Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
Nitoe duku duku kwenye swala moja. Rais anasema tuiachie Wizara ya Mambo ya Nje na serikali kuamua tujiunge na OIC au hapana. Yaani tusitoe maoni yetu.
Sasa wanataka kutumia maoni ya nani kama si haya tunayotoa sisi Watanzania? Serikali inatakiwa kufanya maamuzi yake kutokana na maoni ya Watanzania. Wakati mwingine inabidi hata kuunda kamati ya kukusanya maoni hayo.
Ni UTAFITI kuhusu nini anafanya Ndugu Membe? Si alishatoa maoni yake? Kwa nini Rais anataka tukae kimya?
OIC ni (Organisation of Islamic Countries) Umoja wa Nchi za Kiislamu. Sisi sio nchi ya Kiislamu. Hata kama kuna nchi ambazo sii za Kiislamu zilizoamua kujiunga na OIC, si sawa kusema na sisi tujiunge. Two wrongs do not make a right.
Kama nilivyosema siku za nyuma, ni maoni yangu kwamba JK ameamua siku nyingi kuiingiza Tanzania OIC. Sasa anatafuta tu njia za kufanya hivyo. Kusema tusilizungumzie hilo swala tuiache serikali ni mbinu mpya, lakini ni mbinu ya ajabu!