Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 56
Pundamilia07,
Mkuu yote sawa...nimepiga simu ofisi ya British Airways hapa wamenambia ticket wana issue ONLY to Dar - Tanzania..siwezi kufikishwa Mwanza kwa sababu hakuna member wa timu yao anayekwenda huko...
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na connection kanambia wanaweza tu kunisafirisha ikiwa kuna mashirika ambayo ni franchise yao, ni codeshare partners wao pia kikubwa zaidi ni member wa network ya ushirikiano (Airlines Allience) ambayo shirika linatakiwa kuwa member au subsidiary wake kunifikisha Mwanza..Sasa sielewi kinachoendelea kama kanifunga kamba sijui lakini majibu yake ndio hayo siwezi kupata ticket moja hadi Mwanza - Tanzania.
Ni wazi kabisa hayo maelezo sahihi kwani nilichoandika ndiyo sahihi na wala hakihitaji nyongeza. Lakini pia inategemea jibu ulilolipata lilitokana na swali gani ulilouliza. Anyway let me give you benefit of doubt kwamba BA hawezi kukata ticket kwa sector ya Mwanza kwasababu ATCL imesimamishwa uanachama wa IATA, lakini pia siyo sababu kubwa sana ya kufanya abiria asifike Mwanza, kwani katika reservation system Precision Air mwanachama wa IATA anakwenda Mwanza. Kama nilivyosema hapo juu kuwa majibu hutegemea na swali lilivyoulizwa.
Mkuu, hizo hesabu za asilimia 70 ya wasafiri wa ndege kwenda nje unafikira nimetunga!..Hata hivyo haiusiani kabisa na ATCL isipokuwa ni hesabu ambayo nimeipata toka chombo cha serikali hivyo siwezi kuiweka kama unavyodai kwa sababu sikuipata toka site fulani..
Nachokuomba chukulia kuwa ni kweli
Takwimu ni kitu muhimu sana hasa pale tunapojenga hoja. Kama nilivyoandika hapo awali kwa vile source ya data hizo ni 'unknown' siweza kuzikata wala kuzikubali.
na jaribu kuangalia jinsi gani ATCL inaweza kufanya kazi zaidi kwa kushirikiana na mashirka kama Emirates kwa sababu nilizoandika mwanzoni..USHIRIKIANO . Iwe kwa kununua hisa, iwe kwa Ubia, iwe kujiunga na Allience yote kwangu ni sawa maadam tunaweza kusafirisha abiria wetu toka Mwanza< Bukoba moja kwa moja kwenda nje with a connection Dar au Kili..
Mkuu wangu Mashirika yote makubwa duniani mbali na ku run international flights yana mashirika madogo yanayo run ndani ya nchi zao iwe Uingereza, France, Japan au America na kuna ushirikiano kmkubwa kati ya shirika mama (International) pamoja na hilo la ndani (Local).. huwezi kuchukua Air Canada kuja Toronto au Vancouver ukaunganisha na shirika lolote la ndani ati maadam kuna ndege inakwenda huko..
Ushauri wangu juu ya hili ni kuwa ukombozi wa ATCL hautategemea kujiunga na mashirika makubwa, kinachotakiwa hapa ni ATCL isafishe nyumba yake na kujenga uwezo kwanza wa soko la ndani na Region kabla haijajiingiza kwenye International market. Wakiweza kufanya vema kwenye soko la ndani na Region then watakuwa attractive kiasi cha kuweza kuwavuta washirika wakubwa kufanya nao biashara. Ikiwa ATCL haijimudu katika soko la ndani sitegemei kama mashirika makubwa uliyoyataja yatakuwa na haja ya kufanya kazi na ATCL. Nafasi ya ATCL kufanya vizuri ndani na Region ipo kubwa sana japokuwa Kenya Airways atampa upinzani usoepukika kwa kutumia tool yake aliyoiweka ndani ya nchi yetu yaani Precision Air.
Hata hivyo, tumeongea vya kutosha na ushauri wangu kwa serikali yetu ni kuliokoa shirika hili lakini badala ya kuliwekea regulations, wakati umefika sisi tuondoe hizo regulations ambazo hazihusiani kabisa na Policies zaidi ya kuwepo mkono wa serikali ndani ya Uongozi wa chombo hicho..ATCL iwe huru (public private company) na viongozi wake WAPYA wapewe nguvu ya kuwa Responsible na Accountable..
Mimi pamoja na kuwa siyo msemaji wa serikali, lakini nia kubwa ya serikali ni kuona kuwa katika nchi hii ATCL inaendelea kuwa mhimili mkubwa au muhimu katika kuendeleza sekta ya anga. Kwa hiyo basi kitendo chochote cha serikali kuiwacha ATCL isiweze kuendelea na shughuli zake ni sawasawa na kujitega yenyewe.
Serikali inataka kuwa na Airline ambayo itakuwa profitable na ikibidi hapo mbeleni serikali ibakize hisa chache tu na kuwacha sehemu nyingine imilikiwe na strategic partners na umma kwa ujumla. Endapo ATCL itakuwa katika misingi mizuri ni wazi kabisa faida zitokanazo na uwepo wake ni nyingi na zenye manufaa kwa taifa kuanzia employment, utaalam kwenye sekta hiyo, kodi za serikali nk.
Serikali kama mwenye hisa 100% ni wazi ndiye mwenye kauli ya mwisho na hatima ya ATCL kwa hiyo kama ilivyo kwa mwenye mali yeyote ana uamuzi wa kufanya lile ambalo anaona lina manufaa kwake. Haitakuwa rahisi na sawia kuikataza serikali isiisimamie ATCL ilhali yenyewe ndiyo mmiliki wake na inataratibu zake za kuendesha mambo yake. Kama imeamua kuunda tume, basi hayo ndiyo matakwa yake, cha msingi ni kuangalia hii tume imeagizwa nini. Kwa maoni yangu binafsi terms of reference za tume ni sahihi na tume kuwepo pia ni sahihi. Ni vizuri tupate kujua inside ya matatizo ya ATCL zaidi ya haya ambayo tunayajua, tuvute subira tutoe maoni yetu na nina hakika tume inayaona na kuyapima kwa uzito wake kwa maana na wao pia katika utendaji wao wanasikiliza public reactions.
Mengi nilikwisha andika huko nyuma ni jinsi gani ninaona inafaa kufanyika juu ya kuiunda ATCL mpya mnaweza kurudia kusoma na kuchangia pale mnapoona inafaa.
Bottom line ni kuwa ATCL ijengwe na kuendeshwa katika misingi ya biashara ilivyo sasa na wala si katika hali ya kufikirika.
For more information unaweza kunipata katika pundamilia@rocketmail.com
---------------------------------------------------------------------
Last edited: