Aisee
Husninyo hii ishu ya kuolewa sijui kuvalishwa pete is not as simple as we all wish it was. It's more complex than that.
Yani unaweza ukaipata hiyo pete na isimaanishe kwamba UNATHAMINIWA, UNAPENDWA, UNAJALIWA n.k Mwenzio anaweza akawa anataka tu housemaid who can perfoms 'EXTRA DUTIES' whenever needed na asiyedai mshahara. Utafanya kazi kama slave, utazaa na kulea weeeee mpaka uso ukushuke wakati mwenzio ambae hajavikwa pete ndio anaekula goodtime. Stress zote za jamaa uta-deal nazo wewe, uchovu wake na matatizo yote ya kifedha na kiafya yatakuhusu wewe na pete yako kidoleni.
Nnachojaribu kusema ni kwamba watu wanaoa na kuolewa kwasababu za kila aina. Vile vile watu hawaoi na kuolewa kwasababu za kila aina. Unaweza ukawa na mtu asikuvishe pete lakini akawa anakuthamini, anakujali na kukupenda zaidi ya ambae anataka kukuvalisha pete kwasababu pete sio moyo useme ndo anakuwa amekukabidhi utembee nao. Pete ni kama mkufu tu, unaweza kuvalishwa ili utumike bila kuhisi/kuona unatumika.
Jambo la muhimu ni kuomba umpate atakaekuthamini with or without the ring. Usiweke thamani kubwa kwenye pete, weka thamani kubwa kwenye matendo yake na namna alivyokuweka kwenye maisha yake. Kama ana nia ya kukupa hiyo pete atakupa tu bila hata kuiulizia au hata kuitaka. Besides, kuiomba kunapunguza ile hisia ya wewe mwanamke kuombwa uwe mke wa fulani. Acha yeye mwenyewe akupe, mwenyewe aonyeshe nia ya kukuoa usije ukawa unalazimisha.
Ila kama mtu anataka pete alimradi pete . .mwambie tu "Ebwana ehhhh..mi nshachoka kuvaa na kuonyesha 'cocktail ring' tu kila siku..nataka na ya ndoa sasa, tusichoshane bila kuweka alama kidoleni".