Hukumu ya Segerea Watanzania tumejifunza nini?

Walidai kuwa kuna ushahidi mwingine wa mashahidi wao ambao Jaji ama aliuruka au hakuupa uzito. Wakili Kibatala alisema wameamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na kwamba leo wanawasilisha mahakamani taarifa ya kusudio hilo. Licha ya Jaji kusoma hukumu hiyo kwa Kiswahili, ilidhihirika kuwa bado kuna wafuasi wengine wa Chadema ambao waliielewa kinyume.

Walidai kuwa pamoja na Dk Mahanga kushinda, Jaji amewaamuru mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mdaiwa wa tatu, Msimamizi wa Uchaguzi (RO) walipe gharama za kesi. "Sasa kama Makongoro alishinda kihalali kwa nini awaamuru wengine walipe gharama za kesi? Hii si inadhihirisha kuwa walikiuka taratibu,?" alisikika mmoja wa wafuasi hao akihoji huku akiungwa mkono na wafuasi wengine.

Mwananchi
Hukumu hii naifananisha na hukumu iliyotolea na kamati cha ligi iliyoipa Azam FC ushindi huku refari akifutwa kuchezesha kabisa soka nikawa najiuliza sasa kama kosa ni la refa iweje Azam wapewe ushindi lakini jana haki imetendeka Game litarudiwa hata hii nina uhakika majaji wataweka pembeni unazi wao zidi ya CCM...Mahanga siyo mbunge....
 
Nlidhani gharama atalpia Mpendazoe kumbe sivyo!
This is possible only in Tanzania bse alyenzisha kesi ni Mpendazoe.
Anyway leta hukumu kwanza maana mapovu yasije yakaanza kututoka kumbe sivyo
 
Katika kusoma habari hii kwenye magazeti amabayo yameainisha hukumu ya kesi ya uchaguzi Jimbo la Segerea kumpa ushindi Makongoro dhidi ya Mpendazone, utata ambao nimeuona katika gazeti Mwananchi ni hapa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi kulipa gharama za uchaguzi, ni dalili tosha kwamba kulikuwa na udhaifu wa utendaji ambao vyombo hivyo vimehusika, vinginevyo Mpendazone pekee aliyefungua kesi angebebesha mzigo huo.

Kwa hiyo makosa ya NEC ambayo yalifanywa makusudi kwa ajili ya kuibeba CCM, basi hayawezi kutengua matokea? Ngoja tuone ya Mnyika itakuwaje, maana tunaweza kuona double standard hapa sasa!
 
Hukumu hii naifananisha na hukumu iliyotolea na kamati cha ligi iliyoipa Azam FC ushindi huku refari akifutwa kuchezesha kabisa soka nikawa najiuliza sasa kama kosa ni la refa iweje Azam wapewe ushindi lakini jana haki imetendeka Game litarudiwa hata hii nina uhakika majaji wataweka pembeni unazi wao zidi ya CCM...Mahanga siyo mbunge....

Jamaa akiula uwaziri tena basi tusahau Ikulu lazima itaingilia mamlaka ya mahakama hivyo haki itabakwa.
 
Sikilizeni jamani uozo Wa mahanga unajulikana na hao wasimamizi walitangazaje matokeo kabla ya vituo vyote kuwasilisha kura zote inamana walishaona mahanga kapigwa na M .Zoe sasa Kama kweli hakimu ameona mkurugenzi na msimamizi wanatakiwa kukupa garama za kesi basi uchaguzi huo haukuwa Wa haki tutawalaani na wataendelea kuchukiwa kila panapokucha.
 
Ok! As far as I know anayeshindwa hutakiwa kulipa costs! Sasa inapotokea upande mwingne kulipishwa, tena gharama zote, tatizo linajidhihirisha!
 
Ukweli ni kuwa tuwekeeni hukumu tuione!.

Katika kupitia magezeti kadhaa ambapo waandishi walikuwa katika kesi hiyo Mahakama kuu, nimeshtushwa na habari kwamba Mwanasheria wa serikali na msimamizi wa uchaguzi wanabeba mzigo wa kulipa gharama za uchaguzi, kwa nini magazeti mengine hayajaandika ukweli huo? Au gazeti la Mwananchi limezua uwongo?
Kama ni kweli hukumu ndio hivyo,
ukiukwaji wa uchaguzi ulifanywa na mwanasheria wa serikali
Hali kadhalika Msimamizi wa Uchaguzi alivuruga uchaguzi, la sivyo wasingebebeshwa mzigo.
 
Kwani kama chadema hawajashinda/madai yao kukubaliwa, ndiyo tiketi ya haki kukiukwa siku hizi?.
.
"Ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Walidai kuwa kuna ushahidi mwingine wa mashahidi wao ambao Jaji ama aliuruka au hakuupa uzito. Wakili Kibatala alisema wameamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na kwamba leo wanawasilisha mahakamani taarifa ya kusudio hilo. Licha ya Jaji kusoma hukumu hiyo kwa Kiswahili, ilidhihirika kuwa bado kuna wafuasi wengine wa Chadema ambao waliielewa kinyume.

Walidai kuwa pamoja na Dk Mahanga kushinda, Jaji amewaamuru mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mdaiwa wa tatu, Msimamizi wa Uchaguzi (RO) walipe gharama za kesi. "Sasa kama Makongoro alishinda kihalali kwa nini awaamuru wengine walipe gharama za kesi? Hii si inadhihirisha kuwa walikiuka taratibu,?" alisikika mmoja wa wafuasi hao akihoji huku akiungwa mkono na wafuasi wengine.

Mwananchi

Mimi nimesoma gazeti la mwananchi, kwa mujibu wa gazeti mtu anayetakiwa kulipa gharama ni yule aliyeshindwa kesi. Angalia red kwenye hiki kipande nilichonukuu kutoka kwenye gazeti. Gazeti limeeleza vizuri kabisa kuwa licha ya hukumu hiyo kusomwa kwa kiswahili ilidhihirika kuwa bado kuna wafuasi wengine wa CHADEMA ambao waliielewa kinyume. Angalia red tena hapo chini kwenye kipande cha nukuu ya gazeti.

Kwa kifupi kutokana na gazeti la mwananchi hukumu iko very clear kuwa aliyeshindwa kesi ndiye anatakiwa kulipa gharama za kesi.

''Hivyo ninaamuru kwamba Dk Milton Makongoro Mahanga alichaguliwa kihalali kuwa Mbunge wa Segerea, cheti kitatolewa kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuthibitisha kuwa alichaguliwa kihalali na mdaiwa wa kwanza, wa pili na wa tatu watalipwa gharama za kesi," alisema Jaji Profesa Juma''

KUMBUKA MDAIWA WA KWANZA NI MAHANGA, WA PILI NI MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI(AG) , NA WA TATU NI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI(RO). SASA HAWA NDIO WASTAHILI KILIPWA GHARAMA ZA KESI NA SIO WAO KULIPA.

Walidai kuwa kuna ushahidi mwingine wa mashahidi wao ambao Jaji ama aliuruka au hakuupa uzito. Wakili Kibatala alisema wameamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na kwamba leo wanawasilisha mahakamani taarifa ya kusudio hilo. Licha ya Jaji kusoma hukumu hiyo kwa Kiswahili, ilidhihirika kuwa bado kuna wafuasi wengine wa Chadema ambao waliielewa kinyume.

Walidai kuwa pamoja na Dk Mahanga kushinda, Jaji amewaamuru mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mdaiwa wa tatu, Msimamizi wa Uchaguzi (RO) walipe gharama za kesi. "Sasa kama Makongoro alishinda kihalali kwa nini awaamuru wengine walipe gharama za kesi? Hii si inadhihirisha kuwa walikiuka taratibu,?" alisikika mmoja wa wafuasi hao akihoji huku akiungwa mkono na wafuasi wengine.
 
Hao ndio majaji-ccm, a.k.a majaji wa voda fasta.
Ni watu wa vituko sana, akili zao kama mwanaasha.
 
Ili kuwa na mjadala wenye tija kwa wale wenye uwelewa mdogo wa haya maswala ya sheria ni bora kungoja nakala ya hukumu ya kesi ya Mpendazoe ili kuona kilichojiri.Kwani inawezekana mwandishi wa Mwananchi hakusikia vizuri au amenukuu vibaya.
 
Kuna dalili za wazi kuwa tukiweka upande ushabiki wa kisiasa, Mpendazone hakuwa na ushahidi wenye vielelezo vya kuthibitisha tuhuma za kuvuruga ushahidi. Walao angejitahidi kufanyia kazi tuhuma moja kikamilifu ambayo ingekuwa na vielelezo vya wazi angeshinda, lakini hii ya longolongo mahakama haihitaji zaidi ya ushahidi wa wazi si wa kusikia au kuambiwa.

Nisingefikiria kukata rufaa ni kuzidi kujiongezea gharama ambazo zinaweza kuepukika, kwani sitazamii kama matokeo yatabadilika kutokana na kutoleta ushahidi wa wazi mahakamani usioleta shaka pamoja na vielelezo vyake.
 
Ili kuwa na mjadala wenye tija kwa wale wenye uwelewa mdogo wa haya maswala ya sheria ni bora kungoja nakala ya hukumu ya kesi ya Mpendazoe ili kuona kilichojiri.Kwani inawezekana mwandishi wa Mwananchi hakusikia vizuri au amenukuu vibaya.

Kadiri ya Mwandishi wa Mwananchi alisema uelewa mdogo wa waliohudhuria mahakama na kuitafsiri visivyo hukumu hiyo, lakini yeye kama mwandishi angetakiwa kutoandika kitu kama hicho ambacho kinakanganya wasomaji wa gazeti. Na sijaona kitu kama hicho katika magezeti mengine yaliyoandika habari hiyo.
 
Kupitia uzi huu naomba kufahamishwa endapo jaji akitoa hukumu kwa mizengwe na kupendelea kuna mtu wa kuweza kumwadabisha kama ilivyo kwa marefa wa mpira?
 
Back
Top Bottom