AljuniorTz
JF-Expert Member
- Jan 6, 2009
- 544
- 19
Updated by Invisible:
Watuhumiwa wote wameachiwa hawana hatia!
Hii ndio Tanzania, kuna watu miongoni mwetu watakula wali hadi wanakufa; kuna watu watakula ukoko hadi wanakufa na kuna watu watakula matandu hadi wanakufa.
Mwenye nacho ataongezewa daima dumu na asiekuwa nacho ataendelea kunyang'anywa hata kile kidogo alichokipata.
Kisingizio tunaambiwa ushahidi uliotolewa hauna nguvu za kuwatia hatiani moja kwa moja, ndio yale yale "... marehemu alikuwa ndio mwenye makosa...". Hatujajua hukumu imesemaje kuhusu wale ndugu zetu waliouawa. Je, WALIKUWA NI MAJAMBAZI???
Ila tukumbuke UBAYA WOTE HULIPWA HAPA HAPA DUNIANI, na watalipwa, watalipwa, watalipwa kwa waliyoyachuma kwa mikono yao kabla hawajarudishwa kaburini wakiwa hawana kauli.