Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Bageni na wenzake si waseme waliua nini Sinza posta? huu nao ni upuuzi yaani mahakama inakubali kudanganywa tu. Sinza waliua nini? wakamwaga na damu ya bata, wakatoboa na matundu eti ni risasi. Serikali ikate rufaa mara moja.
 
No matter what, wale wafanyabiashara waliuwawa kinyama na mtu/watu. Zombe na wenzake waliongea uongo kwenye vyombo vya habari.
Poleni wana-mahenge na familia ya akina Chigumbi. Truth will prevail...
 
Mahakama zetu ni nzuri sana bado hazijaharibika kwa rushwa.

Wengi hamkuhudhuria kesi hii ilipokuwa ikisikilizwa, Zombe aliweza kuvunja chain ya kumuingiza yeye kwenye mauaji.

Mimi nimehudhuria mahakamani na Zombe mwenyewe na timu yake ya wanasheria ilikuwa na hoja nzito.
 
Sasa, mnasubiri kesi za EPA, kina Mramba na Kina Chenge? Hii ndio Tz.
 
Nimekosa imani kabisa na na hii mihimili ya DOLA kwa TZ!!! Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inabidi ikate rufaa. tutaanza kuhisi ibaya hata kifo cha LEMA kiliongezewa speed ili asitoe ushahidi.
 
Haya yote tumwachie Mungu kwani ndo anayejua...

Hii ndio fatalistic mentality inayotumaliza nchi changa hii.

Mungu ataku fixia justice system ya nchi yako how, amshushe Malaika Gabrieli awe Mkurugenzi wa Mashitaka?
 
huyu mtu hukumu yake haiko mahakamani iko kwa wanananchi wenyewe.yawezekana mahakama isineone kosa kwasababu hakushuhudia lolote
 
Ndugu wana JF napata simu huku porini kwamba watu wanakimbia kurudi Majumbani kisa Zombe kaachiwa yaweza kutokea vurugu .Je kuna ukweli wa jambo la Zombe kuachiwa ama jamaa kanipata tu ?
 
Hii ndio fatalistic mentality inayotumaliza nchi changa hii.

Mungu ataku fixia justice system ya nchi yako how, amshushe Malaika Gabrieli awe Mkurugenzi wa Mashitaka?
Hahaha...

- Ni mapenzi ya Mungu
- Hatuna jinsi, imeshakuwa tu
- Sasa mimi nifanyeje?
- Wakubwa washaamua bwana...
- Mungu atatusaidia tuu...

We acha tu!
 
ni kweli aise jaji hajawahoji pale Sinza waliua nini? na damu za pale sinza, na matundu waliyotoboa lol! leo ni siku ambayo sheria imeshindwa kabisa. woooote wako huruuuuuu
 
ni kweli aise jaji hajawahoji pale Sinza waliua nini? na damu za pale sinza, na matundu waliyotoboa lol! leo ni siku ambayo sheria imeshindwa kabisa. woooote wako huruuuuuu

Ina maana Jaji amehukumu kuwa wale waliouawa walikuwa majambazi au?
 
Mkuu naambiwa timu nzima ya Zombe wote wako huru ? Ama kweli nchi yangu Tanzania maisha ya mpiga kura hayana maana mbele ya ufisadi .Ina wale jamaa waliua na nani ?
 
Assuming anachosema INVISIBLE ni kweli kuwa kundi lile halikuwa na hatia walau kwa uamuzi wa jaji msomi massati, tunaelekea slowly but surely into anarchy,ambapo tutatumia sheria ya msituni:the survival of the fittest!

Baada ya precedence hiyo naamini mno katika UTOPIA (SOMA MUNGU MWENYEEZI) NAAMINI PAMOJA NA MZEE K.KAUNDA KWAMBA KISASI HALISI NI JUU YA MUNGU MWENYEWE NA ATAKITEKELEZA KWA WAKATI WAKE ILI WANAOCHEKA LEO WALIE KAMA WAKE NA WATOTO WA MAREHEMU WALE WALIVYOLIA!

Yule mwenzao mmoja waliyembadilishia kesi toka mauaji ya makusudi hadi mauaji ya kutokukusudia, mbona yalipomfika mauti Morogoro hawakuweza kumkingia.

MBONI ALIYEKUWA ANAELEKEZA ASAIDIWE HAKUMZUIA ZIRAILI HUKO MOROGORO? HAKUNA CHA BEST MAN WALA NINI!SO IT IS A MATTER OF TIME AND THE OMNIPRESENT, OMNISCIENT,OMNI POTENT GOD WILL MET OUT HIS JUSTICE TO ALL!VERY VERY PAINFUL!
 
Zombe hoyeeeee hez freeeeeeeeee nowwwww...but kaokota embe chini ya mkorosho alafu anafurahia..hauta pita mwaka lazima yatamkuta kama yale ya ditopile..mwache asherekee embe lililo dondoka kwenye mkorosho!
 
Hii ndio fatalistic mentality inayotumaliza nchi changa hii.

Mungu ataku fixia justice system ya nchi yako how, amshushe Malaika Gabrieli awe Mkurugenzi wa Mashitaka?

Mkuu hii ni kali.

Back to the point,

Issue kubwa si mahakama. Kesi ni ushahidi! JAJI hawezi kukufunga kama ushahidi uliotolewa ni hafifu. Muelekeze vidole vyenu kwa mwendesha mashtaki wa Jamhuri. Either alikuwa incompetent au ni kweli Zombe et al..hakuwa na hatia. Mimi sijui.

Harafu ile tume ya Prof. Juma hata kama ilibaini uzembe au uhusika wa watuhumiwa katika haya mauaji, mahakama hailazimiki kutoa hukumu kwa kutumia reference ya ile report ya kamati.

Kwa haraka haraka naweza kusema ofisi ya mwanasheria wetu iko VERY incompetent. Jamani wote mmeona mikataba ya akina Richmond nk..wote mnaona serikali inavyo-poteza kesi ambazo convictions zilikuwa imminent..Its so sad..But this is what happens when you politicize justice system. WATU WANAOGOPA KUFANYA KAZI ZAO kiutalaam.

Ngoja tusubiri acquittal ya akina Mramba na wenzake. Its so sad kweli.
 
Hakiak Zombe sasa tajiri .Vyeo atapewa , mishahara yote na kazini atarudi .Nchi yangu ina kazi kubwa sana .
 
Updated by Invisible:

Watuhumiwa wote wameachiwa hawana hatia!

08_09_m1wn67.jpg
Aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe akiwa nje ya jengo la Mahakama Kuu mkoani humo muda mfupi baada ya mahakama hiyo kumuachia huru yeye na wenzake wanane.
VIDEO | PODCASTSVIDEO ZAIDI | MAONI
 
This has been the sad tread of the day!!! Nakumbuka msemo usemao "Ng'ombe wa maskini hazai". Kweli mkulima yule wa Mahenge aliyetegemea wanawe kwa kipato cha madini, biashara halali, waliuawa halafu eti leo hakuna kosa??? Na unataka kuniambia kuwa vyombo vya upelelezi vilishindwa kuwakamata wauaji halisi, au tuseme ni maandalizi ya kesi yenyewe yalidhamiriwa hivyo kuanzia mwanzo kwa kuwa wenye mapeni waliyapenyeza?? Kila mahali ni ufisadi tu.
This is a shame!!! ..... All the accused not guilty!!!!! Haingii kichwani kwangu. Ilipangwa kuanzia awali wakati wa uandaaji wa mashtaka!!!

Kuna kisa cha kuchekesha zaidi!!! Naamini mtakumbuka ule wizi wa hela za NMB pale mataa ya Ubungo!!! Kuna shahidi mmoja muhimu sana ambaye ni dereva alinyang'anywa gari ili kufanikisha wizi ule na baadaye gari ilipatikana kama yalivyopatikana mengine (kumbuka walikuwa wanapora magari na kuyatelekeza baada ya short driving). Yule dereva aliweza kuandika maelezo na ku-identify 5 criminals bila utata kabisa na aliandika ushahidi mzito sana. Kesi iliendeshwa, wakati anaitwa kuja kutoa ushahidi ilishindikana maana yale maelezo yake ya gwaride la utambuzi yalibadilishwa na yale aliyoandika kituoni (ya awali kabisa) yalipotea!!! Mwenye gari aliposikia hivyo kwa kuwa anajua sheria aliwavaa watu wa DPP na wakakiri kuwa wanafatilia na watamwita baadaye na sidhani kama shahidi huyu muhimu aliitwa tena!!!! Huyuu shahidi ndiyea angetoa uhakika wa kuwatia watuhumiwa 5 kati ya zaidi ya kumi hatiani, lakini mchezo mchafu ulichezwa!!! Hii ndizo systems ambazo zinatakiwa ziwasaidie wananchi.

______________________________________________________

Currently Active Users Viewing This Thread: 467 (139 members and 328 guests)
Maane, 7ceven, Aljazeera, AmaniKatoshi, Arsenal, babukijana, Balantanda, Bambo, Bambo jr, Belo, Bint, Bongolander, BornTown, Buchanan, Bujibuji, Buswelu, Bwana, Chakaza, Chaku, Damky, Dawson, Dilunga, Ebrigitha, FairPlayer, Fatuma, Fidel80, gervase malimi, GM7, gn30, hampungas, Herg, Hofstede, Hujale, Inviolata, Ipo siku, itubi, IVAPI, Jafar, joellincoln, JosM, jubest, Kafiribangi, Kagoma, KAM, Kang, Katibukata, Kenge (Eng), Kicheruka, Kigoma, Kimambo, Kimbweka, Kimori, kinepi_nepi, Kireka1980, Kite Munganga, Koiya, KOMBESANA, kunda, Kuntakinte, Kyemba, libidozy, Lunanilo, Lussadam, Magezi, Makingi George, Malunde-Malundi, Masatu, Masikini, Mateso, Maverick, Mbalamwezi, Mburahati, Mbwajira, mchakato, mchizi, Mchukia Fisadi, Mhafidhina, Minael, Mnhenwa Ndege, mnozya, MP, mpingo, Mpingo1, Mponjoli, msadiki, msaranga, Msindima, Mtabaruka, Mtana, Mtu66, muadilifu, Mugo"The Great", mujuni2, Mundu, mwaka, mwalimu, Mwita Maranya, Mzee Mwafrika, mzundu, Naminyo, Ncha, Ndaga, Nego, Ngongo, Njilembera, Novatus, Offish, Pasco, PhD, Pretty, Prince, rkili, Robin, ronaldinho, rosebella, Safari_ni_Safari, Santa-Mariah, Shy, siame jg, sinani, Solent, Son of Alaska, SONDAS, taffu69, Thadeus, ThinkPad, tsidekenu, Tuandamane, TzPride, Ulamaa, Utamaduni, vstdar, Wa mmoja, Wa Tsavo, Wakunyuti, Wambandwa, watu, ygjunior
 
Back
Top Bottom