Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

watanzania tujiandae, tutakufa sana kama mahakama zetu zipo kienyeji kama hivyo, na kama ni hivyo ile tume iliyoundwa kuchunguza mauaji wote wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ya kuidanganya serhgkali. Du hi ndio bongo watu wanakufa wenyewe
 
Nitakuwa sina shukrani kama nitakosa kuwashukuru wote waliotuhabarisha hii habari tokea hasubu mpaka kuhitimisha "invisible" Ahsanteni sana Mungu awabariki kwani mmefanya kazi ya kujituma hadi dakika ya mwisho.

Haya yote tumwachie Mungu kwani ndo anayejua pengine anataka watu waelewe kwa kupitia fulani pengine kuna maajabu yatatokea kupitia hii kesi. Si mliona kwa Ditto!! pamoja na kulindwa na Mkulu lakini Mungu akamchukua haraka. Ahsanteni - Roho za marehemu zipumzike kwa amani.
 
Tanzania ehh nchi yangu ehhh, asiachiwe mchezo nani ataweza kuwapiga mabomu ya machezi wapinzani wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2010
 
Watanzania bana, sasa mnadhani wapi haki itapatikana?

Dah, Mahakama Kuu haiwezi kufanya kosa, mashtaka yalikuwa dhaifu na mtuhumiwa sasa anarajea mtaani kukabiliana na vyombo vya habari vilivyomchafua jina... Kaazi kwelikweli

Lakini si aliyeua ni Koplo Saad ambaye hayupo? Vyombo vya habari na wamiliki wake wakae mkao wa kuanza kulumbana na Zombe kwa kudaiwa fidia

Mkuu, vyombo vya habari vilikuwa vinaripoti mashtaka. Hii ni tofauti na defamation. Sasa mngetaka kesi zisiripotiwe kwa kulinda majina ya watu?

je anaweza kukamatwa tena ? na kushitakiwa upya ?
labda ije evidence mpya. Ama sivyo wanasema inakuwa double jeapardy.

mahakama inafanya kazi kutokana na ushahidi unaoletwa mbele yake na wala si kwa kusoma magazeti na hisia!

Hivi mlitaka iweje? Kama Zombe hakuua na ushahidi hautoshelezi, mnataka ahukumiwe kwa sheria ipi? Mashtaka ni dhaifu wakuu!

Angalia hata nilichogusia kuhusiana na kesi ya kina Mramba... Kesi hiyo pia inaelekea ni dhaifu tu!

Kesi ya kina Mramba: Serikali itashindwa!

Inaweza ikawa inawauma wengi lakini sheria ni msumeno...

Tungeomba kupata nakala ya hiyo hukumu waheshimiwa. Tatizo nionalo ni kwamba watu wanalalamika kwa sababu kesi/evidence inajengwa na wale wale wanaojilinda. Yani kwa sasa ivi huwezi ona tofauti ya prosecution na serikali. Hili linatokana na kina Change waliokuwa AJ kuwa karibu mno na serikali. Wewe unadhani leo serikali ikishinda hii kesi, itakuwa ina-set precedent gani? Si wanaofuata nao lazima wale ndani. Baada ya kuzungumza na practitioner mbalimbali, nadhani kwa tz, sheria ni kama maji ya matopo. Haiko wazi kabisa. Na operation ya mahakama ni poor sana. There is a lot that needs to change. Watu wengi wanadhani sheria inaleta haki peke yake. Sheria inasaidia pia kuleta maendeleo. Kwa mfano, inalinda property rights, kiasi kwamba mimi naweza leo kukuazima pesa nikijua zitarudi kisheria. Hivyo, sheria inasaidia kuwepo kwa imani, na hivyo kufanya watu wawe involved katika biashara, nk.
 
Haki inadaiwa kivyoyote wewe, hata kumuua jaji Masati....kumbuka watu wamepoteza ndugu zao kwa ulafi wa Zombe, na ni dhahiri bado tunaletewa za kuleta. Acha woga, mafisadi hawana msalie mtume.
Tatizo sio woga mazee,bali nakushangaa tu jinsi unavyowahsauri watu walioko Dar waingie mtaani wafnaye vurugu kudai haki kisha wapigwe virungu na polisi(kama siyo risasi) wakamatwe na kufunguliwa mashtaka kisha wahukumiwe ilhali wewe uko mikoani/majuu unakula tu BATA...Haiwezekani aisee
 
Ukweli huo ulionekana hata wakati wa utoaji ushahidi,mashahidi karibu wote ushahidi wao ulikuwa ni wa hisia zaidi kuliko ukweli husika,Binafsi niliamini Zombe angeachiwa kutokana na ushahidi dhaifu uliotolewa.

Tufikie mahala tuwe tunaangalia mwenendo wa kesi na si kushangaa hukumu,kulikuwa na mapungufu mengi mno kwa mashahidi wa mashitaka wakitoa ushahidi dhaifu mno uliotanguliwa na jazba bila kuangalia uzito wa kesi ya mauaji.Binafsi ningeshangaa kama JUDGE angeweza kutoa hukumu kwa kuangalia mazingira ya nje ya mwenendo wa kesi na si ushahidi na mwenendo mzima wa kesi...

Pia hili ni fundisho kwa vyombo vyetu vya habari kwa namna ambavyo vinaweza kupotosha sheria,naamini kama JUDGE angekuwa dhaifu angeweza toa hukumu ili kufurahisha jamii na si kwa kuangalia mwenendo wa kesi na ushahidi,Kwa kweli JUDGE amekuwa objective.nilifuatilia kwa makini kesi ya Zombe na kwa kiasi kikubwa ushahidi kwenye kesi ya kuua ulikuwa ni dhaifu mno,kwa kiasi kikubwa kesi ilikuwa ni ya kisiasa zaidi.

Hi ni changamoto kwa wanahabari kuipitia hukumu ya JUDGE na kuangalia namna alivyofikia hitimisho na madhaifu atayoonyesha kwenye marejeo ya ushahidi na mwenendo mzima wa kesi kwa ajili ya kuinua upeo wetu wanahabari kwenye habari zinazohusu mambo mazito kama haya ya mauaji ya kukusudiwa yatendwayo na baadhi ya maaskari wetu.

mkuu kuna mahali unamiss kitu, Hivi Bageni na wenzake kusema waliua watu Sinza posta na wakamwaga damu ya bata, wakatoboa matundu kwa bisbisi nk hiyo ni sawa? waonyeshe basi watu waliowaua Sinza! Waseme sasa wamewapeleka wapi wale vijana wa mahenge ebo!
 
Sheria ndio imemtoa, na sheria hiyo hiyo ndio itamuwezesha kurudi tena kwenye government na kutundikwa Cheo kingine.
 
maelezo ya Bageni yalikuwa haya

Mbele ya Jaji Salum Massatti anayeisikiliza kesi hiyo, Bageni alidai kuwa Zombe alimweleza kuwa walisoma na Jaji Kipenka darasa moja katika Shule ya Sekondari Songea na kwamba ameahidi kuwasaidia katika suala la mauaji hayo.

"Mshitakiwa wa kwanza aliniambia kuwa Jaji Kipenka ni "classmate" wake... walisoma naye darasa moja Songea Boys na kwamba wamewasiliana na amemwambia kuwa tupeleke taarifa iliyorekebishwa ili awasaidie vijana wetu," alidai Bageni wakati akijibu maswali kutoka kwa wakili wa serikali, Angaza Mwipopo.

Bageni alidai kutokana na ushauri huo wa Zombe waliamua kuibadili taarifa waliyoipeleka kwenye tume hiyo, tofauti na taarifa waliyoiandaa ambayo ilipelekwa katika kitengo cha uhalifu, maarufu kama 99.
 
Sheria imechukua mkondo wake!

Mh. Pinda alisema kama kuna ushahidi hakuna haja ya kuwapeleka mahakamani wananchi wamalizie hukuhuko mkasema oooh Waziri mkuu haheshimu utawala wa sheria sasa mmeziona sheria zinavyofanya kazi yake.

Mtihani kwa serikali, Zombe yuko nje tuone kama watakata rufaa!
 
Ni kweli inawezekana kwamba Zombe hana hatia. Lakini mambo kama haya ambapo jamii inaona wazi kabisa kwamba kuna uwalakini mkubwa halafu Mahakama inapindisha hukumu au inazingatia ushahidi ambao hauna uzito ili kufikia malengo wanayoyataka then hii ndio inawafanya watu kukosa imani na vyombo vya serikali.

Kwa hali hii wananchi wengi wataendelea kuvunjika moyo, kukata tamaa na kuendelea kukerwa na Serikali yao yote kwa ujumla.

Kila chombo cha serikali kwa sasa kinanyooshewa kidole kwa kuwa Dhaifu. Bunge kwa kushindwa kuwatetea wananchi pamoja na wabunge kujilimbikizia mali na kuonekana kutowajali wananchi, Serikali kwa kuwa mbali na wananchi na kufungia macho maovu makubwa kwenye jamii na Mahakama kuwa sehemu ya kuhalalisha uovu.

Inakatisha tamaa zaidi kuona kwamba mambo makubwa kabisa na yenye mustakabali wa kitaifa huchukuliwa kirahisi rahisi au hupindishwa wakati mambo madogo hukemewa na kuchukuliwa hatua kubwa ya kuyakomesha kabisa. Kwa hali hii itakua ni vigumu sana kukomesha Mob Justice (kuchukua sheria mikononi).

Hukumu ya Zombe is a big scandal, shame and mockery of the Justice system in our country but a tainted corruption and grave recklessness, lack of profesionalism, ignorance of the Attorney General Office, investigation and Police Department.
 
well said!
 
hi kweli haitakuwa na impact kwenye chaguzi zijazo kweli, na wanamahenge watalichukuliaje ? Nawadhani leo usingizi utatoweka kule kwa wale marehemu, maana mategemeo ya walio wengi hayakutimia, na kila mtu anahisi kulikuwa kuna njama ya wale waliokuwa watuhumiwa kuachiwa, si vyema kumuhukumu mtu kabla ila huwezi cheza ng'oma bila kupata vumbi au jasho
 
Huyu ni Jaji Masati leo kageuka kabisa....

Jaji Salum Massati wa Mahakama ya Rufani Tanzania, anayesikiliza kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Kaimu Kamanda na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar Salaam, Abdallah Zombe na wenzake tisa, amehoji kama kweli marehemu walikufa wakati wakipambana na polisi, kwa nini majereha waliyopata yanafanana.

Alisema kinachomtia shaka ni matokeo ya uchunguzi wa miili ya marehemu (postmoterm) kuonyesha kuwa marehemu wote wanne walipigwa risasi maeneo yanayofanana kisogoni, kinyume na maelezo kwamba kulikuwa na kurushiana risasi kati ya watuhumiwa na polisi.

Jaji Massati alielezea wasiwasi wake huo jana mara, baada ya mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Christopher Bageni, kuhojiwa na wakili wake, mawakili wa upande wa mashitaka na wazee wawili wa baraza.

Jaji alisema majibu ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa marehemu wote walipigwa risasi kisogoni sehemu zinazofana hivyo alihoji kama kulikuwa na mapambano baina yao na polisi kama inavyodaiwa na Zombe na wenzake, iweje sehemu zilizopita risasi katika miili ya marehemu zifanane.

Jaji Massati anayeisikiliza kesi hiyo ya mauaji katika Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema inaonyesha kuwa risasi zile zilipigwa moja kwa moja na si upande wa kati wa mashambulizi yanayosemekana yalikuwepo baina ya polisi na wafanyabiashara hao.
 
Leo hii ni furaha na vifijo kwa familia ya Zombe na washirika wake. Lakini pia ni siku ambayo Tanzania imeingia katika histori mpya. Historia ya kuwafanya wananchi wawe mahakimu wenyewe?, Polisi waendeleze uuaji na uporaji kwani wanajua kuwa sheria kwao haina tatizo. Ila cha kushangaza zaidi ni serikali kuonesha kuwa sheria si msumeno na majaji hawapo huru wanafuata amri za wanasiasa.

Kama kweli serikali ipo makini kwenye hili wakate rufaa hapo hapo. Haiingii akili polisi kuwatorosha wauaji kama jaji anavyosema huu ni usanii wa kisheria na kulindana. Macho yote ni 2010. Serikali ina agenda Moja tu tusipowalinda polisi hawatatulinda 2010. Haya nchi yao

POLENI SANA NDUGU WA MAREHEMU KINA CHIGUMBI.
 
Ni kweli inawezekana kwamba Zombe hana hatia. Lakini mambo kama haya ambapo jamii inaona wazi kabisa kwamba kuna uwalakini mkubwa halafu Mahakama inapindisha hukumu au inazingatia ushahidi ambao hauna uzito ili kufikia malengo wanayoyataka then hii ndio inawafanya watu kukosa imani na vyombo vya serikali.

Kwa hali hii wananchi wengi wataendelea kuvunjika moyo, kukata tamaa na kuendelea kukerwa na Serikali yao yote kwa ujumla.

Kila chombo cha serikali kwa sasa kinanyooshewa kidole kwa kuwa Dhaifu. Bunge kwa kushindwa kuwatetea wananchi pamoja na wabunge kujilimbikizia mali na kuonekana kutowajali wananchi, Serikali kwa kuwa mbali na wananchi na kufungia macho maovu makubwa kwenye jamii na Mahakama kuwa sehemu ya kuhalalisha uovu.

Inakatisha tamaa zaidi kuona kwamba mambo makubwa kabisa na yenye mustakabali wa kitaifa huchukuliwa kirahisi rahisi au hupindishwa wakati mambo madogo hukemewa na kuchukuliwa hatua kubwa ya kuyakomesha kabisa. Kwa hali hii itakua ni vigumu sana kukomesha Mob Justice (kuchukua sheria mikononi).

Hukumu ya Zombe is a big scandal, shame and mockery of the Justice system in our country but a tainted corruption and grave recklessness, lack of profesionalism, ignorance of the Attorney General Office, investigation and Police Department.

Hapo mkuu,

Sijui mtu yeyote ataanzia wapi kuwambia watu waache kuchukua sheria mkononi na badala yake wawafikishe watuhumiwa polisi na baadaye mahakamani.

Inawezekana mahakama imefuata ushahidi uliotolewa. Lakini kwa jinsi ambavyo watu wanavyoifahamu hii kesi na ilivyogusa hisia za wengi; kulikuwa na haja ya kuhakikisha kesi isionekane ni kishekesho au mchezo wa kuigiza. Binafsi naona aibu!
 
Sheria haijawahi kumlida mnyonge hata siku moja. Sheria zipo kwa ajili ya ruling class kwa kulinda interest zao basi. So see where you belong and decide.
 
tujenga kangaroo nation tusipokuwa makini, serikali inapenda kumfurahisha kila mmoja, waislamu wakitaka kadhi sawa, mtapewa, ukifika muda wa kuwapa usanii unaanza, hili la zombe lilionekana wazi, lilikuzwa bila sababu, tume za kuchunguza bila sababu, mashtaka dhaifu mahakamani bila sababu, wide coverage bila sababu, sasa learned judge amapta muda mzuri akasikiliza pande zote, akakataa kabisa hisia na magazeti tunamlaumu!
 
haya nilisema kuwa leo atakula ubwabwa kwake, na iliyobaki tutapiga yoweee but jioni tutasahau na kuangalia tena NEC huko dodoma, hii sio nchi ndugu zangu, hakuna haki,mwananchi wa kawaida heri ya mbwa, sasa hapo sheria mkononi ndo suluhu pekee, tuwe kama watalebani tuu,imagine familia za marehemu wale?wanauawa bila hatiahalafu hakuna wa kuwajibishwa?je huyu hakimu anaijua sheria?je rufaa inaweza pelekwa wapi?mungu tusaidie twafa!!
 
please uptade members and those inthe legal fratenity-learned brothers digest theissue when the rulling is completed
 
Back
Top Bottom