Pundamilia07,
Baadhi ya mashirika ambayo umeyataja (with exceptional ya SABENA ambayo haipo tene) yanasafirisha abiria wao kuja Tanzania bila ya kuhitaji kuleta ndege zao. Utaratibu wa usafirishaji abiria wa ndege upo katika levels tofauti. Airline ya Pakistan inaweza kuuza tiketi ya Karachi - Dar na kumkubeba abiria kutoka Karachi hadi Dubai then kwa njia ya Dubai - Dar career anaweza kuwa Emirates (Si lazima Airline ya Pakistan iwe na ushirikiano wa moja kwa moja na Emirates). taratibu zinazotumika hapo ni zile za IATA.
Kwa hiyo basi kutokuja kwa Ndege zao hakuna maana yeyote zaidi ya mikakati yao ya kuendesha airline hizo kwa ufanisi.
Mkuu samahani ni wewe ambaye hukunisoma vizuri..maelezo yako hayo hapo juu ndiyo kitu nalichozungumzia muda wote huko nyuma.. Kisha sio sheria za IATA kubadilihana abiria mkuu hata kidogo ni mikataba baina ya mashirika mawili kuhusu usafirishaji wa Abiria. iwe kuna Ubia ama makubaliano ya contracts..Naelewa fika kwamba mashirika yale yote hayafiki tena Tanzania lakini abiria wake wanakuja na mashirika mengine tofauti na wakati wa Nyerere..Lakini mkuu wangu my point is, huwezi kusafirisha abiria wa shirika fulani wakati fedha imelipwa nchi nyingine ni lazima kuna makubaliano kati ya mashirika mawili jinsi ya kugawana mapato ya msafiri mmoja aliyesafiri kwa ndege mbili za mashrika mawili tofauti..Na sio swala Huo ndio Ubia naozungumzia mimi, na sielewi unaposema Emirates wangekwisha nunua hisa ikiwa ATCL sio public sokoni, hizo hisa watazinunua vipi ikiwa hujapeleka mali yetu sokoni? ..
Mkuu Emirates wanahitaji abiria zaidi toka Tanzania ikiwa kuna uwezekano wa kuvunja masoko ya ndege nyingine zilizobakia..tunaweza kuwa regional (Tanzania) partner wa Emirates with our goals being connection Tanzania and the world, na wanaweza tu kukunua hisa pale tutakapo tangaza kuwa Public soko letu DSE..Kitu muhimu kwao ni soko, vitu kama
Ebu wewe nambie mkuu wangu kam Unaishi Mwanza na unaweza kuapata ticket ya kwenda London bila kuja Dar utaacha kusafiri na ATCL toka Mwanza kuja Dar au Kili na kuunganisha na Emirates?.. Je ni Watanzania wangapi watakao penda kufanya hivyo (air of their choice) badala ya kuja Dar kutafuta ticket za BA, KLM au Swiss Air ambazo hatuna mpango wa kubadilishana nao wasafiri kama ulivyozungumzia hapo juu!
Bila shaka mauzo ya ticket za Emirates zitaongezeka..Emirates hawana haja ya kufahamu ATCL ina mtaji kiasi gani isipokuwa tunaweza vipi kuongeza soko lao nchini.. ATCL itakwenda nchi jirani na kuvuta wasafiri wa Emirates nchi za Asia na Ulaya na pengine hata sisi ATCL kuwa na ndege moja kwenda Dubai kila siku..
Ndivyo mashirika yote yanavyoshirikiana mkuu wangu Ubia unakuja tu kwa kutazama thamani ya soko lililopo, vitu kama Load factor, Revenue, seat miles na kadhalika of which I'm pretty sure tupo juu safi, bearing in mind population yetu na matatizo ya Usafiri mwingine nchini.
Again nitarudia kusema tatizo la ATCL ni UONGOZI mbaya nothing to do with shirika ATCL..soko na mali zake zote ziko safi..Kama vile Tanzania yenye Utajiri mkubwa lakini ndio nchi maskini iloshindikana kutokana na Uongozi mbaya... Potential ipo na ndiyo inawasukuma wawekeshaji kumiminika nchini kwa sababu hatuna tena policies za Ujamaa (mkono wa serikali).. Aliyesubiri kuona Tanzania ikiinuka kwanza would be the looser mkuu wangu..Tanzania itainuliwa na wale walio take risk na ndio watakaofaidika na uwekeshaji wao.. Tukisha pata mabawa tu kila kitu kitakuwa ghali na hakuna tena mwalimu..
Sasa ukifikiria njia ya kuondoka Umaskini huu ni kuuza nchi kwanza badala ya ku deal na main problem utakuwa hujafanya kitu zaidi ya kupoteza kila kitu kama tulivyopoteza madini..Watu walinunua share za Barricks mara tu waliposikia wameshinda mikataba fulani ya machimbo.. kabla hata hawajachimba shimo moja mkuu wangu lakini kila siku zinavyokwenda na utajri kuzidi ndivyo share zake zinavyosidi kuwa ghali kwa wananchi..Hivyo swala la ATCL sio swala la Innovation ni swala la kufuata mfumo uliokuwepo sasa hivi duniani.. mashrika yote unayoyaona ya ndege yalitoka mikononi mwa serikali na kuingia ktk soko huria wakati biahsra ya ndege ilikuwa ikitumba..Watabiri wa wall street hutazama mbele na sio kitu ambacho tayari kinazalisha na risk ni ndogo, faida yake huwa ndogo sana..
Swala la uongozi mbaya ndani ya ATCL ni swala ambalo linaweza kabisa kumalizwa within one month of operating. Wakisha ingia wajuzi wa biashara na kuwekesha fedha zao utaona mwenyewe mabadiliko sehemu zote za uzembe..trust me.
Niliyoaandika kuhusu Nyerere ni kwamba hapakuwepo na makubaliano ya namna hii ndio maana mashirka hayo yote yalileta ndege zao. Sasa uliposema kwamba Ubia kati ya KLM na ATC ulitakiwa toka wakati wa mwalimu ndipo niliposema isingewezekana kabisa kwa sababu mbali na siasa zetu mfumo huo haukuwepo kabisa duniani..sijui kama umenielewa hapo..