Zombe huyo nje na wenzake!!!!. Wote wametolewa kwa mlango wa nyuma kwa magari mawili ya polisi landcriser p/up wakiwa wanashangilia kama mashabiki wa mpira waliopanda p/up. Huku magari matatu ya polisi na silaha kali wakiwalinda. Kote kulikuwa kumemwagwa askari kanzu nje na ndani, magari ya FFU na gari la maji washawasha!!!Kwa mtizamo wa kiundani huo tangu asubuhi ule ulinzi ualiashiria mamamuzi ya kuwachukiza wananchi.
Wenye vyombo vya habari jiandaeni kwa kesi za fidia, serikali jiandae kwa fidia!!!
Je sasa, ni nani aliwaua wale wazalendo?? Je ni mtu mmoja Saadat aliweza kuwabeba wote na kuwapeleka pande bila msaada na kuwalipua??? Jamani sijaelewa hizi mnazosema sheria!!! Ila kuna jambo, subirini na yule mzee Mahenge atajibu, tena kwa kishindo, aliapa!!!!! Msiniulize atajibu kivipi, ila atajibu.