Kwanini bei elekezi ya Sukari haifuatwi?

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
386
765
Serikali ilitangaza bei elekezi ya sukari kwa nchi nzima lakini mpaka sasa bei hiyo haifuatwi na bei ya sukari imebaki vile vile kabla ya matangazo ya bei elekezi.

Kwa nini?
 
Serikali ilitangaza bei elekezi ya sukari kwa nchi nzima lakini mpaka sasa bei hiyo haifuatwi na bei ya sukari imebaki vile vile kabla ya matangazo ya bei elekezi. Kwa nini?
Niliwaambia humu kupitia makala/yangu kwamba sukari haishukagi bei tangu Julai 2001 (miaka 23) hata ikiagizwa kwa wingi kiasi gani, bei elekezi ni porojo za kisiasa.
 
Haya mambo ya Divide and Rule watu tunatafutana Uchawi wenyewe kwa wenyewe badala ya kuwajibisha Mamlaka Husika....

Hio Serikali haikujua kwamba Supply ni ndogo kipindi hiki ? , Hii ni mara ya Kwanza ? Haya mambo ya Kupeana Bei elekezi vitu vikipungua na Vikiwa vingi kwamba hatupangiani Bei ni Utawala kukosa suluhisho na kuendeleza Maigizo
 
Serikali imefanya nini kusaidiana na wafanya biashara kuongeza upatikanaji wa sukari kwa bei nafuu mpaka iwapangie bei?

Ule waraka ulikaa kisiasa kupoza vuguvugu la Maandamano.
 
Kwa sababu ni siasa tu, sio rahisi kihivyo kupanga bei kwenye uchumi wa soko huria.
 
Serikali ilitangaza bei elekezi ya sukari kwa nchi nzima lakini mpaka sasa bei hiyo haifuatwi na bei ya sukari imebaki vile vile kabla ya matangazo ya bei elekezi.

Kwa nini?
Kwa kuwa hii biashara inaratibiwa na chikundi cha watu yenye nasaba, badala ya Biashara kuwa ya ushindani, hivyo hivyo chikundi ndio kinacho panga bei na sio nguvu ya solo.Chiongozi wetu wa juu wanasema wanafanya sindiketi.
 
Ni kwasabb aliyepanga bei elekezi anawaogopa watu 4 tu nchi hii. Kwahiyo alipanga bei kibabe.

Angelikiwa anawaogopa wananchi wenye nchi angewashirikisha ktk kupanga bei elekezi na ingefuatwa.
 
Back
Top Bottom