ALITUANGUSHA SANA KWA KUKUBALI NYUMBA ZETU ZIUZWE..hilo tu lakini mengine huyu jamaa anaweza mnyonge mnyongeni..haiwezekani watu wawe wanajiamulia tu kufanya ujinga kama nchi haina kiongozi na sisi tubaliki ujinga...
if i was magufuri, i would have done the same, nampongeza kwa alichofanya. hii nchi si kilabu cha pombe kwamba watu wanaweza kufanya chochote kama vile hakuna uongozi na mamlaka.
siku Tanzania tukija kujikomboa kutokakwenye huu ukoloni wa wauza mafuta, wamiliki wa malori na wengine nitashukuru Mungu. nafikiri serikari yetu sasa ihakikishe inaboresha reli ya kati na tazara ili nchi iwe huru. tutaburutwa hadi lini?
sijafurahi unaposema nabwabwaja, hii ni lugha ya wahuni, si lugha ya watu wazima wenye busara. sijui umri wako. sisi wengine hatujazoea kutukanwa. kama ungekuwa na busara ungefafanua zaidi nielewe pale ambapo unafikiri sijaelewa bila kutamka kuwa nabwabwaja. this is a discussion forum. hata hivyo, nilijua kuwa hapa tunajadili effects za mgomo wa malori, si hayo mengine unayosema magufuli amefanya. huko mimi siko, sikujua kuwa suala limeletwa hapa kama shambulizi dhidi ya mtu, pengine una ugomvi naye who knows; hiyo tu kuongea kama mhuni uliponijibu unaonyesha kuwa haujafikia kiwango cha watu wazima kuweza kujadili hoja, hivyo hata hii topic unaipunguza thamani kwa hadhi ya mtu aliyeileta. samahani, kwaheri.
Kwani hii forum ni ya kufurahishana!uyo BAK hajakosea ni kweli hapo nilipobold unategemea nini unapomwaga petroli kwenye moto.wenye akili wameona liwaziri lako limeleta hasara ,limetuaibisha,limetufedhehesha wewe unakuja kutuletea Non sense!Kama umeona alofanya ni sawa je alichoamuru waziri mkubwa ambacho ni kinyume na lilichofanya hilo liMakufuli hebu comment busara ni ipi.
Na haiwezekani pia kiongozi kukurupuka na kufanya maamuzi bila kuangalia athari kwa walipa kodi. Angeweza kabisa kukaa meza moja na chama cha wasafirishaji kwa njia ya barabara nchini na kufikia muafaka huku usafirishaji wa bidhaa muhimu ukiendelea bila kuathirika.
Mara ya pili hii maamuzi yake yamebatilishwa na viongozi wake. Hasara aliyokwishaiingiza Serikali ni zaidi ya Trillioni kama tutaweka gharama za kuwakodishia nyumba (Shilingi bilioni 300 and counting) wateule mbali mbali wa Serikali ambao kwa nyadhifa zao walistahili kupewa nyumba na Serikali katika mikoa mbali mbali nchini, lakini kwa kuwa nyumba hizo zilishauzwa tena kwa bei chee basi wengi walibidi wawekwe kwenye mahoteli ya kifahari ambayo ni gharama kubwa sana kwa walipa kodi.
Pia nyumba zile kama zingeamuliwa kuuzwa kwa bei ya soko na siyo bei ya kutupa basi Serikali ingejipatia mapesa chungu nzima zaidi ya trillion (shilingi) lakini mafisadi Mkapa na mwenzie Magufuli kwa kujua kwamba kwa bei ya soko wasingeweza kuzigusa nyumba zile wakaamua kufanya ufisadi. Hasara kwa Taifa kwa maamuzi ya kukurupuka kuhifadhi samaki shilingi milioni 700, hasara ya juzi shilingi bilioni 1 na nusu na hasara nyingine mbali mbali. Kuna faida gani ya kuwa na waziri kama huyu ambaye maamuzi yake mengi yamekuwa ni mzigo kwa walipa kodi nchini na mara mbili sasa yamebatilishwa na mabosi wake!?
sijafurahi unaposema nabwabwaja, hii ni lugha ya wahuni, si lugha ya watu wazima wenye busara. sijui umri wako. sisi wengine hatujazoea kutukanwa. kama ungekuwa na busara ungefafanua zaidi nielewe pale ambapo unafikiri sijaelewa bila kutamka kuwa nabwabwaja. this is a discussion forum. hata hivyo, nilijua kuwa hapa tunajadili effects za mgomo wa malori, si hayo mengine unayosema magufuli amefanya. huko mimi siko, sikujua kuwa suala limeletwa hapa kama shambulizi dhidi ya mtu, pengine una ugomvi naye who knows; hiyo tu kuongea kama mhuni uliponijibu unaonyesha kuwa haujafikia kiwango cha watu wazima kuweza kujadili hoja, hivyo hata hii topic unaipunguza thamani kwa hadhi ya mtu aliyeileta. samahani, kwaheri.
Why this loser is still in the cabinet? :rant:
Tehe tehe tehe,ukoloni wa wenye malori na wauza mafuta. Da jamaa wanaweza kutulaza njaa wakiamua hawa! Enzi za sokoine, cjui kama angewaacha wafanye haya, huu ni uhujumu uchumi bila kutafuna maneno.
Magufuli is a hero and truly Tanzanian.Keep it up.Ni ajabu kuruhusu watu kujadiliana kuvunja sheria.Magufuli hajatunga sheria yoyote bali aliamua kuisimamia kwa manufaa ya umma.Uamuzi aliotoa PM haukuwa kwa manufaa ya umma bali kuwapendelea wenye malori ambao tunajua ni viongozi au washirika wa viongozi serikalini.Mimi natangaza kuwa naunga mkono Team Magufuli-2015 kama ataingia kwenye mbio za urais.Yeye tu mpaka sasa ndie anaonekana kuwa na uchungu na nchi yetu tukufu.
ALITUANGUSHA SANA KWA KUKUBALI NYUMBA ZETU ZIUZWE..hilo tu lakini mengine huyu jamaa anaweza mnyonge mnyongeni..haiwezekani watu wawe wanajiamulia tu kufanya ujinga kama nchi haina kiongozi na sisi tubaliki ujinga...
Huwezi kuongelea loss inayonekana kwa siku moja hadi tano kwa malori kugoma unaacha kuongelea loss inayopatikana kwenye uhalibifu wa barabara tena basi ndefu karibu nchi nzima kwa siku tano ambao ungesababishwa na hayo malori tuambie kujenga kilomita moja ya barabara ni shilingi ngapi?
sheria ya kutenganisha biashara na siasa bado???Mwakyembe anataka kutuambia hii meli iliyotia nanga recently ni kubwa kuliko ile maarufu ilikuje Enzi za ujana wetu MV KISHTOBE. Only vijana wa zamani tunaikumbuka Mv Kishtobe...
Magufuli ni msomi feki, sijajua amesomea nini na wala sitajishugulisha kujua but nilitaraji amesoma kiasi cha kutosha kujua kuwa every measuring instrument has a margin for error of 5%, weighbridge measures are among. Simply as that Magufuli hakutakiwa kubishania 5% kabisa. PIA amemkasirisha boss wake Baba Riziwani kwa kuwa wana mamia ya malory yatakayoathirika na hiyo 5%
Huwezi kuongelea loss inayonekana kwa siku moja hadi tano kwa malori kugoma unaacha kuongelea loss inayopatikana kwenye uhalibifu wa barabara tena basi ndefu karibu nchi nzima kwa siku tano ambao ungesababishwa na hayo malori tuambie kujenga kilomita moja ya barabara ni shilingi ngapi?
sheria ya kutenganisha biashara na siasa bado???
Barabara nchini zinajengwa ili kurahisisha usafiri wa bidhaa muhimu na Watanzania toka point A kwenda point B. Hakuna ajabu yoyote kwa barabara kuharibika na hili linatokea katika kila nchi duniani. Tatizo la barabara zetu kuharibika haraka mno ni kwa sababu zinajengwa katika viwango duni sana na hakuna utamaduni wa kuzifanyia matengenezo madogo madogo kila mwaka ili ziweze kudumu kwa miaka mingi bila matengenezo makubwa na ya gharama.