Hotuba za Rais kila mwezi

Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Jamani nimeangalia na kusikiliza hotuba najiuliza amesema nini huyo jamaa?????Can someone explain plseeeeeeeeeee????Nimeona ma Rais lakini wasasa kiboko, du!!!!!!

it's beyond explanation....

the same bongo you have known for ever .... usanii to the bones
 


Miaka 15, wizara ya nje bado inafanya utafiti, Membe amemaliza utafiti lakini hajaiarifu serikali, lakini ameamua kuwaarifu wananchi,

You are right.

Ndio maana Kikwete mjanja kasema "nijuavyo mimi Wizara haijamaliza."

Yani hata Kikwete mwenyewe, Rais wa Jamhuri, hana uhakika kama Waziri wake, Membe, kamaliza.

Nobody knows squat in this country. And you wonder why the press doesn't know jack squat. I mean, the President himself doesn't know squat.

Maybe things are just unknowable in this country.

Or maybe there is just nothing to know!!
 
halafu eti tunashangaa kwa nini nchi haiendelei!!!!!!!!!!!!!
 
Nimeona ma Rais lakini wasasa kiboko, du!!!!!!

Unashangaa,haya mavuno alipanda mbengu MWINYI,sasa watz tunalazimika kura,,,hata kama za moto.

Wadugu tumrudishe MKAPA kitini nini?au Salim Mwarabu?
 
Na. KLHN News

Rais Kikwete amezungumza na Taifa katika utaratibu wake wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi. Hotuba yake hiyo iliyocheleweshwa ka karibu saa moja na nusu ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na wananchi hasa kutokana na uzito wa mambo ambayo Rais alitarajiwa kuzungumzia.

Akizungumza katika hotuba hiyo ambayo ilionekana kuwa imerekodiwa Rais Kikwete alizungumzia mambo makubwa manne ambayo aliyatolea maelezo kwa kirefu. Hata hivyo jambo kubwa ambalo wananchi wengi walikuwa wanasubiri kulisikia ni hatua zilizochukuliwa dhidi ya makampuni na watu waliohusika na wizi wa fedha za EPA na kujua hatima ya uchunguzi mzima.

Pamoja na hilo suala jingine ambalo wananchi walikuwa wanasubiri kwa hamu ni msimamo wa serikali yake kuhusu suala ambalo linaonekana kuwagawanya wananchi kwa misingi ya dini. Suala hilo ni mpango wa Serikali ya Muungano kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC)

Akizungumzia suala la OIC ambalo alilipa umuhimu wa kwanza Rais Kikwete alisema kuwa mjadala wa OIC jinsi unavyoendeshwa sasa hivi ni “mjadala usiofurahisha”. Akielezea zaidi kutokufurahisha kwa mjadala huo Rais Kikwete alisema kuwa mjadala huo una “sura ya malumbano baina ya waumini wa dini zetu kuu na kupandikiza chuki baina ya serikali”

Kwa mujibu wa Rais msukumo wa kujiunga na taasisi hiyo zaidi unatoka Zanzibar ambayo ilikuwa imejiunga mwaka 1993 na kulazimika kujitoa miezi saba baadaye baada ya pingamizi toka serikali ya Muungano. “Tangu wakati huo Zanzibar wamekuwa wanasubiri uamuzi wa Serikali ya Muungano. Kila wakati wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa wanaliuzia suala hilo.”

Hata hivyo akionekana kutofautiana na Waziri Membe Rais Kikwete alisema kuwa hakuna utafiti uliofanyika kuhusu suala la OIC na hivyo serikali bado inasubiri utafiti huo toka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje. “Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haijakamilisha kazi yake ya utafiti na hivyo haijawasilisha Serikalini matokeo ya utafiti wao pamoja na mapendekezo yao kwa ajili ya kutafakariwa na kuamuliwa ipasavyo.”

Hata hivyo kauli hiyo ya Rais inapingana na kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe. Bernard Membe akizungumza Bungeni Augusti 22, 2008 ambapo akizungumzia suala la OIC alinukuliwa kusema kuwa “sasa tumefanya utafiti wa kutosha na kugundua kuwa OIC ina faida kwetu na haina madhara, hivyo tunafanya mchakato wa kujiunga, lakini ni vema ikaeleweka wazi kuwa, Zanzibar wasingeweza kupata ridhaa ya kujiunga nayo kwa sababu si nchi katika uso wa kimataifa,”

Ni kauli hiyo ya Waziri Membe ndiyo iliyosababisha wimbi la shutma na malalamikko ya Taifa kuburuzwa kwenda kujiunga OIC na wakati huo huo kupata pongezi kuwa wakati muafaka umefika wa kufanya hivyo kwani “utafiti” tayari umeshafanyika.

Rais alielezea msimamo wa serikali kuwa “Serikali haijafanya uamuzi wowote kuhusu suala la OIC kwa vile hatujapokea mapendekezo yoyote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.”
Rais amewataka wananchi wawe na subira.

Kuhusu suala jingine ambalo limekuwa mwiba kwa serikali Rais Kikwete ameeleza kuwa kufuatia hotuba yake ya Augusti 21 aliagiza makampuni yaliyolipwa bilioni 90 kuhakikisha yanarudisha fedha hizo na yale ambayo yatashindwa kufanya hivyo yatachukuliwa hatua.

“Leo ndiyo siku ya mwisho. Napenda kuwajulisha kuwa, taarifa nilizoletewa majira ya mchana leo(Ijumaa), ni kuwa kiasi cha shilingi 69,326,437,650 kati ya shilingi 90,359,078,804 zilikuwa zimerejeshwa. Hii ni sawa na asilimia 76.7.” alisema Rais.

Aliwaambia wananchi kuwa leo (Jumamosi) taarifa zaidi itatolewa kuhusu “kiasi” halisi kilichorudishwa. Kutokana na kauli yake hiyo inawezekana hesabu hiyo isiwe sahihi. Wachambuzi wa suala hili la EPA wanaonekana kushangazwa na Rais kutaja namba ambayo siyo sahihi na masaa machache baadaye iliyo sahihi itolewe.

Kuhusu wale ambao hawakuitikia wito huo Rais Kikwete alisema kuwa ametoa maagizo kuwa “Kamati (ya Mwanasheria Mkuu) ikabidhi majalada yao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka mara moja, kwa hatua zipasazo za kisheria.” Agizo hilo alilolitoa Rais ni sawasawa na agizo alilolitoa wakati wa kuunda tume ya Mwanyika pale alipomuagiza Mwanasheria Mkuu “kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu na makampuni yote yaliyohusika na uhalifu huu”. Haijaeleweka tofauti ya uelewa wa Agizo hilo la kwanza na la pili ni nini hasa kwa sababu ofisi ya DPP iko chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Uamuzi huo unahusu makampuni yale 13 kati ya ya 22 yanayohusishwa na wizi wa EPA. Kuhusu makampuni 9 yaliyosalia ambayo yanadaiwa kulipwa bilioni 40 Rais Kikwete alisema kuwa “nasubiri taarifa yao mpya kuhusu maendeleo ya uchunguzi huo. Taarifa niliyopewa wiki mbili zilizopita zinaonyesha kuwa polisi wetu bado hawajapata majibu kutoka kwa wenzao
katika nchi walizoomba msaada. Hivyo, nakusudia kuwataka waendelee kufuatilia kwa wenzao ili hatua zipasazo ziweze kuchukuliwa.”

Kwa maneno mengine uchunguzi kuhusu makampuni hayo bado haujaanza kwani Rais ndiyo amekusudia “kuwatataka waendelee” kufuatialia makampuni hayo 9. Makampuni hayo ni pamoja na kampuni inayodaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz, ya Kagoda Agricultural.

Hata hivyo Rais aliwahakikishia wananchi kuwa utaratibu wa kuzigawa fedha hizo kwenye sekta ya kilimo Umekamilika.

Mambo mengine ambayo Rais aliyazungumzia kwa kirefu ni pamoja na suala la madai ya walimu, mauaji ya Albino, na suala hali ya kiuchumi ya dunia


Mbona hujatoa chanzo chako cha habari babu?..au KLHN News mlitumiwa copy ya hotuba?..

Mbongo mbongo tu.
 
Ningependa kujua majina ya hizo kampuni 9 ili tumsaidie uchunguzi.

Hakuna cha kampuni tisa wala nini, tunajua hiyo 43 bilioni ndio hela zilizopelekwa CCM kwenye uchaguzi according to rostam & Co.

Kwa hiyo hakuna cha uchunguzi wa Nje wala nini.

Rais huna haja ya kuwasumbua vijana wenzetu walioshindwa kulipa hizo bilioni 21, waacha nao wapete kwanza hela si za serikali ok bwana.

Kama Jeetu hayupo kwenye kesi, pse tupunguzie hasira ili tusahau mambo ya EPA, umeamua noma iwe noma, sawa mkuu wa Kaya.

FREE LUKAZA, FREE MALEGESI.

ndio bangusilo wenyewe hawa eeh?
 
Hivi hamjui kwamba as we now speak Lukaza is in Dubai............. Kumbukeni mkuu alisema wamenyang'anywa pasi
 
Mmhh Lukaza na Malegesi ni wa nani hawa?
kuna ndugu ana jina kama hilo hapa Cuba,mmmmhhh
 
Hivi hamjui kwamba as we now speak Lukaza is in Dubai............. Kumbukeni mkuu alisema wamenyang'anywa pasi



..kama mambo yenyewe ndio haaya bora arudi tu aendelee na kazi..kwani hakuna kesi....kikwete..mwenyewe anatoa hotuba ya leo ana wasiwasi na kuangalia angalia kando..hajiamini utafikiri ameshikiwa bunduki....yaani sielewi kabisa kwa nini rais anakuwa namna hii...sijapata kuona....
 
Sina mbavu hapa! Yaani kuna mtu alikuwa anategemea atasema kitu cha maana? Kweli watanzania tuna hope sana, tungepata kiongozi mzuri tungefika mbali.
 
WATANZANIA TUENDELEE KUFANYA SUBRA SUBRA SUBRA SUBRA SUBRA
Zile kauli za kuwa hivi INAWEZEKANA vile INAWEZEKA.Kwa ari na nguvu mpya
sasa inaonyesha tunaishia kwenye subirabado miaka miwili amalize kipindi chake si tunasubiri nini?mpaka leo? jamani huyu jamaa hana mpango kaaabisa BURE AGHALI
 
Mbona hujatoa chanzo chako cha habari babu?..au KLHN News mlitumiwa copy ya hotuba?..

Mbongo mbongo tu.

well ndiyo nilipata nakala kabla na ungekuwa umeangalia KLHnews.com utaona kuwa taarifa hii ilikuwa kule kabla hujaiona hapa... nilishadokeza vyote atakavyosema.... well you can't fathom that..
 
hajiamini utafikiri ameshikiwa bunduki....yaani sielewi kabisa kwa nini rais anakuwa namna hii...sijapata kuona....

wasomi acheni majungu kwa sana,sisi ndie tulimpigia kampeni JK kwa sana tuu,vuneni mlichopanda.

ooohhhh....malecela hafai...ana...hiki na kile...mzeeee,yeah sasa tunaramba joka..malecela anaenjoy na kutucheka.

ivi tulishindwa hata kumpigia kampeni mwandosya?aaaa


Wito:Mwanakijiji CCM kushindwa uchaguzi ni kazi,ivo basi nakuomba uandae programmu maalumu ya kuhakikisha mwandosya anakubalika for urais 2010.

ni mawazo tuu..
 
Siwezi kushangaa kusikia Chilingati anaaandaaa maandamano ya kupongeza hotuba nzuri ya Raisi Kiwete, Kwa kweli nimechoka kabisa...something need to be done JK ni mgonjwa na anahitaji msaada.

Ushi
 
Siwezi kushangaa kusikia Chilingati anaaandaaa maandamano ya kupongeza hotuba nzuri ya Raisi Kiwete, Kwa kweli nimechoka kabisa...something need to be done JK ni mgonjwa na anahitaji msaada.

Ushi

unadhani ni ugonjwa ndugu, tatizo hapo ni kudesa, tena kudesa onto! angeamua kukaa chini na kuandika hotuba yake mwenyewe, halafu akasaidiana na hao madogo kuedit na kupata input kwa hao mawaziri wake, pengine kungekuwa na tofauti kidogo!
 
unadhani ni ugonjwa ndugu, tatizo hapo ni kudesa, tena kudesa onto! angeamua kukaa chini na kuandika hotuba yake mwenyewe, halafu akasaidiana na hao madogo kuedit na kupata input kwa hao mawaziri wake, pengine kungekuwa na tofauti kidogo!

Mum, nakubaliana na wewe kabisa, last year nilienda pale UDASA, kupata kilegeza koo na kuongea na wahadhiri wa UDSM, bahati mbaya siku hiyo Muungwana analikuwa anahutubia pia....Professor mmoja alisema tafadhali muhudumu badili channel weka channel 5, Kikwete hana cha kuongea namfahamu tokea akiwa mwanafunzi wangu....nilimmuliza vipi kwani jamaa...yule mzee hakuona aibu kusema JK alikuwa ni mtu wa makalai na hata chuo alimaliza kwa kubebwa. Kwa hiyo nakubali kabisa jamaa upstairs ni bure kabisa zezeta, hawezi hata kujua watanzania tunataka nini? yeye ni mizaha ya kikwere tu

Ushi
 
Hayo yalikuwa mazungumzo ya kahawa kati ya Kikwete na washikaji wake pale Saigoni mtaa Livingstone wakisindikiza ubwabwa wa jioni. Mwenzenu bado nasubiri hotuba atakayotoa Raisi wa Tanzania kwa wananchi wake - labda mnambie naishi kwenye ulimwengu wa peke yangu. Acheni mzaha bandugu naenda kulala, akianza hotuba nitamwomba mwanangu aniamshe.
 
Back
Top Bottom