Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Zombe kaachiwa!! Mie nilisema hii nchi, viongozi wake ni kama mawe, hayasikii!! Very dissappointing! Sasa ina maana wale waliouawa walikuwa ni majambazi au? Tumewachoka viongozi wa nchi hii na mahakama yenu, I wish watanzania tungefungua macho na kuona kwamba kuongea tu haitoshi!
 
Last edited:
Zombe huyo nje na wenzake!!!!. Wote wametolewa kwa mlango wa nyuma kwa magari mawili ya polisi landcriser p/up wakiwa wanashangilia kama mashabiki wa mpira waliopanda p/up. Huku magari matatu ya polisi na silaha kali wakiwalinda. Kote kulikuwa kumemwagwa askari kanzu nje na ndani, magari ya FFU na gari la maji washawasha!!!Kwa mtizamo wa kiundani huo tangu asubuhi ule ulinzi ualiashiria mamamuzi ya kuwachukiza wananchi.

Wenye vyombo vya habari jiandaeni kwa kesi za fidia, serikali jiandae kwa fidia!!!
Je sasa, ni nani aliwaua wale wazalendo?? Je ni mtu mmoja Saadat aliweza kuwabeba wote na kuwapeleka pande bila msaada na kuwalipua??? Jamani sijaelewa hizi mnazosema sheria!!! Ila kuna jambo, subirini na yule mzee Mahenge atajibu, tena kwa kishindo, aliapa!!!!! Msiniulize atajibu kivipi, ila atajibu.

kwi kwi kwi, si heri ya sheria mkononi? haya ya haki hatuyawezi sisi, kwasababu wapelelezi ni dhaifu sana.
 
Habari ndio hiyo, jaji anadai watuhumiwa wote hawahusiki, amewapa kazi polisi polisi wawasake waliohusika kuwaua. Jaji anadai upande wa mashtaka wameshindwa kuprove beyond reasonable doubt kwamba kina Zombe wanahusika na mauaji!
 
Mi hii nilisha angalia toka mwanzo jamaa atachukua ushindi, serikali inashindwa kutengeneza mashtaka na inashindwa kukusanya ushahidi ulio jitosheleza mnategemea nini tatizo lipo kwa hao wanao endesha mashtaka.
 
Kwa jinsi ninavyomjua yule mvimba macho hakiyanani waandishi kaeni chonjo hasa wale waliomuhukumu kabla, hana masihara eti yule!!!, acha hiyo fidia lkn mkono wake pia atautumia kisawasawa, yaani ni kama kumuona osama ameingia ofisini kwako
 
Leo Masati ametoa maamuzi yanayochanganya sana,Kweli the "court is not your mama"
 
Naanza kupata picha kwanini huku uswahilini kwetu wakikamata mwizi, jambazi etc wanaamua kumaliza kesi wenyewe!
 
Kaka umenigusa sana zombe ni fisadi aliyeua watu very directly akina mramba , rostam ,el , jkm, karamagi na wenzao wanatuua watanzania polepole so mi nafikiri zombe ahukumiwe kunyongwa instantly na hao mafisadi wengine tuwakamate tuwaue taratibu leo unakata mguu wa kulia a month later wa kushoto unasubiri miezi miwili unakata mkono naamini kwa stahili hii tanzania itanyooka tu.

si JK si zombe wote wauaji tuu.. lkn bana waangalie wameumiza sana watu halafu wanaachiwa huru kisa mwanasheria ameweza kupindishapindisha maneno pale mahakamani kitaalamu.. kuna hukumu za nje za mikononi mwa watu walioadhiriwa na hawa watu
 
Kwa jinsi ninavyomjua yule mvimba macho hakiyanani waandishi kaeni chonjo hasa wale waliomuhukumu kabla, hana masihara eti yule!!!, acha hiyo fidia lkn mkono wake pia atautumia kisawasawa, yaani ni kama kumuona osama ameingia ofisini kwako

Kwani wananchi wenyewe hawana mahakama zao? Mbona tunazitumia kila siku kwa KCC? Naomba Zombe afikishwe huko tuondoe udhia!
 
Haki inadaiwa kivyoyote wewe, hata kumuua jaji Masati....kumbuka watu wamepoteza ndugu zao kwa ulafi wa Zombe, na ni dhahiri bado tunaletewa za kuleta. Acha woga, mafisadi hawana msalie mtume.

Hapo juu.....ningekuwa mi ndo hao ndugu za wale marehemu....nge do the needful.....labda ni si mjukuu wa Mkwawa!
 
Hatimaye kaachiwa!! Haya ndio mambo ya sheria za kibongo bongo. Bado zamu ya Liyumba, naye atatoka soon.
 
Kwa maana hiyo wale wafanyabiashara wa madini walijiuwa wenyewe! Si shangai wananchi wanapoamua kuuwa vibaka mtaani, bado kidogo wataanza shughulikia fisadi.
Aliyeua alishatoroshwa, itakuwa ni kurudia kosa kuwahukumu kifo watu ambao hawakuua
 
tusipoteze muda.. I told you from the very begining ..kuwa zombe hatafungwa ..kwa kuwa he was doing what he use to do in the name of the republic....hata kama kwenye undertaking amekosea...hayo ni makosa kazini...impact ya kumnyonga ingekuwa kubwa kuliko kumwachia..

kumnyonga kungeondoa morali wa kazi wa maafisa wengine wenye crown....ambao wanaendelea kufanya kazi kama ya zombe!!! Kazi za namna hiyo zipo kwenye taifa lolote.....ikifikia mahali walinzi wa amani wakijiona kuwa ..kwenye utendaji wao wakikutwa na kosa wanaenda kusulibiwa hadharani na si kwenye mahakama za kijeshi ....au chombo huzika ....taifa linakuwa linapoteza muelekeo...na kunakuwa hakuna siri !!

ndio maana marekani kwenye hili wapo straight ....wamelazimisha mkataba unaozuia askari au kiongozi wao anayetekeleza majukumu popote pale kushitakiwa the hague au kwenye maakama nyingine zaidi ya za kwa [za kijeshi]....ili kuondoa uwezekano wa kuadhirika!!!

kesi ya zombe ilikuwa ni sanaa nyingine...kwani hukumu yake ilikuwa inajulikana si lolote.....ni ile hali ya kuwa na serikali inayopenda kuwafuraisha watu hata kwenye mambo ambayo wananchi wa kawaida hawakupaswa kuyajuwa.....ulikuwa upotezaji wa muda wa hali ya juuu!!!

na matokeo ndio haya ....
 
Timu ya wanasheria waliomsimamia huyu jamaa imetengeneza CV ya nguvu.Watafanya sana biashara.
 
Mkuu Naminyo, daima sheria huwa tunataka ichukue mkondo wake, na hali ndivyo ilivyokuwa.

Tarajia hali kama hii hii kwenye kesi za EPA n.k.

Inafurahisha sana, Mungu ibariki Tanzania
Na watu wake!
 
Naamini kulikuwa na mapungufu upande wa mashtaka otherwise Masati huwa ni very strict and systematic judge. AG anatakiwa akate rufaa au wadakwe wafunguliwe mashtaka upya.

Ukweli huo ulionekana hata wakati wa utoaji ushahidi,mashahidi karibu wote ushahidi wao ulikuwa ni wa hisia zaidi kuliko ukweli husika,Binafsi niliamini Zombe angeachiwa kutokana na ushahidi dhaifu uliotolewa.

Tufikie mahala tuwe tunaangalia mwenendo wa kesi na si kushangaa hukumu,kulikuwa na mapungufu mengi mno kwa mashahidi wa mashitaka wakitoa ushahidi dhaifu mno uliotanguliwa na jazba bila kuangalia uzito wa kesi ya mauaji.Binafsi ningeshangaa kama JUDGE angeweza kutoa hukumu kwa kuangalia mazingira ya nje ya mwenendo wa kesi na si ushahidi na mwenendo mzima wa kesi...

Pia hili ni fundisho kwa vyombo vyetu vya habari kwa namna ambavyo vinaweza kupotosha sheria,naamini kama JUDGE angekuwa dhaifu angeweza toa hukumu ili kufurahisha jamii na si kwa kuangalia mwenendo wa kesi na ushahidi,Kwa kweli JUDGE amekuwa objective.nilifuatilia kwa makini kesi ya Zombe na kwa kiasi kikubwa ushahidi kwenye kesi ya kuua ulikuwa ni dhaifu mno,kwa kiasi kikubwa kesi ilikuwa ni ya kisiasa zaidi.

Hi ni changamoto kwa wanahabari kuipitia hukumu ya JUDGE na kuangalia namna alivyofikia hitimisho na madhaifu atayoonyesha kwenye marejeo ya ushahidi na mwenendo mzima wa kesi kwa ajili ya kuinua upeo wetu wanahabari kwenye habari zinazohusu mambo mazito kama haya ya mauaji ya kukusudiwa yatendwayo na baadhi ya maaskari wetu.
 
Back
Top Bottom