Hukumu ya Segerea Watanzania tumejifunza nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya Segerea Watanzania tumejifunza nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naytsory, May 3, 2012.

 1. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Inanipa shida kuamini kama mahakama zetu zinatenda haki hasa pale ambapo mshitakiwa ni kiongozi wa serikali au mfanyabiashara mkubwa hata kama kuna ushahidi uliojitosheleza. Kwa hali hii 2015 tutakapomkamata mgombea au kada wa chama tawala (ccm) anakiuka sheria ya uchaguzi hatuna haja ya kumkabidhi kwa vyombo vya dola, tutamshughulikia wenyewe hata iwe fundisho kwa wengine wanaotarajia kulindwa na vyombo vya dola. Tutawahamasisha nguvu ya umma katika hili na hasa vijana, nawasilisha kwenu wakuu.
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Labda gap hili litazibwa na katiba maana mfumo wa saizi unaoondoa independence ya mahakama kwa kuwa wao ni wateule wa rais.
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Lusambo!

  Nimeipenda hii hakika!
   
 4. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Chini ya utawala uliopo na wabunge wengi wa ccm sina imani kama maamuzi ya wananchi yataheshimiwa. Maana wako kimaslahi na kichama zaidi.
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Naytsory!

  Nakwambia hata chama chao hawajengi tena!
  Hakika wapo kwa ajili ya matumbo yao na familia zao tu!

  Kwa ujumla ni janga kwa Taifa letu!
   
 6. B

  Bubona JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama hatuwezi kupitia mlangoni na nyumba haina madirisha, njia pekee tunayobakiwa nayo ni kufumua paa!!
   
 7. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mteule wa mteuliwa hata akifanya nini, ni kitu gani kitakachotushawishi kuwa ametenda haki? Labda awe radical na mwenye morals za hali ya juu lakini wote wako kwa maslahi ya aliyeteua. Huu ndiyo mfumo watawala wanaulilia ubaki. Labda tufike mahali kwa kujichukulia haki wenyewe kwani kwa mfumo huu sioni mtoa haki!
   
 8. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Let bygone be bygone, there's a difference btn LAW & JUSTICE!Law iz there bt it cant exercise justice effectively coz who enacted it uses it as a defensive mechanism!There must b anaza way,we must find it by anymeans!
   
 9. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Lakini inawezekana vipi Jaji atende haki ikiwa haimfurahishi aliyemteua? Vinginevyo kwa ridhaa ya aliyemteua na ikiwa maamuzi hayana madhara kwa chama tawala wala si kwa katiba ya nchi waliyoapa kuilinda. Watanzania kwa pamoja tunaweza kuhukumu kwa haki na kwa maslahi ya Taifa.
   
 10. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilichojifunza ni kwamba, ili uweze kupata haki uwe na urafiki na wakubwa kama na mh. Rais na majaji, pia muwe mmesoma pamoja kama pale UDASA..hapo haki utaipata tanzania!
   
 11. n

  nalekwando New Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nimejifunza kwamba hata wao ccm wanafahamu kuwa mahakama zetu hazitendi haki; inategemea tu Nani anashitaki nini kwa interest ipi. Kwa hiyo kutegemea hukumu kama ya mahanga ni kawaida sana;hata rufaa haiwezi kusaidia. Labda kama rufaa ingekuwa inasikilizwa kimataifa hapo ndo ungeona haki inatendeka kwa kuogopa kwa majaji wetu kuumbuka.
   
 12. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nilichojifunza ni kuwa "Sheria zipo ili kuweka utaratibu na usimamizi wa namna ya kuendesha kesi na kutoa hoja na sio kusimamia HAKI, vilevile Majaji wapo ili kutoa haki kwa matakwa yao au waliowateua"

  Hivi kwa kesi kama ya MAKONGORO ilivyokuwa na matundu madogo kiasi kile amewezaje kutoka bila hata kubomoa ukuta ili apate nafasi kubwa ya kupita...??

  Kesi,mashahidi,ushahidi,jaji, sheria, hukumu, adhabu....Wanasheria kazi ipo!!
   
 13. k

  kabombe JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,649
  Likes Received: 8,607
  Trophy Points: 280
  Malalamiko yote hapo hapo juu ni kama matusi kwa wanaoamini sheria.Mbona sehemu nyingi tu CCM wamebwagwa na mahakama?Aeshi anatisha Sumbawanga nzima..katika kila investment 3 za maana mji ule moja yake lakini katupwa.Tunatakiwa tuelewe kuwa Mahakamani la msingi ni ushahidi usio na shaka
   
 14. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Kwa matukio mengi yaliyojiri ktk uchaguzi mkuu 2010 na chaguzi ndogo zilizofuata kwa upande mmoja na mwenendo wa mahakama na polisi kwa upande mwingine, natabiri kuwa kutakuwepo na matukio mengi ya wananchi kujichukulia sheria mikononi chaguzi zijazo kutokana na kukosekana kwa haki ktk mihimili hii ya dola.
   
 15. Non stop

  Non stop Senior Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa hukumu ile ya jana, mbali na Mahanga kuzomewa kwamba mwiziii mwiziiii,.watawala wetu wasitegemee kupata heshima tena kutoka kwa watawaliwa, na vitendo hivi naamini vinachochea zaidi mageuzi hasa pale haki inapoonekana wazi kisha inapindishwa kwa either nguvu ya pesa au kwa mabavu.,2015 haiko mbali sana naamini kilio cha watz hakitaenda bure, malipo yake yanakuja.
   
 16. n

  nalekwando New Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikukuita vuvuzela itakuwa ni haki yako;acha ushabiki wa kijinga wewe. Tumia mkali kufikri " nyanoko"
   
 17. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hawa majaji wamekuwa wachumia tumbo kupitiliza. Wanaidhalilisha professional yao sana, sijui wanachokiogopa ni kipi, ukishateuliwa jaji, rais haweze kumtengua judge from that post, unless amefanya professional misconduct, na sub committee ya majaji wa jumuia ya madola waka prove that. Lkn hawa majaji wamekuwa waoga mno, huwezi kuwatofautisha akili zao na mtu kama Nepi.
  Wamesahau majukumu yao, wamebakia kuwa kama laba stampu ya wana ccm, kwa kweli ni aibu sana...
   
 18. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hivi mkuu, mh. Mahanga alikamatwa na masanduku ya kura na kituo cha polisi kapelekwa, ushahidi huo umetolewa mahakamani, hilo tu halitoshi kuwa amevunja sheria ya uchaguzi? Mbona ushahidi dhidi Mbunge wa Arusha Mh. Lema haukujitosheleza lakini maamuzi ya Jaji hata wenzake walimshangaa. Mh. Aeshi ushahidi ulijitosheleza na ndiyo maana wananchi walionekana kuridhika na hukumu. Usijustify kwa kuwa ccm walishindwa Sumbawanga basi na iwe hivyo kwa CDM, hautakuwa sahihi. Yawezekana hukuwa unafuatilia kesi hizi.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Walidai kuwa kuna ushahidi mwingine wa mashahidi wao ambao Jaji ama aliuruka au hakuupa uzito. Wakili Kibatala alisema wameamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na kwamba leo wanawasilisha mahakamani taarifa ya kusudio hilo. Licha ya Jaji kusoma hukumu hiyo kwa Kiswahili, ilidhihirika kuwa bado kuna wafuasi wengine wa Chadema ambao waliielewa kinyume.

  Walidai kuwa pamoja na Dk Mahanga kushinda, Jaji amewaamuru mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo,
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mdaiwa wa tatu, Msimamizi wa Uchaguzi (RO) walipe gharama za kesi. “Sasa kama Makongoro alishinda kihalali kwa nini awaamuru wengine walipe gharama za kesi? Hii si inadhihirisha kuwa walikiuka taratibu,?” alisikika mmoja wa wafuasi hao akihoji huku akiungwa mkono na wafuasi wengine.

  Mwananchi
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katika kusoma habari hii kwenye magazeti amabayo yameainisha hukumu ya kesi ya uchaguzi Jimbo la Segerea kumpa ushindi Makongoro dhidi ya Mpendazone, utata ambao nimeuona katika gazeti Mwananchi ni hapa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi kulipa gharama za uchaguzi, ni dalili tosha kwamba kulikuwa na udhaifu wa utendaji ambao vyombo hivyo vimehusika, vinginevyo Mpendazone pekee aliyefungua kesi angebebesha mzigo huo.
   
Loading...