Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,933
- 4,706
Katika gazeti la mwananchi la leo kuna mahojiano yaliyofanywa kati ya mwananchi na mwanasiasa mkongwe nchini Msuya ambaye aliwahi kushikilia nyadhifa za juu katika uongozi wa Tanzania. Nilipokuwa nafuatilia maoni yake nilikutana na neno ambalo limekuwa likinitatiza mda mrefu. Neno lenyewe ni USWAHILI. Binafsi nimekuwa nikijivunia lugha yangu ya kiswahili hasa ninapokuwa na watu wa mataifa mengine wasiokijua. Hapa tena nakutana na mtanzania tena mwenye hashima kubwa kwa nafasi yake anautaja USWAHILI kama tabia kinzani.
Hapa nikijaribu kumnukuu Msuya :- 'Clinton alikuwa na kashifa ya ngono na kunusurika kupoteza urais, wenzetu hawana utani katika sheria, hawana mchezo. HUKU KWETU TATIZO BADO KUNA USWAHILI' mwisho wa kunukuu.
Hapana shaka kwamba msuya ana maanisha serikali yetu sii makini.
Hebu wakuu wa JF nisaidieni umakini wetu tutaupata kwa kuiepuka lugha yetu ya kiswahili? Au uswahili unaolaumiwa hapa na mara nyingi tu huko nyuma nimesikia ukilaumiwa ni nini haswa? Tusaidiana tafadhali.
.