Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
Mkuu Mkandara,
nimekuoata maelezo yako, lakini ukweli ni kwamba ATCL kama ilivyo sasa haina mvuto kwa wanunuzi hasa katika mfumo wa hisa. Watu wanaponunua hisa wanatarajia kupata dividends kutoka kwenye faida itakayotengenezwa. Sasa ukiangalia ATCL haitengenezi faida zaidi ya hasara, kwa mantiki hiyo hata ukisema uzipenyeze kinamna-namna pale kwenye soko la hisa hakuna atakayeweza kuzinunua kwani kwa ukizinunua maana yake utapata hasara na kama mtaji kako katakwenda na maji.
Kitu ambacho kinaweza kufanyika ni mwenye mali sasa hivi kwa maana ya serikali kutafuta mbia ambaye watajumuika kuiendesha ATCL endapo serikali itaona haiwezi kubeba mzigo wa risk at 100%.
Baada ya hapo endapo kampuni itaanza kutengeneza faida kutoka katika operations zake (Operating Profit), kuweza kuonesha kuwa kunauwezekano wa faida kuongezeka na kuimarika kifedha nk, then
hapo hisa zake zitaweza kupanda thamani na kuuzika.
Au njia nyiingine ni serikali kubaki peke yake na kufanya mikakati ya kuliimarisha na hatimaye kufikia kiwango cha kuridhisha kuweza kupata faida nk kama nilivyoainisha hapo juu.
Au njia nyingine serikali kuiuza ATCL kwa mmiliki mpya, lakini katika hali ilivyo sasa ATCL atakayenunua ndiye atakaepanga bei.