How GOD is smart

Upo sahihi
 
Tupe andiko linalosema Mungu yupo sirini
 
duuuh.
 
Huyo mungu sio ndio alioleta gharika na kuuwa watu duniani enzi za nuhu?

Sasa anakuaje smart kama anauwa watu kama Alshabab?
Huyu mungu ni undefined sana, hana mfumo thabiti wa kuaminika

Alisema usiue katka amri zake lakini yeye ndiye aliyekua wa kwanza kuivunja amri hii (kweli nimeamini sheria zimewekwa ili zivunjwe)

Alisema usitamani wala hupaswi kua na wivu, yote hayo ni makatazo ambayo sio mema lakini yeye mwenyewe ana wivu hataki watu waabudu miungu mingine at the same he claimed to gave us a freewill WTF? Sasa hapo mbona anauingilia uhuru aliotupa je huo ni uhuru au utumwa?



Sent using unknown device
 
Hivi nadharia ya nyoka na tunda la mti wa katikati si sawa na nyoka ni tupu ya kiume halafu tunda la mti wa katikati ni tupu ya kike?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nadharia ya nyoka na mti wa kati kati imekua translated tofauti tofauti na imechangia sana mfumuko wa makanisa mengi. Lakini ukitumia rules za bible wamesema hutakiwi kuongeza kitu wala kupunguza kilichomo mle ndani all you need ni kusoma tu nakuya hifadhi kichwani, kwaiyo ukitafsiri neno litakufanya uongeze neno ambapo utakua umekiuka sheria za bible



Sent using unknown device
 
Hitler aliua watu wengi na vitabu vilivyoandika stor yake vimemsema kua ni gaidi, hata kama kuna mema alishawahi kuyafanya hayajapewa priority kama ubaya wake

Osama nae aliua watu pamoja na kulipua lile jengo pale usa nae yupo kwenye orodha ya magaidi waliotikisa dunia

Ajabu

Mungu kaua watu wengi sana tena kwa mauaji ya kikatili na tena kuthibitisha hilo kua mchakato wake wa kuendeleza ukatili haujafika kikomo ame ahidi jehanamu ya milele ambayo ina moto uwakao milele. Lakini vitabu vilivyoandika habari zake zimemuita kua ni mwenye upendo wote, mwenye huruma na anaesamehe

Sent using unknown device
 
Katoa adhabu kwa wale wote walioenda kinyume na taratibu zake.
Isitoshe kabla ya kuangamiza kile kizazi cha kabla ya gharika aliwapa mda wa miaka 120 ya kutubia na kurudi kwenye njia za MUNGU.KAtika kipindi hichi NUHU na METHUSHELA walikuwa wakihubiri habari njema na kuwaambia Watu watubu vinginevyo gharika itakuja.Ika hawakusikia.

Kwa hiyo walipata walichostaili.Hakuna ukatili hapo.Walionywa wakagoma.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwa kama soul inaona ila haionwi je wamewezaje kujua jinsia ya huyo mungu bila kuona?

Sent using unknown device
 
Kwani jinsia ya MUNGU MWENYEZI Ni ipi?Mimi siijui. Nisaidie Kama unaijua.

Sent using Jamii Forums mobile app
He created the universe

Hapo washa mdescribe kwa jinsia ya kiume

Ukija kwenye zile sala za kwa jina la baba na la mwana na la roho, taali hapo jinsia yake ishakua revealed so fact yakusema kua haonekaniki inakua na ukakasi kuikubali

Sent using unknown device
 
Mkuu sidhani Kama walimaanisha kuwa yeye Ni mwanamme.
Ninachoolewa Ni kwamba hicho kiwakilishi(he) kimetumika kumpa sifa.Wangeweza kutumia (she) lakini he imetumika maana mwanamme Ni mkuu kuliko mwanamke.Sasa hakuna kiwakilishi kingine kikuu zaidi ya hicho katika kuonyesha heshima kwa MUNGU MWENYEZI.Kama kingekuwepo Basi kingeweza kutumika.

Neno baba pia linatumika wakati mwingine tena Sana tu lakini sio kigezo kuwa MUNGU Ni mwanamme.Ni swala la kuonyesha heshima.
Jinsia zote kaziumba MUNGU na zote zinaheshimika lakini yakiume ndio Chanzo Cha ya kike na ndio maana inatumika Sana.
Sijawahi kuona andiko lolote linaloonyesha kuwa MUNGU MWENYEZI Ni wa jinsia gani.

Hivyo ndivyo ninavyoelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwanza ni vizuri tujue ni Mungu mwenye sifa zipi aliyekua akiangamiza hivyo vizazi

Mungu mjuzi wa yote, kwa maana hakuna jambo geni kwake, kwa sifa hii kama ndio anayo huyo mungu basi hakufanya haki. Kama aliwapa miaka 120 ili wajirudi inaonesha wazi kua hakuweza kujua kua watakaidi kutubia





Sent using unknown device
 

Neno baba hutumika kuwakilisha jinsia ya kiume kinyume na hapo ni tusi au dhihaka.

Neno baba halitumiki kama heshima kwasababu lishajitosheleza kulingana na umri wa mwanaume, hapa namaanisha kua sio kila mwenye jinsia ya kiume ni baba ila kila baba ni lazima awe mwanaume

Mimi namuheshimu mama yangu lakini nikimuita baba atamaind na ni haki yake kwasababu nitakua nimemkosea heshima

Sitegemei wewe ukamuita mama yako baba halafu akakuuliza unamaanisha nini ukamjibu kua hiyo ni heshima na yeye akaridhika

Sent using unknown device
 
MUNGU anajua Kila kitu.Lakini hapendi tuwe na mwisho mbaya.Anajua kabisa sisi tunafanya makosa na ndio maana anatupa nafasi ya KUTUBU ili atusamehe.Na ndio Alichokitaka kwa kizazi cha kwanza enzi za NUHU.Lakini waligoma na baadae wakaadhibiwa.

Wapo walifuata maelekezo ya kina Nuhu na Methushela wakatubu na kusamehewa.Hawa walikufa vifo vya kawaida kabla hata ya gharika.
Methushela mwenyewe alikufa miaka michache kabla ya gharika.
Waliobaki hawakutaka kusikia.Kipindi Cha Toba kikaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okay mkuu.
Umeeleza vizuri.
Cha kufanya Ni kwamba wewe mtukuze MUNGU MWENYEZI kwa namna yoyote ile unayoijua bill kumkejeli au kumdhihaki au kumtukana.Ukitaka kutumia kiwakilishi chochote (He or She) ilimradi tu unampa ile heshima kuu mi naona sawa tu.Lakini haitamaanisha kuwa MUNGU MWENYEZI Ni kike au wa kiume.
Hivyo viwakilishi vinatumika badala ya kutaja majina yake tu.

Mimi siijui jinsia ya MUNGU ,umri wake, rangi yake,n.k.
Ninachojua yupo na anatenda Kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hana jinsia inamaana Mungu sio kiumbe hai kama ilivyo kwa upande wa mawe nk?

Sent using unknown device
 
Ukishasema kua hapendi tuwe na mwisho mbaya hapo unakua umemvua vyeo vya uwezo wote, inamaana naye mungu anakua na desire?? Kwamba kuna vitu mungu anataka vifanyike kwa namna atayopenda yeye ila inashindikana?

Mimi pia sipendi kua maskini, desire yangu ni kuwa kama billget ila inashindikana



Sent using unknown device
 
Wewe ndio umemvua hivyo vyeo mkuu.
Desire za MUNGU NI KUTUTAKIA MEMA.Kwa sharti moja la kufuata sheria zake na kumtii.Ila hajakulazimisha lakini amekupa tahadhari. Ukuzingatia tahadhari au sheria zake utakuwa na mafanikio.
Option ya kumwabudu au kutokumwabudu Ni wewe na Mimi kuamua wapi tushikilie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo mungu shauku yake ilikua nikututakia mema ila alishindwa?

Sent using unknown device
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…