How Air Tanzania Should be Restructured | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

How Air Tanzania Should be Restructured

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lee, Jan 6, 2009.

 1. l

  lee Member

  #1
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Reducing Staff by a half
  2. Review contract to all suppliers
  3. Advertise CEO to local and international newspaper
  4. Return A320 to lessor
  5. Lease 70 seater Dash 8 - Q400 ( for fleet commonality)
  6. Concentrate on Domestic Market on IATA summer schedule
  7. launch international destination on Winter Schedule
  8. Train local crews to Dash 8 qualification
  9. Close regional offices - focus on GSA
  10. Interline with other Airlines for feeding
  11. Resolving technical issues required by IATA for these 3 months
  12. 2 Dash 8 - 300 goes major C check maintanace

  Summer Schedule effective from 29 march
  Morning Departure Bank

  DAR MZA 06:30 Q400
  JRO 07:00 Q300
  ZNZ 08:00 Q300

  Afternoon Departure Bank

  DAR MTY 11:30 Q300
  ZNZ 11:40 EQV

  Evening Departure Bank

  DAR MZA 14:30 Q400
  JRO 14:30 Q300
  ZNZ 14:40 Q300


  DAR ZNZ 17:40 Q300

  This will allow inter city connectivity and maximum fleet utilisation


  Will it be profitable?

  What is your opinion?
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  I tend to agree with almost all that Lee is suggesting except for the Internatinal destinations I would suggest ATCL should only venture internationally after consolidating the domestic market. The government should know that the main problem facing ATCL is not the inadequate capital injection by the shareholder but also the lack of managerial capacity to run the Airline. Yuo can pump as much money as you wish, but with the current management you will never succeed; this is an undisputable fact which the powers that be must accept!!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kbla hayajafanyika hayo yote, kwanza Mattaka na watu wake waondolewe, iwekwe menejiment mpya na kisha idadi ya wafanyakazi ipinguzwe kulingana na idadi ya ndege zitakazokuwepo
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180

  Ningeomba wahusika waje kwanza mtoni na waangalie business model ya Southwest Airlines.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na haya yote; lakini kwanza ningeona serikali iuze hisa za ATCL kwa Watanzania au mashirika ya kitanzania ili iendeshwe kibiashara na umiliki uwe mikononi mwa watu wanaojali faida inayotokana na huduma nzuri.
   
 6. K

  Koba JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..acha ife tuu na wanaojua biashara za ndege,high quality service & profit oriented ,capital za kutosha bila ubabaishaji watafanya kazi na wapo wengi tuu,serikali iwekeze kwenye strong regulating bodies kama safety,high standard of services etc na iwekeze kwenye kujenga Airports
   
 7. s

  skasuku Senior Member

  #7
  Jan 6, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo umesema la maana. Hawa Southwest Airlines ndio wakongwe/waanzilishi wa huduma za anga kwa bei nafuu. Makampuni makubwa mengine ambayo yameiga business model ya hawa SWA ni Easy Jet ya UK, Ryan Air ya Ireland n.k.

  Pendekezo langu ni kwa serekali kuvunja bodi ya ATCL ya sasa, teua bodi mpya, na kabla hawajaanza shughuli yoyote bodi mpya iweze kuja na business plan madhubuti. Kwenda mbele tutaweza judge mafanikio ya hii bodi kutokana na jinsi watakavyo deliver hiyo business plan.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Nami naafiki wazo la hapo juu ni zuri na ukute wana business plan nzuri ila wamekalia chukua twende hakina mwenyewe...maana mataka anarekebisha makosa aliyofanya b4...aibe akitoka anataka ubunge kilosa....
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Im with you. No way the Government can compete in the airline industry, no way!!
   
 10. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Just get rid of that BARADHULI called DAVID MATTAKA and recall shemeji DUMISANE who really knows airline industry....

  Well, if there is a need to sulvage it anyway...

  Tanzanianjema
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji ili kuwauzia hisa wadanganyika ni lazima shirika liwe economically viable!! Wananchi walinunua shares za TOL mpaka sasa hawajafaidika hata chembe! Wazo lako ni zuri , kwanza serikali iliimarishe shirika kama vile ng'ombe unamnenepesha kwanza ndio unamchinja ndio unapata nyama nyingi.!!
   
 12. L

  Lione Senior Member

  #12
  Jan 7, 2009
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya yooote,ni sawa sawia,lakini kuna haya yafuatayo ambayo ni muhimu saana,
  hizo dash8 zao je zina uwezo wa kuhimili mazingira yetu haya?yani viwanja vyetu vya vumbi na changarawe?ikumbukwe kwamba ziliwahi kuletwa maramoja hapo kabla,na zikaproove failure,kwenye haya maviwanja yetu,p
  2:set up ya ofisi yao yaani derpatments zote,na watu wenyewe iko modenized kiasi gani?hapa tunaangalia suala kiufundi zaidi,yaani,kuanzia wataalamu wa billing,pale revenue accounts,wapo skilled kiasi gani,naje wanayo hio billing section?wanawatu wa revenue management(yield management)?na wapo skilled kiasi gani?
  na nikiasi gani hawa revenuemanagement na revenue accounts wanahusiana?
  3:wanatakiwa wawe na contact centre,incase kuna delay,ama cancelation,ili wasafiri wasije tu airport bila kutaarifiwa

  4:eek:peration derpatment set up yao ikoje?maana wanatakiwa wawe na watu skilled hapa kwenye operation control centre,na flight operations,
  5:network planing derpatment yao ikoje?
  hapa nadhani inawabidi wawe makini kidogo,na hapa ndipo wanapoangukia siku zote hawa atcl,
  6:je wastani wa umri wa wafanyakazi,ukoje?maana sehemu kubwa ya wafanyakazi wa atcl ni wazee,sasa hapa kuna tatizo la chalanges,na namna ya kuzitacle,
  naomba kuwakilisha.
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ATCL inahitaji kuwa overhaul kabisa na kujengwa upya. Management ya ATCL iliyopo sasa hivi haiwezi kuleta tija katika biashara hii ya anga kwa wakati huu tulionao. Uwezo wao wa kiutawala na kiuendeshaji katika aviation industry umekuwa ni mdogo ama dhaifu kulikoni mahitaji ya wakati. Aidha, muundo wa management haukujipanga kukidhi haja ya vision and mission ya ATCL as well as strategies. Kampuni inakosa uwezo wa kugenerate reliable information and facts za kuweza kuja na a viable and sound business development plans. Zaidi ya hapo, products za ATCL ambazo zinaingizwa sokoni na zile ambazo tayari ziko katika soko hazikutafitiwa kwa kiwango cha kutosha cha kuweza kuziweka products katika hali ya ushindani na vilevile kuiletea kampuni faida. Kana kwamba haitoshi equipment utilization haioneshi usahihi wa kutumika katika kiwangi ambacho kinaridhisha kwa maana kulinganisha na mapato dhidi ya soko.
  Inawezekana kabisa leo hii ukitaka kujua beak-even ya route kama ya Dar - Mwanza per equipment sijui kama inaweza kupatikana ikiwa ni sahihi.
  In short, nobody knows what's going on katika kampuni japo kuwa wakuu wako busy na wanakwenda kazini kila leo. Udhaifu huu katika management hauwezi kurekebishwa kwa kuwaacha wahusika waendelee kubahatisha, la hasha mikakati ya kweli lazima ifanyike. Biashara ya usafiri wa anga siyo lelema, ni biashara ngumu inayohitaji umakini wa hali ya juu katika uendeshaji wake. Kila siku ninaamini kuwa pale ambapo tumeona kuna matatizo basi hatujachelewa, turekebishe leo kwani hali ya ATCL iliyokuwa nayo jana ni nafuu zaid kuliko ya leo, kwa maan inaendelea kupata hasara zaidi na zaidi na vilevile kupoteza imani kutoka kwa wateja na wadau wengine.

  Ninaendelea kushauri kama ambavyo nilifanya huko nyuma kuwa:

  1) ATCL ingie kwenye kipindi cha mpito kwa kuweka menejimenti na bodi ya muda. Elevate among the existing workforce ambao wanauzoefu kushika nafasi za menejimenti na iundwe bodi ya mpito pia.

  2) Ndani ya miezi 6, serikali ihakikishe kuwa imempata consultant ambaye atatoa ushauri na huduma ya menejimenti kama ambavyo ilivyoinuliwa Kenya Airways. Kenya Airways iliajiri management consultants nadhani from Speed Wing ya UK ambao ndiyo waliisuka kabla ya kuwaachia wazalendo.

  3) Serikali ikasimu madaraka kwa consultant kuajiri wazalendo (Hapa ninapendekeza Vijana hata kama ni fresh graduates) ambao watafanya kazi kwa pamoja na hao consultants kwa kipindi cha miezi 36 au hadi 48 ili kuwafanya wajenge uwezo wa kufanya kazi katika menejimenti level and at the same time wajenge team spirit.

  Hii timu ya wazalendo ndiyo itakayokuja kuwa chachu ya uendeshaji na kurithisha utaalam kwa wazalendo wengine.

  Ninahakika kuwa katika kipindi ambacho washauri watakuwepo Serikali na ATCL itafaidika kwa kupata utaalam ambao kwa muda mrefu kumekuwa na gap la kupokezana katika kada za kitaalam ndani ya shirika la ndege.

  Vilevile nina amini kuwa kwa mara ya kwanza baada ya kupita muda mrefu sana, ATCL inawezakuwa na mkakati wa kibiashara ambao utakuwa umetafitiwa kitaalam na kuwa na uwezo wa kutekelezeka na kuleta tija.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kuna wakati ATC ilikuwa ktk hali nzuri sana pamoja na kwamba tulikuwa ktk Ujamaa na mnakumbuka ikiongozwa na Mwapachu.. Nadhani ipo haja ya kumweka tena Mwapachu ktk board of Directors ya shirika hilo na kama alivyosema Mwanakijiji, ATC iuze share zake kwa wananchi kupitia soko letu DSE..
   
 15. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #15
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wakuu haya mawazo mnayoyabandika hapa ni mazuri sana.Tatizo wenye mali(serikali) washaamua kuwauzia wachina.
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkandara,

  Nimekusoma mkuu, hali unayosema nzuri wakati huo kwa ATCL ni kwamba ilikuwa ni sehemu muhimu katika kuzalisha wataalam na utaalam wa aviation. Kwa sababu ninakumbuka mipango ya mafunzo kwa wafanyakazi ilikuwa ni across the board Hali hii ilisaidia Tanzania kuwa na wataalam wengi marubani, mafundi, wataalamu wa uendeshaji, mapato, huduma za abiria nk. Lakini mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza kwa ATC pamoja na sera za serikali juu ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma ATC ili-ceased kuwa kitovu cha kuzalisha wataalam. Tatizo la upungufu wa wataalam katika sekta hiyo ndiyo linaloitafuna ATC na nchi hii kwa sasa

  Wazo la kuuza hisa za ATCL ni wazo zuri lakini linahitaji muda muafaka yaani hadi hapo ATCL itakapokuwa profitable na kuweza kutoa matumaini ya kuendelea kufanya vizuri. Sasa hivi hata uuze hisa hiizo kwa Sh.10 nobody will bid kwani kampuni hatengenezi faida.

  Tukitazama upande wa pili wa 'shilingi' Air Tanzania wakati huo iliendeshwa kwa kutumia pamoja na mambo mengine, ilikuwa ni ruzuku ya serikali. Shirika halikuwa likitengeneza faida kutokana na operations zake.

  Wakati wa Marehemu Sanare ATCL ili ripoti nadhani kwa mara ya kwanza au baada ya muda mrefu faida iliyotokana na uendeshaji (Opreting profit). Japokuwa faida ilikuwa ndogo sana lakini ilitosha kuonesha kuwa ATCL ilikuwa inaelekea katika mwelekeo mzuri.

  Wazo la kuwarudisha akina Mwapachu, silikatai, lakini ninashauri huyu Mzee aachwe apumzike, kazi nzuri aliyoifanya ATC inatosha

  Kwa sasa hivi hisa za ATCL haziwezi kuuzika kwa bei nzuri kwani kampuni haitengenezi faida. ATCL inahitaji kuwa profitable na vilevile ni lazima ionekane inaamiinika.
   
  Last edited: Jan 8, 2009
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Iuzwe tu! Mbona waSwiss na waZambia wameweza? Pesa zitakazookolewa ziwekweze kwenye usafiri wa reli! Tuongeze tracks na twende kwenye umeme badala ya diesel.

  Amandla......
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundamilia07,
  Mkuu wangu siku zote unauza share mwanzo wa kujipanua unless ni biashara binafsi.. ATCL ikisha ota mbawa ni vigumu sana kwa viongozi kuachia tena kwani ulaji utakuwa hapo.. kumbuka Watu na Mazingira, utamaduni wa maskini siku zote husubiri mtoto kavunja ungo tu...Kwa hiyo mfumo bora kwa watu maskini ni kutafuta Upatu kisha nguvu ikija patikana serikali haina mkono wake ndani tena..
  Kisha kuna swala la ushirikiano kati ya shirika hili na yale ya nchi za Ulaya.. Ni muhimu kushirikiana na shirika ambalo linatoka nchi yenye kutuletea watalii. wafanya biashara wengi zaidi kwa mwaka.. Yaani hiyo Airline ya nje inawaleta hadi Dar na ATCL ni kazi yake kuwapeleka mikoani.. Nchi kama China ni hasara tupu kwani ni wasafiri wakubwa ni Watanzania wenyewe from Dar to Shanghai wakirudi nchini wanaishia JKN Airport.. ATCL haina kitu sawa na kutumia jina la Hard rock cafe wakati unauza safari na Kilimanjaro beer!
  Pili naona Fundi Mchundo kasema Uza tu, sijui kama anaweza kunipa data zaidi kuhusu Zambia na Uswiss..Zambia wameuza shirika lao au ndio ktk bankruptcy!..
  Nakumbuka Sabena, serikali ya Ubelgiji walikubali kushindwa wakauza basi ndio kifo cha shirika hadi leo tokea wameuza shirika hilo cancer haiishi..wanajutia ku give up!.. hakuna nchi duniani ime give up kwa usafiri wa ndege no matter how big is the competition..
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....nchi nyingi zilizoendelea hazina National airline,ni private companies tuu na mojawapo ni States na usafiri ni first class,huko Belgium sijui kama wana tatizo la usafiri wa ndege kwa ajiri ya kufa sabena,Precision ni private company lakini huduma zake kwa sasa ni nzuri kuliko hao ATCL ambao wanabebwa kuanzia kwenye policy mpaka financing,wape Precision playing field ya ATCL bila hata cent uone kazi...hivi tunataka National airline au usafiri mzuri kwa wananchi bila kujali ownership?
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Koba,
  Mkuu nadhani hujanisoma vizuri.. nimependelkeza ATCL kuuza hisa kwa wananchi ktk soko letu yaani iwe Public company... na kwa lugha ya kibongo ndio private company hivyoo. US wana mashirika mengi sana ya ndege kiasi kwamba sio swala la cha ngama na nakuhakikishia huwezi kuona wanauza nje unless nchi ambazo wanashirikiana au kubadilishana Innovation Technology nchi kama UK na Germany kwa sababu sasa hivi ushindani ni mkubwa sana kutoka Asia. Siku zote wanajua kina nani Allies au adui yao kibiashara.. We don't!
  Tanzania tukiwauzia China hiyo ATCL unafikiri unaweza kunipa mfano wake kibiashara, madai ya private co ikiwa hakuna tofauti na mkoloni alivyokuwa akiendesha Ukoloni Afrika - sehemu ya kuja chuma..Kweli
  Private company means Private people not Government owns the company lakini ukiangalia sheria zao za kufungua shirika private kama hilo kwa wageni utaona milango imefungwa na nafasi finyu sana imetolewa kwa wageni..Sisi mapazia wazi, milango waiz na madirisha wakati nyumba yenyewe hata dari haina..Palepale bob - watu na mazingira..

  Shirika kuwa Private company haina maana zaidi ya kuondoa mkono wa serikali lakini mapato yake yanazunguka ndani na pia kodi yake ambayo ndio muhimu shirika linafanyiwa registration ya makao makuu ndani ya nchi yetu..

  ATCL ni mali ya Tanzania na inatakiwa tujivunie kiuchumi kama vile Marekani wanapojivunia mashirika ya magari Ford, GM na kadhalika kuwa ni American brand kwa sababu ndiko wanakochuma...Hata shirika kama North west Airline NWA walipo file chapter 11 wamejaribu weee hadi imefikia kuuza kununuliwa na shirika la ndani Delta ambalo pia lipo ktk soko lao...
  Bila shaka tunatakiwa ku move out of Government control lakini inatakiwa kuwepo uwezo kwanza wa kufanya hivyo taratibu serikali iuze share kwa wananchi hadi hapo tunakapoweza kujitenga kabisa na serikali sio kukurupuka na kuuza nje share zetu..Trust ATCL itakuwa a foreign company na watapewa msamaha wa kodi ambazo ni muhimu kwa maendeleo yetu.. Hii ni biashara mkuu inabidi tuanze kufikiria biashara kwani Ubepari hautowi mwanya kwenye makosa..

  Tumeyaona kwenye madini sasa mnataka kurudia makosa yaleyale. Precision Airways ni ya mtu mmoja ambaye kesho anaweza kuamua akafunga au kuiuza kwa mtu yeyote it's not a public property..Kutoa mfano wa services zake hiyo mkuu ni cheap shot kwa sababu ATCL kama shirika ipo ktk hali mbaya kiuchumi kutokana na makapa shume ndani ya Uongozi wa shirika na serikali yenyewe. Kwa hiyo matatizo ya Uongozi yasitumike kabisa kuliadhibu shirika zima kwa kutumia mfano wa Precision hali viongozi wa ATCL wakihashiwa Presicion wakatumia mfumo wa uongozi toka ATCL matokeo yake Precision itakuwa another ATCL..Tuwe wakweli ktk kukubali makosa yetu badala ya kunyooshea kidole shirika.
  Kuna uwezekano mkubwa wa ATCL kufanikiwa ikiwa itakuwa privatized in a sense of a Public company (kuuza share kwa wananchi)...Merger na mashirka kama Emarites au Gulf Air ni wazo zuri pia kwani nafikiri ndizo ndege zenye kusafiriwa sana na wakazi wa nchi za Afrika mashariki na kati.
   
Loading...