Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Genius Mzee

Member
Jul 29, 2021
50
222
Kuna mjadala unaendelea space pale twitter aisee kama haya maazimio ya kususia bidhaa na huduma yatafanikiwa hakika itakuwa hatari kwa uchumi.

Ushauri, Serikali wakutane na wapinzani haraka maana hata mishahara ya mapolisi inaweza kukosa huko mbeleni.

Ni ushauri tu mnaweza kuufanyia kazi au kuupuza ila kama hatua hizi zitafanikiwa hata kwa 25% makusanyo yataporomoka sana.

View attachment 1877729
 
Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato.

Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki.

Wanasema kuwa, jamii ya Watanzania wakipunguza matumizi ya bidhaa na huduma kama vile unywaji wa Bia, kupunguza matumizi ya sukari, maji ya kunywa, kupunguza miamala isiyo ya lazima na vyakula katika hoteli zilizosajiliwa.

Wanaamini kuwa kupunguza huko matumizi ya huduma na bidhaa itasababisha serikali kukosa kiasi kikubwa cha mapato.

Na kukosa huko mapato itasababisha serikali ishindwe kujiendesha kwa sababu mapato yamepungua. Na bila shaka, kutafuta namna ya kukaa na wadau na kuzungumza nao ili kuweza kutatua yaliyomo.

Wanaamini kuwa, njia hii ya kususia bidhaa na huduma 'Boycotting' itakuwa na ufanisi kwa sababu hakuna polisi watakaokuja kuwalazimisha watu watumie.

Wanaona kuwa njia hii ni ya amani na hivyo itawalazimisha serikali kurudi katika Misingi ya Utawala bora na kuleta uchocheo wa Katiba mpya.

Je, CHADEMA watafanikiwa kwa njia hii?
 
Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato.

Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki.
Huu ni uzushi wako mwenyewe, acha kudanganya watu.

Chadema wanaweza kuwa na kasoro kadhaa lakini sio kukosa akili kiasi hiki kwamba wadhani wakisusia bidhaa itakuwa na impact kwenye uchumi kwa sababu hata CCM wakisusia hakuwezi kuwa na impact.

Kwa hiyo hii kitu umejitungia kichwani halafu unaileta hapa ukisingizia Chadema
 
Mkuu,

Tafadhali fuatilia mjadala huo Twitter. Sina haja ya kuongopa.

Fuatilia hapa:
 
Kwasabu chadema wapo wachache hawatofanikiwa ,labda wananchi kwa ujumla bila kujali vyama ndio hiyo kitu itawezekana kumbuka walisusia voda mpaka sasa inadunda
Voda unajua hali yake lakini kwa miaka 5 iliyopita.

Unajua mwaka Jana wametengeneza hasara ya 60 billions?

Kilichopi ni mpesa sio voda, voda ilishakufa kitambo sana .

Na mpesa wakicheza haya matozo inakufa nayo.
 
Back
Top Bottom