Humphrey Polepole nakusubiri uongelee suala la Zanzibar kupata mkopo kupita Serikali ya Muungano

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,093
144,558
Bwana Humphrey Polepole, sasa tunataka kusikia maoni yako kuhusu huu ukopaji wa mikopo kutoka nje huku Zanzibar ikishirikishwa na kupata mgao.

Pamoja na mambo mengine,ulilaumu na kukosoa mawaziri kutosema lolote kuhusu kauli ya Mama kula kwa urefu wa kamba yake, na hapo hapo kumpiga kijembe Mama kwa kauli hiyo. Sasa tunataka kusikia kuhusu hili la Zanzibar kupata mkopo kupitia serikali ya Muungano.

Tunakusubiri ingawa na wewe ulishapoteza credibility.
 
Hiyo kauli ya mbunge Polepole unayoisubiri ambayo labda ataitolea Twitter au Facebook haitakuwa na cha maana wala impact yoyote.
 
Ukiwa na Smarthone yako unaweza ukadhan Polepole ni moja ya Majabali ya Siasa Nchini

Ukizima Simu ukaingia Tandale ukauliza Pole pole ni nani watu wanawez wasielewe unamzungumzia nani na wale wasiomjua ndio hasa Wapiga kura

Uzuri wa Tanganyika wanaofatilia Siasa hawapigi kura na wasiofuatilia ndio Wapiga kura wa kudumu

Yule Zeruzeru aliogombea 'Undugai' aliongea point moja muhimu sana kwangu…Wenye nafasi ya kuzungumza Bongo hawana cha kuzungumza na wasio na nafasi ya kuzungumza ndio wenye cha kuzungumza

Kidumu Chama cha Mapinduzi
 
Sasa kama unaona alishapoteza credibility akiongea ndio utapata faida gani.
Ama unamkubali kimyakimya lakini unaogopa madongo ya wahuni humundani.

Tukubali tu polepole ana hoja za msingi kwenye machapisho yake.

Hata ndugai nae alikuwa na hoja ya msingi kwenye mikopo.

Jaribu kuwa huru.
 
Kuna maoni mengine huwa hayasemwi hadharani hakuna mwanaccm anayeridhika na huo mkopo labda wale wanaofaidi utawala wa rais
 
Ukiwa na Smarthone yako unaweza ukadhan Polepole ni moja ya Majabali ya Siasa Nchini

Ukizima Simu ukaingia Tandale ukauliza Pole pole ni nani watu wanawez wasielewe unamzungumzia nani na wale wasiomjua ndio hasa Wapiga kura

Uzuri wa Tanganyika wanaofatilia Siasa hawapigi kura na wasiofuatilia ndio Wapiga kura wa kudumu

Yule Zeruzeru aliogombea 'Undugai' aliongea point moja muhimu sana kwangu…Wenye nafasi ya kuzungumza Bongo hawana cha kuzungumza na wasio na nafasi ya kuzungumza ndio wenye cha kuzungumza

Kidumu Chama cha Mapinduzi
Huu ujinga wenu ndio unaendekeza miungu watu, ndio maana siku hizi wanaaanza kauli za "wenye chama chao"

Polepole, wewe, Makamba na wengine wote ni sawa, muache ujuha wenu wa kuvimbiwa madaraka na kuanza kuwatenga wengine.
 
Binadamu ni sawa kinadharia ila si sawa kiuhalisia.
Huu ujinga wenu ndio unaendekeza miungu watu, ndio maana siku hizi wanaaanza kauli za "wenye chama chao"

Polepole, wewe, Makamba na wengine wote ni sawa, muache ujuha wenu wa kuvimbiwa madaraka na kuanza kuwatenga wengine.
 
Bwana Humphrey Polepole, sasa tunataka kusikia maoni yako kuhusu huu ukopaji wa mikopo kutoka nje huku Zanzibar ikishirikishwa na kupata mgao.

Pamoja na mambo mengine,ulilaumu na kukosoa mawaziri kutosema lolote kuhusu kauli ya Mama kula kwa urefu wa kamba yake, na hapo hapo kumpiga kijembe Mama kwa kauli hiyo. Sasa tunataka kusikia kuhusu hili la Zanzibar kupata mkopo kupitia serikali ya Muungano.

Tunakusubiri ingawa na wewe ulishapoteza credibility.
Mbona mna roho mbaya nyie. Kamkopo kadogo tu , tubilioni mia mbili kwa ajili ya maji kamefunguliwa nyuzi Mia. Acheni hizo . Mbona nyie mnaikalia nchi yetu kumabavu? Tuachieni basi nchi yetu.
 
Back
Top Bottom