how to get the ring.

Naomba kujua ka kwenye harusi ya Kana kulikua na ring. Hizi nyingine ni mbwembwe tu.
 
hahahaha, umeona eeeeh. ujue mpwa wako siogopi? sijui makofidensi gani nimepewa mie. lol

Naona Mpwa wangu.....na ukiwa huogopi kama hivyo na una qualities zote basi ujue yupo tu hakuachiii ng'o!
 
yaani nimeipenda comment yako maana naona sasa umeweza kuyatazama mahusiano kwa jicho la tatu. safi sana, najua usharuhusu moyo wako kupenda tena. lol

Umeanza.......

Si nilikuambia mimi Padri......????????......lol!!!!!!!

Kuogopa kufanya jambo kwasababu ya jana ni utoto!!!!!
 

na hiyo ndio mentality ya kizamani aliyoongelea steve ya mwanamke kusubiri kuulizwa wakati ndoa waitaka wewe! mimi nahamasisha wanawake walio katika mahusiano ya muda mrefu na wenzi wao waanze kuulizia sio mpaka waulizwe wao
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe hapa.

Lakini kuna watu kwa sababu ambazo sizijui wanaohifia kuingia ktika ndoa, labda historia ya familia zao? Labda majukumu(mtu hayuko stable kiuchumi)? Labda? Labda?

Mtu wa aina hii ukianza kumwekea timeline anaweza ondoka sababu ya hofu tu, si kwamba hakupendi, ila inakuwa kama umemtisha. Je, huoni ni bora kumwacha akakusanya mawazo yake na kuzikabili hofu zake kabla ya kuingia kwenye ndoa au wewe mwanamke kumpa presha za kuingia kwenye ndoa? Na sijui kwa nini wanawake ndio wanatakiwa waweke hii timeline.

Nina binamu yangualifunga ndoa ya kanisani, baada ya mwaka akaanza kulalamika hakuwa tayari kwa ndoa ile. Wamekaa kaa weee, akashindwa kabisa na kutoka kwenye ndoa. Kisa, mwanamke yule alimpelekesha haraka haraka wakaoana, suie tunamtania, kwani alikushikia bunduki kwenda kanisani?

Labda niulize, ni kweli wanamme wanaogopa/hawapendi kuoa?

Kama na wao wanapenda kuoa, kwa nini tuwalazimishe?

 

Kwanza Fixed Point niseme kwamba niliye naye hata sikufikiria mara mbili kumuuliza "will you marry me?" Maana hadi leo, 15yrs later (yes, you read that correct) sijawahi kujuta

Ila najiuliza what would have hapenned kama angekuwa "amechoka" na kuniuliza "utanioa lini"...ingewezekana nisiwe mimi niliye leo.
So, kwa sigle gals and searching, hii habari ya time limit kiafrika afrika haiapply sana,,,,,,, na by the way tunarudi kule kule kwenye kuwa wawazi mwanzo wa mahusiano kwamba status yenu ipi, malengo yenu yepi, nk,. ndoa itakuja tu automatikale

CC Kongosho, (sijui Zombie kamfikisha wapi masikini) snowhite gfsonwin Mtambuzi amu Paloma Filipo Kaunga Asprin MwanajamiiOne Mbu Mr Rocky Ablessed shansarie Heaven on earth
 
Last edited by a moderator:
Umeanza.......

Si nilikuambia mimi Padri......????????......lol!!!!!!!

Kuogopa kufanya jambo kwasababu ya jana ni utoto!!!!!

hata mapadri wanapenda ati. lol, safi sana Eiyer nimeona mabadiliko. ukitendwa mahusiano yaliyopita ni challenge ya kukufanya uwe imara katika mahusiano yajayo na si sababu ya kukupa hofu. tuimbe mapambio sasa.
 
Last edited by a moderator:
na hiyo ndio mentality ya kizamani aliyoongelea steve ya mwanamke kusubiri kuulizwa wakati ndoa waitaka wewe! mimi nahamasisha wanawake walio katika mahusiano ya muda mrefu na wenzi wao waanze kuulizia sio mpaka waulizwe wao
ha haaa, yaani unadhani huyo mwanaume anataka hiyo ndoa na anashindwa kukuuliza? kama hakuulizi ujue hayupo tayari na labda hana mpango wa wewe kuwa mkewe. Ni sawa unaweza kuuliza hatma ya mahusiano kama tu upo tayari kutoka, na siyo kuulizia pete.
 

maisha ni kupanga, wazungu wanasema if you fail to plan you plan to fail... kila mtu ana mipango yake, na huwezi kukurupuka tu. miapango ya kiuchumi waweza jiamulia lakini inapokuja kwenye mahusiano lazma mwenzi wako ajue plans zako maana zinamuhusu, kama plans zako na zake haziendani hakuna kupotezeana muda. mwanamke anataka ndoa after 2 years na wewe haupo tayari basi ajue hilo, hivo hivo kwa mwanaume. mipango ya kimahusiano ni ya mawili na si kusema unamsubiria yeye aseme, una haki pia ya kuongea matarajio yako. bila kuongea utakuwa kwenye mahusiano ambayo huyafurahii.
 
Ndo maana hapo juu niliweka kwenye mabano kuwa mimi siyo mfano mzuri sana....
ni kwa sababu niliulizwa kabla hata sija-settle kwenye mahusiano, yaani mimi naona nayaanza mahusiano tu naulizwa kuolewa, na juzi tu nimeulizwa kuolewa naye tena.....
siamini kwenye kum-push mwanaume akuoe (labda sababu sijawahi kuwa desperate kuolewa) kama kuolewa kunakuja tu. na kweli naamini kama mwanaume anakuhitaji wewe kuwa mwenzi wake wala hasubiri wewe umwulize, atakuuliza tu.
 
kwa hali hii ndo maana kila mwanaume anaepropose ndoa wanawake wengi huwa wanasema tu yes! sio kila mtu anafaa kuwa mume ! hakuna haja ya kujichosha ujue! ndo maana ndoa nyingi siku hizi chali...watu hata hawajui kwanini wanaolewa ujue! sijui harusi ..sijui kuonekana hata sijui ...
 
ha haaa, yaani unadhani huyo mwanaume anataka hiyo ndoa na anashindwa kukuuliza? kama hakuulizi ujue hayupo tayari na labda hana mpango wa wewe kuwa mkewe. Ni sawa unaweza kuuliza hatma ya mahusiano kama tu upo tayari kutoka, na siyo kuulizia pete.

ni kwanini mwanamke asiulize? ni hofu au nini? kwanini unahisi mwanaume ndio anatakiwa kuulizia ndoa?
 
Ha ha ha, mnaweza kuulizana mwanzoni na kuwekana sawa kabisa.

Ila moyo wa binadamu msaliti, mnaweza fika njiani mioyo ikawasaliti aidha wote wawili au mmoja wao. Kama kuna mawasiliano ya kutosha ni bora kuongea na kuwekana sawa mkajua nini cha kuamua kuanzia hapo. Kama mnabadili uelekeo wa mahusiano yenu wote wawili? Au kama mnaahirisha ili msijeumizana zaidi kwa mmoja wenu?

Ndio maana nasema ni kompliketedi kuja na formula.

Nikupe story na mtu wangu wa karibu, japo yeye hajui chimbuko la ndoa yake. Kijana alitongoza msichana mahali, akakuta msichana ana mwanamme wake,. Yule kijana kwa hasira akaenda tongoza mpwa ya yule mwanamme wa msichana aliyekuwa anampenda kama kumkomoa huyo mwanamme aliyemnyang'anya tonge mdomoni. Kweli akampata mpwa, akamlamba kama mara kadhaa. Ile anataka kumtema mpwa, na alikuwa ndio ana miaka 17 tayari ana mimba na mpwa ni wife material. Hadi leo wana watoto watatu.
Hawakuwa na mawasiliano, hakukuwa na nia njema to start with, but wameishia kuvishana pete kanisani.

Lakini hii ya kumwekea CCM timeline ni kujichubua kifua kwa kokoto.

 
Daaahhh mtoa mada umenifanya nikumbuke historia 2 nyuma za kweli kabisa
  1. Incident ya kwanza jamaa alikuwa na girlfriend one day was friday akaenda mchukua alimpigia demu ashuke chuni kabisa, demu akawa ready ila bado room ili jamaa akifika tuu ashuke waondoke. Hee!! ile jamaa kafika kapata parking akampigia demu uko wapi akamwambia nakuja hapo niko kwenye ngazi nashuka simu ikakatwa demu kushuka chini jamaa kumbe alishawasha gari na kuondoka hee demu kufika chini anampigia simu jamaa jamaa kamwambia nimeshaondoka ukitaka kuja kwangu panda basi uje. Looh demu akasema yaani hapa sijaolewa anashindwa kunisubiri dakika 3 jee nikiolewa nae si ndo atakataa kuongozana na mie barabarani isiwe tabu demu akaamua kujitoa kwenye mahusiano ila kabla ya kuondoka akamfata jamaa ili mpashe na kumpa vidonge vyake. Alipofika akamwambia ulichokifanya ni kibaya na sikupendezewa nacho bora uhusiano wetu uishie hapa kwa sababu unaonesha huwezi kunisubiri hata dakika 2 ukinioa si ndo kabisaa. Kwa taarifa yako usifikiri nina shida ya kuolewa na wewe, si lazima nikiachana na wewe ntaolewa na wengine jamaa akaona demu kastukia dili kumbe hakuwa na mpango nae akaomba msamaha ila demu akammwaga. So hapo ni bora kusoma alama za nyakati.
  2. Issue ya pili ilitokea kwamba demu alikuwa na boyfriend wake ambae ndo wanaanza chuo wote wako chuo mwaka wa kwanza. Kama kawa katika maongezi demu akawa anamchombeza huu uhusiano wetu lini utafika kwa wazazi? Jamaa alikuwa anasomea udaktari ila ndo kwanza anaanza level ya medical assistant ndo aende Muhimbili kupata degree. Jamaa alikuwa mkweli hakumdanganya demu akamwambia mie kuoa hadi nipate dregree na niwe na kazi inilipe mshahara mzuri au niwe na hospitali yangu kama si dispensary au pharmacy yangu. LOOOH demu akapiga mahesabu hapo yuko chuo mwaka wa kwanza, hadi jamaa amalize medical assistant bila kufeli au kurudia mwaka ni miaka 3 na akimaliza aende Muhimbili udaktari akifaulu bila kurudia mwaka ni miaka mingine saba na hadi aajiriwe mshahara mzuri au awe na hospitali, dispensary au pharmacy yake ni miaka mingine 3 kwa kukadiria jumla miaka 13 tangu hapo looh wakati huo demu alikuwa na miaka 21 ukijumlisha hiyo miaka 13 atakuwa na miaka 34 hapo ujue hakujaytokea tatizo lolote na iwapo jamaa ni kipanga yaani hatarudia mwaka au kukwama kufungua hosp au disp. yake demu akamwambia asante sana kuniambia ukweli, kweli nakupenda tutakuwa tunabanjuana tukimisiana ila naanza mapema maana sitaweza kukuvumilia hadi umalize. So ni vema kuwekana wazi kuliko kuzeeshana halafu mtu anakuja kuoa mwingine baada ya miaka yote hiyo. Jamaa hadi leo hajaoa ila amezaa watoto 2 na wadada tofauti, alishamaliza udaktari na kaajiriwa na haeleweki ataoa lini. Hivyo wadada ukingijea mkaka akuambie tuoane kesho utadoda na kuchina better ask mapema ujue mchakato.
Kila la kheri kwa wanaotarajia kuolewa/kuoa.

Ni habari iliyowakumba wadada wawili tofauti ninaowafahamu.
 
ni kwanini mwanamke asiulize? ni hofu au nini? kwanini unahisi mwanaume ndio anatakiwa kuulizia ndoa?
ni mazoea tu....
tumezoea yeye ndo ana-propose, analipa mahari, anakuja kukuposa kwa wazazi wako.
sasa mwanamke akianza ku-propose (hiyo ndo maana halisi ya kuulizia ndoa), then utaenda kwa wazazi wake kumposa? na kumlipia mahari? au utaishia kwenye kupropose tu
 
Husyn, mwanamme anayetaka kukuoa hata kama hajasema unakuwa unamjua tu. Hat kama hajawahi sema, na mwanamme anayekuchukulia poa unamjua tu.

Sema wanawake sometimes hatukubali matokeo, unajua kabisa huyu mwanamme kwake wewe ni kipozeo, unataka umfosi akutoe kutoka kwenye kipozeo hadi uwa mke. Wapo wanaofanikiwa, wapo ambao hawafanikiwi kuwalazimisha.

na hiyo ndio mentality ya kizamani aliyoongelea steve ya mwanamke kusubiri kuulizwa wakati ndoa waitaka wewe! mimi nahamasisha wanawake walio katika mahusiano ya muda mrefu na wenzi wao waanze kuulizia sio mpaka waulizwe wao
 
Unaweza kumuuliza mtu amabaye una hakika anakupenda au mtu amabaye anaonesha karidhika na wewe. Lakini si kila husiano unaweza kuuliza.

ni kwanini mwanamke asiulize? ni hofu au nini? kwanini unahisi mwanaume ndio anatakiwa kuulizia ndoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…