Francis Kairu: Kwa Afrika bado ni kibarua kigumu kupambana na utoroshwaji wa fedha haramu

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1697554632247.jpeg

Je, umekua na shauku ya kutaka kujua Fedha haramu ni zipi na kwa nini zinataroshwa?

Karibu ujiunge nasi katika Mjadala na Wataalamu wa Uchumi utakaofanyika Alhamisi ya Oktoba 19, 2023 kuanzia Saa 12 Jioni hadi Saa 2 Usiku kupitia Xspaces ya JamiiForums

Katika Mjadala huu tutaangazia nini Maana ya Utoroshaji, Fedha haramu ni zipi, kwanini zinatoroshwa na kwa njia zipi, na zaidi ya yote nini athari za Utoroshaji huu na Athari zake kwa Nchi hasa kwenye Utoaji wa Huduma za Kijamii

Pia unaweza kutoa maoni na kuuliza maswali yako kupitia uzi huu yatasomwa siku ya mjadala.

Karibu

FRANCIS KAIRU, MSHAURI WA KODI
Ni usafirishaji wa pesa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine kwa njia isiyo halali, wakati mwingine hata pesa husika ilivyopatikana inaweza isiwe halali.

Ni ngumu kufanya biashara katika Nchi moja bila kuhusisha Nchi nyingine, ndivyo ilivyo katika masuala ya fedha, mifumo inayotumika kutoa pesa kutoka Nchi moja kwenda nyingine inaweza kuwa si halali

Baadhi ya njia hizo zinaweza kuwa Benki au kwa Njia ya Simu, hivyo utoroshwaji wa fedha unahusisha kutoa fedha toka taifa moja kwenda lingine katika njia zisizo halali.

Suala hili linatesa sana nchi za Afrika na duniani kote. Nchi nyingi zilizoendelea hupokea sana pesa kutoka nchi zisizo endelea sana. Mfano, ukienda UAE unaweza kupata dhahabu nyingi, unaweza kujiuliza zimetoka wapi? Zimetoka Afrika.

Wale ambao ni watoroshaji wa fedha mara nyingi hutumia benki, stakabadhi za biashara n.k, wanatumia njia zinazoonekana ni halali lakini kumbe wanatumia biashara ili kutorosha hizo pesa.

Makampuni yanayopatikana hapa Afrika wakati mwingine wanatumia utaratibu wa udanganyifu wa kutoa taarifa ya kodi ndogo ili wakikadiriwa waonekane hawapati sana.

Kwa Afrika bado ni kibarua kigumu kupambana na utoroshwaji wa fedha haramu. Nchi kadhaa zimejaribu, ya kwanza ni Afrika Kusini wameimarisha sana mifumo yao na maafisa wa Serikali wamebobea sana kwa kupata mafunzo ya hali ya juu, pia mikataba baina ya Afrika Kusini na nchi zingine katika utozaji wa kodi ipo mingi hivyo ni rahisi kufuatilia watu na makampuni yanayofanya biashara hapo au nje ya hapo, wanaweza kuwafikia kirahisi.

Nchi kama Ghana wamefanya hivyo pia, wameimarisha sheria zao na taasisi za serikali zinazofanya jukumu hili zinajihidi.

Teknolojia imechangia kurahisisha biashara lakini imerahisisha pia kukwepa kodi, mtu anaweza kufanya biashara na asijulikane kama anafanya biashara.

Nchi kama Marekani fanya chochote unachoweza ila hakikisha unalipa kodi, kwetu ni tofauti.

NORAH KAWICHE, MTAALAM WA KODI
Kwa Tanzania tunajaribu sana kupambana na hili suala la utoroshaji wa fedha haramu, mfano kuna sheria ya Anti-Money Laundering Act inayosaidia sana kuzuia utoroshwaji wa fedha.

Tupunguze kinga kwa baadhi ya viongozi ili tushughulike na haya mambo kikamilifu maana kwa upande wa sheria tupo vizuri. Shida ni utekelezaji wa hizi sheria, tukitekeleza vizuri tuna uwezo wa kuzuia utoroshwaji wa fedha, pia tuongeze ushirikiano na nchi zingine ili kuzuia tatizo hili.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa hakuna nchi itakupa taarifa bila kuwa na mkataba nayo, hivyo tujiunge na nchi tofauti ili tupate taarifa.

Sababu za utoroshaji pesa zipo nyingi ikiwemo upatikanaji wa fedha haramu, wanaogopa kuzitumia hapa kwa kuwa watakamatwa (hazijapatikana kwa njia halali) hivyo wanazitoa ili baadae zirudi.

Pia, kwa makampuni mengi huzitoa nje ili kukwepa kodi, au wanatoa fedha sehemu moja kwenda nyingine ili kwenda kuwekeza.

Wengine huangalia exchange rate, wanapeleka sehemu yenye exchange kubwa ili pesa iongezeke.

Fedha haramu ni ile iliyopatikana kwa njia zisizo halali, au pesa halali lakini inahamishwa nchini kinyume cha sheria halali za nchi.

Mfano, mtu haruhusiwi kusafiri na bulk ya fedha zaidi ya milioni 10. Ukikamatwa na mabilioni kwenye mabegi hiyo ni fedha haramu hata kama umeipata kihalali kwa sababu tu ilikuwa inasafirishwa kinyume na sheria za nchi.

Pesa halali inayoenda kutumika kwa mambo yaliyo kinyume cha taratibu hiyo nayo ni fedha haramu.

Madhara ya utoroshaji wa pesa ni kupunguza mapato ya nchi maana huhusisha ukwepaji wa kodi.

Kwa Tanzania pale Bandarini unaweza kujua mzigo unaoingia una thamani gani na tuna Watu wa TRA wanaweza kujua unachoingiza kina thamani gani.

Tatizo kubwa ni Rushwa na sio Sheria, ukienda Bandarini ukatoa Rushwa manake unakuwa umekwepa fedha iliyopaswa kulipwa.

DKT. BALOZI MORWA, MTAALAM WA UCHUMI
Tufahamu kuwa utoroshaji wa Fedha unahusu Fedha nyingi na unagusa watu ambao ni wataalamu.

Athari za Utoroshaji Fedha unaathiri sana masuala ya uchumi ikiwemo viwango vya kubadili Fedha na kuyumbisha Serikali.

Baadhi ya Sheria zetu zinatoa msamaha kwa Wawekezaji wakiwemo wachimba Madini.

Kampuni nyingi zinaagiza mafuta kutoka nje na hazilipi Kodi na wanadanganya wameagiza kwa fedha nyingi.

Kutokana kupata msamaha wa Kodi huu Makampuni mengi yanadanganya kupata hasara kila mwaka kwasababu wanaongeza gharama za uagizaji bidhaa nje.

Hawa watu ni wataalamu na bahati mbaya wamepewa uchochoro huo na Serikali yenyewe.
 
Back
Top Bottom