House girl kaniandikia barua ya mapenzi

House girl kaniandikia barua ya mapenzi

my dear nilikuwaga hivyo kama wewe ila nilijifunza kufanya bajeti kwa mwez nikaweza. si kazi ngumu kama ukiamua. hata kama una watu wengi kama kwangu.
kuna muda ndani kunakuwa na watu 20 niambie lkn namudu kusimamia bajeti, hela yetu ni ya mawazo sana so huwa niko makin kweli kwenye hili
safi sana mwalimu,
nitakuja kwa somo, lol!
 
Hakuna assurance! Kale uone moto wake utaona nyumbani pachungu and every time utakuwa hesitant wa kuchukua maamuzi when it comes to the two of them mpaka mke wako atajua tu. Yanini kurisk maisha ya ndoa yako na vi mtu vya kupita. Vaa uso wa chuma na ukaambie wewe ni mkuu wa familia na huo ujinga haupaswi kufanyika chini ya paa la nyumba yako

You dont even know who she real is?
 
Yaani ulitakiwa umuite huyo binti na kumwambia kwa ukali ''ulivyoandika hivi una maana gani?umetumwa na nani? uhuni wako peleka huko huko hapa umekuja kufanya kazi. kama huwezi kazi iliyokuleta uondoke haraka sana. Umenielewa binti?'' Halafu mfukuzie mbali.

Ila kama wewe umeduwaa mpaka mida hii, anasoma alama za nyakati na anaelewa utaingia line..I beg you, mkeo yupo kwenye kipindi cha kumleta mtoto wenu duniani, usimsaliti tafadhali.

Na uangalie chakula anachokupikia isije akawa anapika mtupu pia kukuwekea vitu vya ajabu..mtoto mambo yamemzidi umri!!
 
Hakuna assurance! Kale uone moto wake utaona nyumbani pachungu and every time utakuwa hesitant wa kuchukua maamuzi when it comes to the two of them mpaka mke wako atajua tu. Yanini kurisk maisha ya ndoa yako na vi mtu vya kupita. Vaa uso wa chuma na ukaambie wewe ni mkuu wa familia na huo ujinga haupaswi kufanyika chini ya paa la nyumba yako

You dont even know who she real is?

Haka kamtu ni hatari sana, huu ujasiri kaupata wapi? Nadhani ametumwa kuja kunivunjia ndoa, na kesho nakarudisha kwao
 
Haka kamtu ni hatari sana, huu ujasiri kaupata wapi? Nadhani ametumwa kuja kunivunjia ndoa, na kesho nakarudisha kwao

Umenena vyema mkuu! Nyumbani kwako ni mahari pa exercise power! Ukila HG u become so immoral and every time u want talk somebody some sense there is this great guilt that will always haunt you! Give your wife her fully deserved respect at least at home
 
Hapo kabinti kana undugu na Lulu kitabia.
Kuwa makini yasije yakakukuta ya Kanu....
 
Ila kama mkeo kaandikiwa kujifungua normal nfikiri hakuwa na haja ya kwenda kwo tena mkoani na huku ana house gal, matokeo yake ndio hayo ndoa inaaza kutegwa... Mimi mume wangu ndio alinikanda maji, house gal alinipikia na mtoto tulisaidiana na mume wangu kumuogesha
 
Hahahahahahahahahahahah!...
Mkuu mwenzetu ameshachanganyikiwa,wewe unamwambia ampeleke shule tena,akimpa umeneja aambiwe kampa cheo mwanafunzi?...
Hii imekaa kama bongo movie hivi lol

but hongera kwa kuzimikiwa na housegirl...

Ushauri wangu kama umeshtushwa kweli basi mpeleke shule huyo mtoto..
miaka 16 anastahili kuwa shule....
 
siwezi toka kwangu nikajifungulie home, uvivu tu, tena na hg yupo? Akandwe kawa unga wa maandazi?

Umekula bingo, mle hg, ptuuu!

Couples nyingine zinaboa sana...

Mke wangu aende kujifungulia kwa sababu ipi ya msingi?

Anyway, cost yake ndo kama hiyo ya kuhashuliwa na beki 3!!


rafiki kwa kuongezea hapo kwenye bongo movie, kama siyo yenyewe basi huo ni uzembe wa baba.........
inakuwaje hg akawa na guts za kukuandikia barua ya mapenzi baba mwenye nyumba?
ameanzaje kwanza........
na anakuhakikishia hatamwambia mkeo.......yaani kaona possibility ya kukataliwa ni almost 0
sijui labda aje mzee mzima Dark City anifafanulie hili kwa ile lugha yetu ya watu wa kale.....
na wewe rafiki inabidi ule uzi wetu urudi hapa kwa lugha mbali mbali........ mimi najitolea kutafuta wakalimani wa kila kabila

Eti nini?

Thubutu....Haiwezekani hata kwa dawa....

Wengine hata maboss wanatuogopa, sembuse beki 3?

Kuna mtu alishasema kuwa ni hatari kuwa na mwanamume aliyejilegeza kama ngozi ya yale machungwa mawili ya uzima!!

Babu DC!!
 
Ha haa haa alikuwa anakula vichwa sio?

siku hizi unaletewa housegirl ana Blackberry ....huku mkeo ana Nokia tochi...
housegirl asubuhi anakwambia ' maambo uncle'?
huku kavaa ki pedo lol

kipedo?house anakugongea kanga moko ndembendembe
 
  • Thanks
Reactions: awp
hata simba kuna wakati huogopa pori, ila ukimrudisha kwao kiambankumbe itasaidia kidogo vi-beki 3 vimejaa kibao mjini hapa vyenye staha
 
Wife yuko mkoani kwa ajili ya kujifungua. Tuliamua aende huko kwa kuwa ni uzazi wake wa kwanza na hapa mjini hatuna ndugu wa kuweza kusaidia mambo ya kumkanda, kumpikia na huduma nyingine kwa mama mzazi.
Akiwa anajiandaa kuondoka, tuliletewa kasichana kadogo ka kazi umri miaka 16.
Kwa kweli sina mazoea nako na muda mwingi niwapo home nautumia kufanya kazi zangu za ofisini.
Leo asubuhi nilimwambia mtoto aniandikie orodha ya vitu tunavyohitaji kwa matumizi ya nyumbani.
Muda huu ndio binti kanipa hiyo orodha ili kesho nikafanye shopping.
Nimeipitia list, na nilipoguza ukurasa wa nyuma ndipo nkakutana na hiyo barua ya mapenzi.
Binti kaanza kwa kunisifia, akamaliza kwa kusema yuko tayari kuwa mpenzi wangu, na anasema tufanye iwe siri mke wangu asijue.
Anadai atahakikisha anamheshimu na kumtii mke wangu.
Hapa nilipo nimechanganyikiwa, maana katoto haka ni kadogo sana sijui ujasiri kameuptata wapi?

Mjanja mmoja ameni-tag uzi huu sijui kwa nini, nimeusoma ila nimejifunza kitu kimoja toka kwa wachangiaji.

Wenye haki yao wako makini na wanatoka povu jingi sana hapa, huenda wengine ni majeruhi wa hii kitu, nampongeza mleta mada maana michango ya wengi ni darasa kwa ulimwengu.

Jambo moja ambalo nimelisoma na ninafikiri ni sahihi ni pale namna unavyojiweka, kwani unaweza kujiweka kwenye mazingira ya kumfanya housegirl aamue kutumia mbinu za kujiachia kujiuuza kwako. Lakini kama mtu umekuwa na madhari ya kuonekana baba kwake na mipaka unayomwekea ni heshima utakayopata toka kwake na kinga yako mwenyewe.

Mengi hufanyika sababu ya kujiruhusu kuwa legelege. Unawezaje kumwagiza housegirl tena mgeni tu amefika karibuni baada ya mkeo kwenda jifungua huko ukweni? Umempa kichwa kuwa mmoja mwenye nafasi katika nyumba la sivyo usingemwambia aorodheshe matumizi ya ndani ya nyumba maana matumizi ndani ya nyumba hujumuisha:
  • Matumizi ya jikoni
  • Matumizi ya chooni
  • Matumizi ya vyumbani
  • Matumizi ya Master bedroom
Iweje umpe housegirl jukumu la kuandika matumizi ya nyumbani ambayo pengine yanajumuisha vyumba nyeti ambavyo hapaswi kuwamo? Binafsi siwezi kuruhusu housegirl akifahamu master bedroom, kwa sababu huko ni secrets za nyumba yetu. Huko mama ni jukumu lake, kama hayupo kwani vigumu mwenyewe kushughulikia chumba kimoja?

Sababu za mke kwenda kujufungua huko kwao kwangu hazina uzito, kwani wengi tu wamejifungua hospitalini na kurudi majumbani kwao huku wakiendelea na mambo ya kawaida na kulea mtoto. Hayo ya kwenda huko vijijini ni mambo ya zamani sana. Mbona rafiki yangu mke wake kajifungua, anachofanya arudipo home ni kumsadia mkeo shughuli mbalimbali hadi arudie nguvu zake lakini kwamba ukweni kuna kukandiana kwani wanajua zaidi kuliko madaktari wa hospitalini?
 
Unaajiri watoto wa chini ya miaka 18 ..wewe ni mtu hatari sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
my dear nilikuwaga hivyo kama wewe ila nilijifunza kufanya bajeti kwa mwez nikaweza. si kazi ngumu kama ukiamua. hata kama una watu wengi kama kwangu.
kuna muda ndani kunakuwa na watu 20 niambie lkn namudu kusimamia bajeti, hela yetu ni ya mawazo sana so huwa niko makin kweli kwenye hili

Jeuri ya watu kujaa nyumbani kwako ni kuwapa kazi, just buni miradi wakusaidie kuzalisha na wavivu watakimbia wenyewe. Lakini usimtese ndugu yako kwani damu nzito kuliko maji.
 
Back
Top Bottom