Refa anaweza kuamua bali ni LAZIMA aamue ni offside sio option.
 
Pacome alikuwa mbele ya Rushine wakati Max anaupiga mpira.Rudia kuangalia.Na sio Refa anaweza kuamua bali ni LAZIMA aamue ni offside sio option.
Karudie kuangalia tena, hi hapa moment ambayo Maxi anapiga shuti ambalo linachezwa na kipa. Angalia alipo Pacome na beki wa Simba, Pacome kazidi wapi?
IMG_20250916_222107.jpg
 
Offside ya wazi hiyo wala haina mbambamba. Hawa marefa wapumbavu wapumbavu huwa wanawatoa wapi?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Rudia kuangalia. AU hujui kwamba obstruction kwenye mpira ni foul.Pacome aliingilia mpira kwa kum obstruct Rushine.
Nimetiza sijaona, Halafu unajua nini maana ya Obstruction?
 
Nimetiza sijaona, Halafu unajua nini maana ya Obstruction?
Kumzuia mchezaji wa timu pinzani asifikie au kucheza mpira kwa kusimama mbele yake bila kuucheza mpira.. Unaangalia kwa mapenzi . Obstruction ipo wazi sana.
 
Rudia kuangalia. AU hujui kwamba obstruction kwenye mpira ni foul.Pacome aliingilia mpira kwa kum obstruct Rushine.
Wewe jamaa unaruka ruka tu, ulisema wakati Maxi anapiga shuti ambalo linachezwa na kipa, Pacome alikuwa kazidi. Umewekewa picha wakati Maxi anapiga shuti uone position ya Pacome ilipo. Saivi unakuja na ngonjera ya obstruction. Hiyo obstruction mwenzetu umeiona wapi?
 
Kumzuia mchezaji wa timu pinzani asifikie au kucheza mpira kwa kusimama mbele yake bila kuucheza mpira.. Unaangalia kwa mapenzi . Obstruction ipo wazi sana.
Kwanza unaelewa kama offside inaanza kuangaliwa kwenye moment ipi? Ni wakati Maxi anapiga mpira ile shuti. Sasa wewe hoja unayoleta kwasasa sio tena offside ni hoja mpya ambayo ni faulo. Kama ni ishu ya offside inaishia katika muda ambao Maxi anapiga shuti na ni wazi Pacome kaonekana yupo katika eneo sahihi hakuotea.
IMG_20250916_222107.jpg
 
Mbumbumbu kesho nina tuishen kuhusu mambo ya ofisa-idi hii ni kwawale mbumbumbu wanajizima data maana kuna mbumbumbu wengine kuna muda network zinakamata.

Darasa litakua kibarazani kwa rage pale kariakoo
 
hukuona pacome aliingilia mchezo akiwa offside na kumblock beki wa simba kufanya tackling kwa max?
Rudia tena kuangalia, ni wakati gani Pacome alikutana na huyo beki simba? Si wakati Max ameshauchukia mpira? Sasa uanze na tukio la Max kuanza kuchukua mpira it means tukio la offside lishakufa. Turudi kwenye clip
 
Yaani unakuwa sio offside bali unakuwa kwenye eneo la offside? Unapokuwa upo kwenye offside position huruhusiwi ku interfere kwenye move kwani unakuwa automatic offside. Ukifunga kwenye rebound ukiwa unatoka kwenye offside position basi ni offside. Kungekuwepo na VAR huo mjadala usingekuwepo.VAR ingeanzia Pacome alipotoka kwenye offside position na kushiriki kwenye move na kufunga akitoka kwenye offside position.
Mkuu waamuzi wanaambiwa wasiamue kitu kwa kubahatisha, wakati Dube anapiga mpira Pacome alikuwa eneo la kuotea, hapa Pacome angegusa mpira tu mwamuzi angepuliza firimbi kuashiria na offside! Lakin unaona Pacome akugusa mpira wala kuingilia mchezo zaidi unamuona Max anauchukua mpira, kitendo cha Max kugusa kwa touch ya kwanza tu tayari mpaka hapo offside ya Pacome imeshakufa, Max anasogea kwa touch ya 2 ndipo Pacome anaonekana kugusa na beki za Simba, hapa sasa labda tuseme ni faulo na sio Offside tena. Mwisho Max anashuti na Camara anacheza lakini Max akiwa anashuti unamuona Pacome alipokuwa? Alikuwa offside? So offside inaangaliwa pia wakati mtoa pasi anatoa wewe unaetafsirika ulikuwa offside ulikuwa wapi?
 
Ukikubali kwamba aligusana na beki za Simba akiwa ametoka kwenye offside position na kufanya obstruction kwa Rushine ndio kuingilia mpira huko hivyo goli alilofunga sio halali.
 
Back
Top Bottom