how to get the ring.

how to get the ring.

................. jana nilikuwa nachungulia kitabu cha steve harvey cha ACT LIKE A LADY THINK LIKE A MAN.ni kitabu kizuri sana ila sie wengine uvivu wa kusoma vitabu tunakosa mengi.

steve anasema wanaume wanajua kabisa kuwa wanawake wanataka ndoa. wanawake wanatakiwa kujiondoa katika mentality ya kizamani ya kusubiri mpaka mwanaume atangaze ndoa. tunatakiwa kuset timeline for the ring, mwambie mpenzi wako unachotaka na matarajio yako. haina maana kuwa katika mahusiano ambayo hayakupeleki kule unataka kwenda, kwa case hiyo tafuta mtu ambaye mna direction moja. wanawake wengi huwa wanashindwa kufunguka kwa wapenzi wao kuhusu ndoa vile wanaogopa au wanahisi ni vigumu lakini ni ngumu zaidi kudate na mtu mpaka mnazaa watoto na hana mpango wa ndoa (wakati wewe intention yako ni kuwin pete).

muoneshe mwanaume thamani yako na asikutumie kama vile amekodi nyumba mwisho wa siku akipata sehemu nzuri anahamia huko. set standards zako na angalia kama anafit huko.

"the
number one cause of failure in this country is the fear of failure.
Fear paralyzes you from taking action. Don’t be afraid to lose
him, because if a man truly loves you, he’s not going
anywhere"

tujadilini jamani, tuanze kuset timeline au twende na zama zetu za mwaka 47 za kusubiri kuambiwa.lol.

nawasilisha.

wasilisho limekubalika... superb thread
 
Aisee Husninyo hii ishu ya kuolewa sijui kuvalishwa pete is not as simple as we all wish it was. It's more complex than that.

Yani unaweza ukaipata hiyo pete na isimaanishe kwamba UNATHAMINIWA, UNAPENDWA, UNAJALIWA n.k Mwenzio anaweza akawa anataka tu housemaid who can perfoms 'EXTRA DUTIES' whenever needed na asiyedai mshahara. Utafanya kazi kama slave, utazaa na kulea weeeee mpaka uso ukushuke wakati mwenzio ambae hajavikwa pete ndio anaekula goodtime. Stress zote za jamaa uta-deal nazo wewe, uchovu wake na matatizo yote ya kifedha na kiafya yatakuhusu wewe na pete yako kidoleni.

Nnachojaribu kusema ni kwamba watu wanaoa na kuolewa kwasababu za kila aina. Vile vile watu hawaoi na kuolewa kwasababu za kila aina. Unaweza ukawa na mtu asikuvishe pete lakini akawa anakuthamini, anakujali na kukupenda zaidi ya ambae anataka kukuvalisha pete kwasababu pete sio moyo useme ndo anakuwa amekukabidhi utembee nao. Pete ni kama mkufu tu, unaweza kuvalishwa ili utumike bila kuhisi/kuona unatumika.

Jambo la muhimu ni kuomba umpate atakaekuthamini with or without the ring. Usiweke thamani kubwa kwenye pete, weka thamani kubwa kwenye matendo yake na namna alivyokuweka kwenye maisha yake. Kama ana nia ya kukupa hiyo pete atakupa tu bila hata kuiulizia au hata kuitaka. Besides, kuiomba kunapunguza ile hisia ya wewe mwanamke kuombwa uwe mke wa fulani. Acha yeye mwenyewe akupe, mwenyewe aonyeshe nia ya kukuoa usije ukawa unalazimisha.

Ila kama mtu anataka pete alimradi pete . .mwambie tu "Ebwana ehhhh..mi nshachoka kuvaa na kuonyesha 'cocktail ring' tu kila siku..nataka na ya ndoa sasa, tusichoshane bila kuweka alama kidoleni".

weeeell said dr... unaweza vshwa ring na usiwekwe moyon tchaaa. Mungu mwenywe ajua jmn.
 
Last edited by a moderator:
Mie hata sijui mihogo yangu ya kukaanga huwa bomba sana pamoja na chumvi na pilipili ya unga najikumbushia enzi za primary na secondary au kama si mihogo basi sambusa za nyama iliyochanganywa na viazi. Sijui hizi chips dume ni aje zinakuwa tamu sana labda wananyunyizia urozi lol!!!! ili kuvutia wateja.

Wakati mwingine kwenda huko ngumu rafiki hasa sisi tuliokua hatuioni nyota ya kijani . Manake walipokua wakitangaza nyota ya kijani hiyooo sisi tulikua tunaona za blue tu. Ila ni kweli kuna maraha yake ya kwenda hukooooo. Umenikumbusha mihogo ya kukaanga na juice ya ukwaju ngoja nkautafute nitengeneze. Huwa najiuliza kwanini chipsi dume ukinunua ina ladha kuliko ya kukaanga home???????
 
haaa mpaka nami nimepatwa na hamu ya hio mihogo ya kukaanga na achari ya mbilimbi....
 
Mie hata sijui mihogo yangu ya kukaanga huwa bomba sana pamoja na chumvi na pilipili ya unga najikumbushia enzi za primary na secondary au kama si mihogo basi sambusa za nyama iliyochanganywa na viazi. Sijui hizi chips dume ni aje zinakuwa tamu sana labda wananyunyizia urozi lol!!!! ili kuvutia wateja.
week end hii nitajaribu kuiandaa ama kweli mambo ya zamani yalikua poa sana. Watu mnajazana kwa kumuuza mihogo a.k.a chipsi dume , viazi havikua popular na walaji wake walikua wachache sana . Nakumbuka pale kibasila secondary nje ya michongoma karibu na hosteli kuna muuza chipsi dume alikuwepo pale.
 
Nimejiuliza kwa nini watu wanavishana pete na kuoana...

Jibu rahisi ni maandiko ya dini nyingi...lakini hiyo si sababu kubwa kwa kuwa wengi wanaoana lakini si watu wa dini kihivyo...wanaenda makanisani na misikitini kama tradition tu lakini siyo kilicho wapa motisha kuoana.

Kila mtu labda ajibu kwa experience yake maana sababu ni nyingi za kufikirika na za kweli inategemea kama unamzungumzia mtu au unajizungumzia

Mimi niliolewa kwa sababu mume wangu alikuwa ananipenda sana na aliogopa kunipoteza kwa wengine kama asingenioa.

Kama wanawake wengine nilipenda kuoelewa...lakini mwenye kuamua ni mwanaume...nasema alinioa out of wasiwasi kwa sababu nilipopata kazi sehemu fulani tu nikamuona hana amani...na haikupita mwezi alienda kujitambulisha officially kwa wazazi na ndani ya muda mfupi tukaoana.

Na hii ni natural ...kama unapenda kitu kwa dhati na unajua kuna njia ya kujihakikishia kuwa chako kwa nini usifanye hivyo...ukiona mtu hatangazi nia jua haoni kama yuko kwenye danger zone...ana uhakika kuwa hana mshindani. Otherwise he is still searching.

Na ndio maana wanawake ambao ni ving'ang'anizi (a.k.a pushy) hawaolewagi japo wanaweza kudumu kwenye uhusiano...unajua kwa nini? kwa sababu mwanaume anajua kwake umefika...

Hii inahusu hata hao wanaoweka time limit...wataweka time limit kwenye kila uhusiano na mwisho wa siku watajikuta wanaongeza number ya lovers lakini hakuna ndoa

Ndio maana utasikia ukitaka kuolewa behave as if you don't care. Hiyo inampa kidume wasiwasi kwamba sooner or late atatemwa
 
Timeline my foot, utaolewa jumamosi na kuachika jumatatu na mavitabu yenuu
 
Jaribu hakikisha mihogo unayonunua ni mizuri ukumbuke Enzi za Judy Boucher hahahahah lol! Mie nilikuwa na mob yangu ya watu 10 tunashuka pale mnazi mmoja karibu na hospital pembeni kuna jamaa alikuwa na kanga mihogo mitamu sana basi tukifika tunamwambia usimuuzie mtu mwingine waambie mihogo yote imenunuliwa na sisi hahahahah lol! tunakula kwa raha zetu mpaka tunatosheka na jamaa alikuwa akittuona tu anafurahia sana maana anajua tulikuwa tunampa biashara nzuri. Haya kila la heri katika kutengeneza mihogo yako week end hii itoke bomba ila angalia usinogewe tu 🙂🙂

week end hii nitajaribu kuiandaa ama kweli mambo ya zamani yalikua poa sana. Watu mnajazana kwa kumuuza mihogo a.k.a chipsi dume , viazi havikua popular na walaji wake walikua wachache sana . Nakumbuka pale kibasila secondary nje ya michongoma karibu na hosteli kuna muuza chipsi dume alikuwepo pale.
 
@Ablessed hiyo link aliyokupa pacha wako ni bomba unaangalia bila tatizo lolote lile ila kilichoniudhi ni kwamba kila baada ya dakika 13 nadhani mpaka 15 inabidi uclick kwenye namba inayofuata (1,2,3.....) ili kuweza kuendelea na movie yako tena unaona latest movies. Also it is very important to have unlimited internet usage, vinginevyo unaweza kuletewa bill itabidi ujifiche....kwa Kiswahili cha MUJINI wanasema itakula kwako.

Wakati mwingine kwenda huko ngumu rafiki hasa sisi tuliokua hatuioni nyota ya kijani . Manake walipokua wakitangaza nyota ya kijani hiyooo sisi tulikua tunaona za blue tu. Ila ni kweli kuna maraha yake ya kwenda hukooooo. Umenikumbusha mihogo ya kukaanga na juice ya ukwaju ngoja nkautafute nitengeneze. Huwa najiuliza kwanini chipsi dume ukinunua ina ladha kuliko ya kukaanga home???????
 
Kwa hiyo Kongosho kama nimekusoma vizuri crritical analysis yako, kuna aina nyingi za mahusiano ya kingono kati ya mwanamke na mwanaume......mengine ya kindoa na mengine sio ya kindoa,.,,,I mean ya timeline na yasiyo ya timeline, ya good time na yasiyo ya god time ila yanaelekea kwenye uwife na ozbend material (@paloma upo)

Sasa basi mtuwacheeeeee.......maaana wanawake wajue pia kuwa sio kila mwanaume anapokutokea anataka NDOA na wewe ....hapana....au RING sijui...kwani ulingoni apo?

CC Asprin cacico Kongosho Fixed Point AshaDii
morning shemeji! mzima?
 
................. jana nilikuwa nachungulia kitabu cha steve harvey cha ACT LIKE A LADY THINK LIKE A MAN.

"the
number one cause of failure in this country is the fear of failure.
Fear paralyzes you from taking action. Don’t be afraid to lose
him, because if a man truly loves you, he’s not going
anywhere"
Wasiwasi huu unahusu wananchi wa nchi gani, ile ya mwandishi wa kitabu au Tanzania.
 
Nimejiuliza kwa nini watu wanavishana pete na kuoana...

Jibu rahisi ni maandiko ya dini nyingi...lakini hiyo si sababu kubwa kwa kuwa wengi wanaoana lakini si watu wa dini kihivyo...wanaenda makanisani na misikitini kama tradition tu lakini siyo kilicho wapa motisha kuoana.

Kila mtu labda ajibu kwa experience yake maana sababu ni nyingi za kufikirika na za kweli inategemea kama unamzungumzia mtu au unajizungumzia

Mimi niliolewa kwa sababu mume wangu alikuwa ananipenda sana na aliogopa kunipoteza kwa wengine kama asingenioa.

Kama wanawake wengine nilipenda kuoelewa...lakini mwenye kuamua ni mwanaume...nasema alinioa out of wasiwasi kwa sababu nilipopata kazi sehemu fulani tu nikamuona hana amani...na haikupita mwezi alienda kujitambulisha officially kwa wazazi na ndani ya muda mfupi tukaoana.

Na hii ni natural ...kama unapenda kitu kwa dhati na unajua kuna njia ya kujihakikishia kuwa chako kwa nini usifanye hivyo...ukiona mtu hatangazi nia jua haoni kama yuko kwenye danger zone...ana uhakika kuwa hana mshindani. Otherwise he is still searching.

Na ndio maana wanawake ambao ni ving'ang'anizi (a.k.a pushy) hawaolewagi japo wanaweza kudumu kwenye uhusiano...unajua kwa nini? kwa sababu mwanaume anajua kwake umefika...

Hii inahusu hata hao wanaoweka time limit...wataweka time limit kwenye kila uhusiano na mwisho wa siku watajikuta wanaongeza number ya lovers lakini hakuna ndoa

Ndio maana utasikia ukitaka kuolewa behave as if you don't care. Hiyo inampa kidume wasiwasi kwamba sooner or late atatemwa

kweli nyumba kubwa, kama mwanaume anajua thamani ya alichonacho na hataki kukipoteza atajikuta ametangaza ndoa tu mwenyewe.. tatizo mapenzi ya sahvi usanii mwingi, natamani ningekuwa nimezaliwa mwaka 47 mie. lol
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ila kwa upande mwengine (positive side) hio time limit inaweza iwe kipimo cha kiasi gani mtu anakuhitaji na una umuhimu gani katika maisha yake.Kwasababu kama ana mapenzi ya dhati kwako hatukubali kukupoteza kirahisi bali atatekeleza hayo matakwa yako!!

swadaktaaa!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom