How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

daah kiswahili kinahitajika, yaani unataka nianze kutafuta kamusi sasa hivi? Ila kiufupi maendeleo ni kama kujenga nyumba lazima uanze na msingi kwanza, na msingi ni pamoja na miundombinu. Kwa sasa vijana tulime tu, kama tukikosa ajira za kuajiriwa au kujiajiri. Ila baadae miundombinu hii itatupa ajira sina shaka sana na hilo. Hata hivyo watu milion 50 hatuwez wote tuka ajiriwa, jamani ajira iko shambani tuliambiwa toka tulivokuwa shule ya msingi, na shambani sio lazima tu tulime hata kufuga kuku pia ni kilimo.
 
Kuwepo na uwazi basi, ili kila mmoja aone faida iletwayo na ndege zetu. Kenya airways pamoja na kuwana routes kibao za kimataifa bado haifanyi faida. Sisi tuna muujiza gani kwa route zetu hizi za ndani? Walipa Kodi tutabebeshwa mzigo mzito was kuhudumia hizi ndege _ let us wait and see. Mbaya zaidi tutakuja kuyasikia haya utawala utakaopita Kama ambavyo leo tunavyosikia madudu ya serikali zilizopita na wakati huo tutakuja tumeshapoteza pesa nyingi Kama mradi wa katiba mpya.
 
Natabiri usiri kwenye kukagua vitabu utaendelea, na shirika litabebwa kwa hela nyingi za walipakodi ambazo hata kwenye bajeti hazimo.

Ili mradi tu watu waseme "Magufuli Oyeee, CCM Oyee".
 

Ukweli ni kwamba aviation industry ina changamoto nyingi tu.

Hata hayo mashirika makubwa nayo yana changamoto nyingi.

Mapema mwaka huu Singapore Airlines iliingia hasara.

Mwaka jana walianza mageuzi ya kupunguza gharama za uendeshaji wa shirika ili waweze kushindana vizuri na washindani wake kutoka Mashariki ya Kati na kwingineko.

Kuogopa kufanya jambo kwa sababu lina changamoto ni defeatist attitude.

Changamoto ni sehemu ya maisha ya kila siku.

Hazikwepeki.

Hivyo hakuna biashara isiyo na changamoto.

 
Mkuu kwa mtanzamo wangu cha kwanza kinatakiwa elimu bora,sasa miundombinu plus elimu bure ya magufuli,utapateje ajira bila ujuzi na maarifa kichwani?
 
Suala si kuogopa kufanya biashara kwa sababu ya changamoto.

Suala ni, serikali iliyoboronga biashara ya korosho imejipanga vipi kuhakikisha haitulishi hasara katika biashara complex sana ya usafiri wa anga?

Mbona haitaki hata vitabu vya shirika vikaguliwe?

Mbona shirika linapelekwa kisiasa, kitu ambacho magwiji wa biashara wameasa ni kibaya na kinachangia sana hasara?
 

Fair points.

Mimi naunga mkono shirika kuendeshwa kiuweledi wa kibiashara.

Kwa maneno mengine, wanasiasa wawaache wataalamu waliendeshe kitaalamu.

Kwa hilo wala sina tatizo kabisa.
 

Mkuu
KQ inafanya loss sababu ya ufisadi wa wakenya.
Kuhusu faida nyingine kacheck KQ jinsi ilivyo boost utalii wa Kenya. Angalia haya mambo kwa three dimensions yani ukija ku jumlisha jinsi KQ ilivyo boost uchumi wa Kenya wala huwezi sema inafanya loss KQ.

Kuhusu ufisadi, ufisadi wa awamu zilizopita ulijulikana kwa wakati huo, ndiyo maana mawaziri wa wakati huo waliachia ngazi. Sidhani ni haki kusema ufisadi wa wakati huo umejulikana awamu hii, yani Richmond, IPTL, meremeta, Buzwag nk wewe umezifahamu awamu ya tano?
 
Kila biashara inachangamoto , hata kufuga kuku wanachangamoto na watu kila siku wanakula loss. Hata kulima watu kila siku wanakula hasara na kilimo hawavuni kitu. Hata viwanda kila siku watu wanafunga viwanda kwa kula loss hata kusoma watu kila siku wana fail na ku disco. Lakini pamoja na hayo, ni kwamba watu bado wanafuga kuku, watu bado wanalima, watu bado wanafungua viwanda vipya , bado wanaenda madarasa yaleyale wengine wengi walio fail humohumo wanafaulu.

Kufikiria mtu fulani kafail na wewe unaishikia bango ni old stone way of thinking, lame thinking for lame people.
 
Mkuu kwa mtanzamo wangu cha kwanza kinatakiwa elimu bora,sasa miundombinu plus elimu bure ya magufuli,utapateje ajira bila ujuzi na maarifa kichwani?
kweli lakini pia elimu sio ya kwanza sanaa kuliko afya. Kwasasa wananchi wajue tu kusoma sio kuajiriwa, watoto wetu wajue kuwa kusoma ni kuongeza maarifa japo lile somo la 'stadi za kazi' mashuleni lilidharaulika miaka ya katikati lakini lilikuwa muhimu sana lile kutiliwa mkazo. Ni maoni yangu tu ndugu.
 
Mkuu mimi sizungumzii elimu hii ya bure ya magufuli ambayo inalenga kumpa mtu cheti badala ya ujuzi na maarifa ,bali nazungumzia elimu bora na si hii bora elimu wanayopewa watoto wa wanyonge,Elimu kwa maana ya ujuzi na maarifa ni muhimu zaidi kuliko afya and any anything ease,watu wakipata elimu nzuri hata uwezo wao wa kujikinga na magonjwa mbalimbali ni mkubwa hivyo kupunguza uhitaji wa huduma za afya
 

Kama huelewi kaa kimya.
CHADEMA mwaka 2015 walikuwa na Ilani inayosema ELIMU,ELIMU,ELIMU. Sasa angalia kile CCM wanachofanya kwenye Elimu inayoitwa ya BURE...!!



Hii ndiyo hali ya ELIMU inayotolewa bure na Serikali ya Magufuli. Badala ya kuwekeza zaidi kwenye Elimu Magufuli na CCM yao wananunua midege na kuji-mwambafy kama vile Zuzu kaokota embe chini ya mnazi...!!! Ukiangalia hiyo midege ukalinganisha na hali ya hizi shule unaweza kulia machozi...!!!Lakini hapa kuna jitu linatamba na kukebehi Watu ati waendeleee KUFYATUA WATOTO WATASOMA BURE.....Shame on you!
 

Attachments

  • 1572404544673.png
    16.6 KB · Views: 14
Basi sawa nimekupata. Ila kiugomvi tu hakuna elimu bora Afrika. Kwa sasa, Afrika tuache tu tusome kufahamu sio kuelewa.
 
Tatizo lako ni moja tu, mzalendo mwenzangu.....

Wewe una pure CCM hater. Hoja zako zote unajenga kupitia magufuli na CCM, hama ungekua hauna ushabiki na chama chochote na hakika maono yako yangekua tufauti kidogo.
 
Na anayezikubali changamoto huyo ni tajiri mtarajiwa. Warusi wanao msemo usemao asiye tayari kuhatarisha maisha yake basi huyo hatakuja kunywa champagne.
 
Upuuzi mtupu, kwa hiyo hizo shule ndio kielelezo cha Tanzania nzima!!, huu ni utoto wa kule facebook na whatsapp.
 
Kenya wenzetu wako very strategic serikali inamiliki just potion ya hisa za shirika, hisa nyingi zinamilikiwa na watu binafsi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…