KERO Huduma za Airtel Tanzania ni mbovu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mamAlia

New Member
Mar 9, 2024
2
2
Habarin wadau,

Naomba mwenye uelewa anijuze nawezaje kupata haki yangu, Tarehe 04 -03-2024 nilitumia Airtel Money kufanya muamala wa TZS 150,000 kwenda tigopesa hiyo pesa kwangu ilitoka lakin haikufika kwenda ilikotumwa.

Nimejaribu kutafuta msaada mara kadhaa katika ofisi za Airtel bila mafanikio yan kinachoonekana ni kama hawawez kutatua changamoto za wateja wao kwa wakati kila ukiwasiliana nao jibu lao wanakuambia subir ndan ya saa 24 pesa yako itarudishwa kwenye simu.

Tangu nianzie kupewa hayo majibu zimeshapita siku zaid ya 8, naomben mwenye uelewa anijuze nifanyaje kupata pesa yangu au mpaka niende kulalamika TCRA.
 
Inaenda wiki ya pili sasa ninazungushwa na watoa huduma wa Airtel kuhusu pesa yangu.

Tarehe 04 -03- 2024 nilitumia Airtel money kutuma pesa Tsh 150,000 kwenda Tigopesa lakini cha kushangaza mpaka leo hii hiyo pesa haijafika na wala kwangu haijarudi.

Nimeenda katika ofisi zao mara kadhaa ila naona kama wameshindwa kunisaidia, kila nikienda wananiambia nisubiri ndani ya saa 24 pesa itarudi lakin mwisho wa siku hakuna pesa inayorudi.

Naombeni msaada nikareport wapi hii kampun ili niweze kupata pesa zangu.
 
Back
Top Bottom