CHADEMA wamepoteza dira kuwaambia Watanzania kususia huduma na bidhaa ili Serikali ikose mapato

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,892
32,308
Wanaukumbi.

CHADEMA tuelezeni hizo Tozo Mpya zinaingizia serikali kiasi gani cha Pesa Kisha mtueleze matumizi ya serikali kama mnavyodai zinaenda kununua mabomu na kulipa polisi mishahara.

Serikali inasema hizo Tozo zitakwenda Tamisemi kujenga madarasa na zahanati zingine zinaenda Taruru kujenda barabara vijijini.

Heche na Lema wanawajaza watu ujinga huko Space, mnawambia watu et wafanye boycott Campaign hii mara nyingi inatumika kwa bidhaa au huduma mfano kampeni za kususia Coca Cola nunua Pepsi au kususia vifurushi vya Vodacom nunua Tigo. Lengo ni kunyoosha kampuni kama haisimamii haki. Unasusia serikali ili umuumize nani kodi zinamnufaisha nani?

Ukisusia kununua Petrol utauza gari au kulipaki nyumbani ukisusia kununua vifurushi tuanze kuandikiana barua au tupeleke salamu kwa mkono?

Ukisusia maji, vinywaji, vyakula utaishi au utakufa.

Miradi ya maendeleo kama Barabara, Huduma za Afya, Shule, zinamnufaisha nani?
 
Mkuu usiwe na wasi wasi maana hata hili pia litapita kama yalivyopita mengine. Uzuri ni kwamba 95% ya watanzania wameshaachana na siasa za kilaghai za Chadema ndo maana kila wanalopanga linabuma.

Kama watu waliweza kuchangia chama chao katika uchaguzi mkuu na michango ikaliwa na mwenyekiti akishirikiana na genge lake, watashindwaje kuchangia tozo ambazo ni kwa ajili ya kuwajengea barabara zao, hospital zao, shule zao nk.

Michango ya uchaguzi imetafunwa vibaya sana na wajanja na hadi leo hakuna mrejesho wa matumizi yake

2528007_20200919_173148.jpg
 
Simba wa nyika bhana. Naona hana mawindo. Aendelee kula kilaji na totoz yake iliyokuwa kiti maalumu. Achunge tu utelezi.
 
Kususia huduma na bidhaa ili serikali ikose mapato na kushindwa kujiendesha ni wazi wanazidi kujiweka mbali na wananchi kwa sababu harakati zinalenga kumuumiza mwananchi wa kawaida sio Rais au wabunge.
 
20210824_160649.jpg

Tatizo sio tozo wala Kodi ila tatizo ni matumizi pesa nyingi ya mapato ya serikali haendi kwenye maendeleo kama wanavyohubiri
 
Kelele za nini nyie si mnunue tu.
Sisi tunasusia kadri itavyowezekana , nyie wenye kibali na nchi hii na mnajiona ndio wenye haki peke yenu..
 
Kususia huduma na bidhaa ili serikali ikose mapato na kushindwa kujiendesha ni wazi wanazidi kujiweka mbali na wananchi kwa sababu harakati zinalenga kumuumiza mwananchi wa kawaida sio Rais au wabunge.
Si ndio vizuri kwa CCM kuvuna kura nyingi kwa wanachi kwa TOZO na makodi.
Yaani MaCCM hamueleweki mnataka nini,
Ni Kama kuku aliekatwa kichwa.
 
Kususia huduma na bidhaa ili serikali ikose mapato na kushindwa kujiendesha ni wazi wanazidi kujiweka mbali na wananchi kwa sababu harakati zinalenga kumuumiza mwananchi wa kawaida sio Rais au wabunge.
Tozo hazimuumizi mwananchi wa kawaida ?
 
Wanaukumbi.

CHADEMA tuelezeni hizo Tozo Mpya zinaingizia serikali kiasi gani cha Pesa Kisha mtueleze matumizi ya serikali kama mnavyodai zinaenda kununua mabomu na kulipa polisi mishahara.

Serikali inasema hizo Tozo zitakwenda Tamisemi kujenga madarasa na zahanati zingine zinaenda Taruru kujenda barabara vijijini.

Heche na Lema wanawajaza watu ujinga huko Space, mnawambia watu et wafanye boycott Campaign hii mara nyingi inatumika kwa bidhaa au huduma mfano kampeni za kususia Coca Cola nunua Pepsi au kususia vifurushi vya Vodacom nunua Tigo. Lengo ni kunyoosha kampuni kama haisimamii haki. Unasusia serikali ili umuumize nani kodi zinamnufaisha nani?

Ukisusia kununua Petrol utauza gari au kulipaki nyumbani ukisusia kununua vifurushi tuanze kuandikiana barua au tupeleke salamu kwa mkono?

Ukisusia maji, vinywaji, vyakula utaishi au utakufa.

Miradi ya maendeleo kama Barabara, Huduma za Afya, Shule, zinamnufaisha nani?
Hivi kabla ya hizi Tozo Madarasa, zahanati/vituo vya afya na Barabara zilikuwa hazijengwi?
Kama vilikuwa vinajengwa pesa ilikuwa inatoka wapi?
Mbona mnatumia hoja nyepesi sana kuhalalisha unyonyaji na upigaji kwa wananchi wenu
 
Kuna namna mbali mbali za kupambana na tawala dhalimu duniani mojawapo ikiwa ni hiyo ya kukwepa kulipa kodi. Wabunge, Mawaziri na Rais hawalipi kodi hivyo hakuna ubaya wowote ule wa Watanzania nao kukwepa huu UTITIRI wa kodi uliokithiri.
Wanaukumbi.

CHADEMA tuelezeni hizo Tozo Mpya zinaingizia serikali kiasi gani cha Pesa Kisha mtueleze matumizi ya serikali kama mnavyodai zinaenda kununua mabomu na kulipa polisi mishahara.

Serikali inasema hizo Tozo zitakwenda Tamisemi kujenga madarasa na zahanati zingine zinaenda Taruru kujenda barabara vijijini.

Heche na Lema wanawajaza watu ujinga huko Space, mnawambia watu et wafanye boycott Campaign hii mara nyingi inatumika kwa bidhaa au huduma mfano kampeni za kususia Coca Cola nunua Pepsi au kususia vifurushi vya Vodacom nunua Tigo. Lengo ni kunyoosha kampuni kama haisimamii haki. Unasusia serikali ili umuumize nani kodi zinamnufaisha nani?

Ukisusia kununua Petrol utauza gari au kulipaki nyumbani ukisusia kununua vifurushi tuanze kuandikiana barua au tupeleke salamu kwa mkono?

Ukisusia maji, vinywaji, vyakula utaishi au utakufa.

Miradi ya maendeleo kama Barabara, Huduma za Afya, Shule, zinamnufaisha nani?
 
Hawa wanasiasa wa CHADEMA wanaoshauri wasile hotelini wasinunue maji wanamiliki Hotels tunaomba waulizeni wameshafunga Hotel zao kama njia mojawapo ya kususa?

Kama zipo wazi kwa sasa wanauza hewa

Bavicha bana.
Kuna tamko rasmi la CHADEMA kuhusu kususa?
 
Back
Top Bottom